Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WASIMAMIZI WA HAKI ZA WANYAMA MPO WAPI?

>> Wednesday, September 28, 2011

Mganga wa Kienyeji Maarufu kama Dr Manyaunyau.
Vijana hawa wakiwa Bara barani wakimzungusha huyu Mnyama aina ya Paka, kwa akili zao wakiamini wamemshika mchawi na wameamua kumsulubisha.
 
 
 
Vitendo hivi vya kikatili kwa wanyama vimekuwa vikiendelea mara kwa mara hasa katika maeneo ambayo yana mrundikano wa makazi ya watu, na hata vingine vikionyeshwa kwenye luninga zetu lakini wahusika wa haki za wanyama wakivitazama tu vikiendelea bila kuvikemea wala kuwachukulia hatua wale wote wanaoshiriki kufanya vitendo hivi.


Kwa mataifa ya wenzetu ni lazima upate hukumu ya kifungo kwa kufanya vitendo hivi.

KAPINGAZ Blog inawaomba wahusika waweze kutimiza majukumu yao na ikiwezekana wawachukulie hatua hawa wote wanaoshiriki kufanya vitendo hivi.
 
 
Nimetumiwa na :
Henry Kapinga wa KAPINGAZ blog

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 4:55 pm  

Inasikitisha kwa kweli...Ila sijui niseme nini kwa sababu hiyo inayoonekana hapo kwenye picha mmhh...ila pia kuna watu wanawatunza wanyama mpaka unashangaa mnyama mpaka ana bima..sasa sijui hapa uangalifu umezidi? najiuliza tu kwa sauti:-(

Rachel Siwa 8:41 pm  

Huyo wanamwita manyaunyau!!@ da'Yasinta hii nimetumiwa lakini naiogopa hata kuiweka maana inatisha.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP