Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katibu wa TA Reading na Mkewe Wameremeta!

>> Sunday, September 25, 2011

Salam,


URBAN PULSE CREATIVE Inawaletea picha za tukio la Harusi ya nguvu iliyofanyika Jumamosi Tarehe 25 septemba 2011 Katika ofisi ya Reading Registrar kati ya Katibu wa Tawi la TA Hapa Mjini Reading Amri Dello na Alice Kapya.


Baada ya Kufunga pingu za maisha tafrija ilifanyika ndani ya Boat na kuzunguka mitaa ya berkshire hadi windsor kwa Queen na kumalizikia katika Mji wa Reading.

Wadau mbalimbali walikuwepo katika sherehe hii akiwepo Mh Balozi wetu Peter Kallaghe.

URBAN PULSE inapenda kuwapa hongera sana Maharusi wetu na kuwatakia kila la kheri katika safari yao ndefu walioianza leo.

MUNGU AWABARIKI,
Asanteni

URBAN PULSE CREATIVE

Bonge la kiss

Zawadi Maalum kutoka kwa Mzee Abdul Dello

Boti inayoitwa caversham Princess ikiwasubiri maarusi tayari kwa ajili ya sherehe

Bwana Harusi akiweka Sahihi kwenye cheti cha ndoa

Bwana harusi Dello

Bwana na Bibi Harusi

Bwana na Bibi Harusi wakiwa wanameremeta

Dello akimlisha keki mkewe

Kila Kitu kimekwenda poa na jiko nshavuta sasa tugange yajayo

Maarusi wakipewa maelekezo kabla ya kuingia kwenye boti

Mh Balozi akitoa nasaha zake kwa bwana na bibi Harusi

Mh Balozi Kallaghe Akiwa na MH Balozi Kapya wakibadilishana mawili matatu

Mh Balozi Kapya na Binti yake wakiingia katika ndani ya Reading Registry Office

Picha ya Pamoja kutoka kwa pande zote za famailia na wadau waliokuja leo kushuhudia Harusi

Pozi baada ya Harusi

Wadau wakijimwaga kwa raha zao

Wakati wa kulisakata Rumba

7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 1:21 pm  

Hongereni maarusi nimeipenda hiyo picha waliokaa kwenye kajumba:-)

Unknown 10:42 pm  

DUUUUH!!!.

Bado ya kwako Kitururu.

Wewe utapanda Boat au ni Ungo?

Hahahahah.

Rachel Siwa 12:04 am  

Mcharia;`]

Unknown 12:14 am  

Naam Swahili kwa waswahili!!

Simon Kitururu 8:29 am  

@Rasta Mcharia na Rachel: :-)

Yasinta Ngonyani 11:30 am  

kweli hapo umesema mchari? twasubiri kadi...

Rachel Siwa 2:16 pm  

Mimi nimeshaanza kuchanga nauli kwa kibubu yakheeeee!!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP