Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Tatizo la waogopao kuonekana hawajui chuchu YASEMEKANA HUWEZA KUWA NI LILE la wasiojua CHUCHU kujifanya wanajua mpaka TITI ZIMA!:-(

>> Wednesday, September 14, 2011

Ndio,....
..... inasemekana wajifanyao KUJUA kila kitu,....
..... labda HILO hutokana tu na udhaifu wao katika kustukia kuwa KIBINADAMU labda  haiwezikani kujua kila kitu na kwahiyo moja ya sifa nzuri kwa MTU MWENYE BUSARA NA UJUAJI  yaweza kuwa ni ukweli akirio kwa kukubali kuna kitu hajui!:-(

Swali:
  • Kwani hujastukia MAISHANI MWAKO kuwa kuna mpaka  baadhi ya ambao labda wangejifunza kutoka HATA kwako ambao wafanyacho ni kujifanya wanajua ambayo labda ni yale ambayo WEWE  ndiye ni MWALIMU na hapo ni hata  tukiruka kipengele kuwa labda pia ni WEWE uliyeanzisha MPAKA hilo SOMO?


Ndio,...
..... yako mambo MENGI ambayo labda sababu za akina Simon Kitururu kutoyajua,...
.... NI  kwa akina Simon Kitururu kujifanya ni WAJUAJI wa kila kitu!:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(





Hebu DOROTHY MASUKA aanzishe upya kwa -Mfan' Omncane

Au tu Dorothy Masuka arudie tu na - MaGumede

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

sam mbogo 1:57 am  

Unapo uliza swali,je ni ujinga? maanayake unakuwa umefikia hali yajuu ya kutakujuwa, kinacho fuata ni kuuliza ili ufahamu jibu lake.katika kuuliza kwako swali hilo upande mwingine atakaye kujibu swali lako haimanishi yeye ndo mjuwaji wa kila kitu.kuuliza swali ni njia mojawapo,kama binaadamu kuonyesha,kujifunza kutoka kwa wengine,pia muulizaji nae siyo kuwa hakuna asilo lijuwa katika ulimwengu huu,yaezekana kabisa baadaye kuweza nayeye kuulizwa swali, na kutoa jibu.I,vihelehele,kimbelembele,kamba,fiksi,nk ndo humfikisha binaadamu katika hali ya kujifanya unajuwa kila kitu.kufahamu na kujuwa ni vitu viwili tofauti. Kaka S.

Simon Kitururu 9:14 am  

@Kaka S: Hapo uliposema,.... nakunukuuu:``.....vihelehele,kimbelembele,kamba,fiksi,nk ndo humfikisha binaadamu katika hali ya kujifanya unajuwa kila kitu.kufahamu na kujuwa ni vitu viwili tofauti.´´´mwisho wa nukuu.

Yani umemaliza kila kitu hapo.


Basi jumatatu nilikutana na jamaa mmoja ambaye alikuwa anataka kufundisha mpaka ambao wametunga somo huku yeye mwenyewe hajui vizuri .

Na wote waliokuwepo walikuwa wanajua aongeleacho mwalimu kakaa kimya ambaye yuko meza hiyohiyo tuliyokuwepo. Nikawaza kuwa ``unajua huyu jamaa angejifanya hajui angefundishwa na source ya somo´´.


Ila baadaye jamaa mwingine akaniambia kuwa wako wasimuliaji ambao hujifanya wanajua kama uchokozi ili wajulishwe. Ila mimi naamini mara nyingi kiherehere kinaweza kufanya mjuaji amuache aliyepotoka aendelee kupotoka.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP