Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

BAADA YA MSIBA KUTOKEA wakati yasemekana huzuni zakinafiki nazo HUHITAJIKA!-...nukuu za MDAU kimuwakilisho!:-(

>> Wednesday, September 14, 2011

 Tahadhari: Najaribu kuyaweka mawazo ya rafiki yangu  kikiswahili aliyekuwa ananiambia kitu kwa ung'eng'e na labda wala sio KIUJINGA BUSARA ambayo ,....
... labda kuna wabishao ndio staili yangu hata ya kumsifia YESU hapa kijiweni!:-(!



Alisema:

Baada ya MSIBA,...
.... hivi ambao hawajafiwa  inahitajika wawe na HUZUNI  za kujilazimisha kwa kuwa watu wazuri ni wale wajibaraguzao  hata kwenye msiba wa JAMBAZI na kudai MAREHEMU alikuwa mtu MZURI?

Mdau nimnukuuyo akaendelea:



Si msiba moja ya maana yake ni MTU kapumzika na LABDA sio kitu cha waliohai kuacha KUISHI kisa mtu KAFA ,...
.... ingawa  ni haki ya WAFIWA KUHUZUNIKA wakifiwa  wakati labda bado jirani yao kiukweli kabisa hahusiki kwenye huzuni hiyo?




Halafu akadai:


Na kwa wasioguswa moja kwa moja na MSIBA ,...
.....hivi  sio UNAFIKI  kujifanya WANAHUZUNIKA wakati  marehemu hawamjui na labda wanahisi pia labda MAREHEMU angekuwa hai KWA WAJUAYE KUHUSU YEYE labda  angekuwa NDIYE  wa kwanza kwa kutowajali WAO hao walazimikao kutokana na presha za jamii kujihuzunisha kisa kuna MSIBA?


Akaendelea :

Na mbona nikitembelea misiba ya WAAFRIKA nahisi kitishacho waafrika wengi ili wahudhurie misiba ya watu na KUHUZUNIKA ni jinsi waogopavyo gharama za misiba zaidi ya  ni kweli wanahudhunika MTU kafa ?

Ndio,...
.... nimnukuuye ambaye ni rafiki yangu sio MUAFRIKA,...
....... na aongeacho kilipandishwa  kwenye madhabahu kutokana na MIE  kuongelea BOMBA LA MAFUTA  lililowalipua ndugu zetu WAKENYA  hapo juzijuzi  ambako ndiko alipo!:-(


Ingawa bado najiuliza kitu,.....
......na  moja ya nijiulizayo hasa kutokana na mambo ya ajali iliyotokea  mpaka TANZANIA kule  ZANZIBAR,..
... ni kuwa HIVI baada ya MSIBA kama huna huzuni ni ushahidi wewe ni MTU mbaya?


Na je kuhuzunika kwenye misiba ya tusiyowafahamu kihivyo ni  maswala ya TAMADUNI  au UTU wakati naamini MAREKANI walipolipuliwa 9/11 kama tu  MV BUKOBA ilipozama  waliohuzunika wengi labda hawakuwa hata na undugu na waliofiwa  na WAKATI hawakufiwa wao wenyewe  ,...
... na ukichunguza zaidi labda unaweza kukuta hao wote WALIOHUZUNIKA hawakutokea katika  TAMADUNI zinazofanana hata kama si WACHINA?


 Swali zaidi KIDUCHU:
  • Si umestukia MISIBANI  watu tofauti huichukulia kitofauti na labda wengine  msiba uleule machozi watatoa baadaye sana wakati wengine WASIFIWAO  wakati  walilotoa ni chozi la kinafiki MSIBANI  labda walisha maliza  kulia na ni fulu kumsengenya kwa waziwazi MAREHEMU??

Naendelea kuwaza,...
... na nakiri MDAU aliyeasili ya TARALILA hii kaniwazisha sana!:-(



...Hebu Peter Tosh arudie- Burial



 Peter Tosh aendelee kivingine ingawa inaweza kuwa ni vilevile  kwa- Why must I cry



Peter Tosh aingizie pia kipengele kwenye - No Sympathy



Halafu ahalalalishe tu kitu tena labda kwa -Mama AFRIKA

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 5:33 pm  

Ahsante kwa kuwakilisha nukuu hii...msiba kusema kweli kila mtu anauchulia kivyake...ila ni kweli kuna wnaohuzunika kinafiki ila nisingependa sana kuongelea kwa undani...

sam mbogo 6:11 pm  

Msiba,ni huzuni. huzuni yaweza kukupata mtu yeyote yule.afe ndugu yako wa damu au rafiki huzuni bado ikopalepale.utamu wa huzuni nipale wa karibu yako anapo kutoka,na hapa kama nilivyosema,rafiki anahusika.kunakitu kina itwa kuguswa,hapa napo husababisha huzuni,watanzania walilia sana alipo fariki sokoine,mmojawapo nyerere.bado najaribu kufikilia huyu binaadamu anaye huzunika kinafiki,inakuwaje,anakuwa katika haligani kibinaadamu,kwani nimuigizaji tu ndiye anawea kuigiza huzuni ya kinafiki,na kukawa na sababu. kaka S.

Simon Kitururu 6:28 pm  

@Dada Yasinta: Ni kweli kabisa ingawa hukumalizia busara.:-(

@Kaka S: Ukifiwa ndio labda hujua ni kwanini kuna kubwazima lijulikanalo kinduli lalia hadharani!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP