Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

LABDA kuna uchaguzi mpaka katika :``NI malaya GANI anatukanwa USO KWA USO kuwa ni CHANGUDOA!´´

>> Thursday, September 15, 2011

Ndio,...
.... inasemekana kuna sababu,...
..... kuna wafaao TUSI ambao hutukanwa CHOBISI TU na watu ,....
..... na sio MBELE ZAO!:-(

Swali:
  • SI inasemekana kuna ambao UTABWENGWA  aka KULA MKONG'OTO  ukiwatusi MBELE zao?

Ndio,...
.... labda siri ya mojawapo ya WABABE hata wale WATAWALA  na sio tu  YULE GANGWE wa MTAA kujisahau ,....
.... ni kuwa hawastukii WANATUKANWA kwa kuwa wamtukanao  wengi hata MWENYEKITI WA KIJIJI hutukania pembeni  wasisikike kwa kuwa  wanahisi hawana ubavu wavarangati  kama MBABE  akiamua  tusi hilo  linahitaji  aliyetukana  ADHIBIWE hata kivarangati!

Swali:
  • Unabisha?
  • Lakini si inawezekana pia WAOGOPAO wamdhaniaye ni MBABE  kuna kitu tu hawajastukia  ambacho labda ni  udhaifu wa huyo MBABE wa MIKWALA na yatishayo yake ni MIKWALA tu?

Ndio,...
.... labda unaweza kushangaa uogopaye kumtukana,...
..... ni jinsi gani sio MBABE kihivyo na  sababu labda ni jinsi tu ajuavyo kuwa  afaaye kuogopwa KIKWELI ni WEWE!:-(

Swali:
  • Si siri ya UBABE hata wa viongozi  wa NCHI wananchi wakistukia kitu   huo ubabe hutoweka kwa kuwa labda ni WANANCHI na sio VIONGOZI ndio kikweli wenye nguvu?

Ndio,...
....  labda hata wewe unisomaye,...
.... inawezekana unachagua TU hata MALAYA  wa kumuita MALAYA  mbele zake!:-(

Na ni wazo tu hili KAMANDA!



Hebu PROFF aanzishe vita upya  kwa-Tabasamu




Nameless na Nyashinski waingilie kati kwa-JIDAI



Au tu Brick & Lace waisogeze tu pembeni kidogo kwa - Love Is Wicked


3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:53 am  

Labda:-)

Simon Kitururu 11:55 am  

@Yasinta: :-)

Yasinta Ngonyani 12:01 pm  

nimeupenda huo wimbo wa tabasamu:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP