Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika ile kitu MASIMANGO RASMI!

>> Wednesday, September 14, 2011


Kumsimanga MTU rasmi,...
..... labda hakuhitaji MASIMANGO yawe ni yale ya USO kwa USO.


Na uso KWA uso,...
..... kama asimangwaye hastukii kiendeleacho ni MASIMANGO,....
...... asimangaye MTU wakati huo labda anajipotezea muda tu .:-(

Swali:
  • AU?
  • Si unajua labda ushawahi kusimangwa RASMI na mpaka umuheshimuye na ni heshima zako  zilizosababisha ufikirie MASIMANGO ni kukosolewa tu na UMHESHIMUYE na sio kusimangwa?

Ndio,...
.... labda SIMANGO ni masimango,...
.... PALE TU tu asimangwaye astukiapo anasimangwa,...
....... kama tu ilivyokuwa tusi ISEMEKANAVYO  huweza kuwa ni SIFA kwa atukanaywe kama tusi lamtu kwake kiuelewa  BADO ni SIFA.:-(


Ni wazo tu hili MKUU!
Tuko PAMOJA,...
.... na nakutakia JUMATANO NJEMA MKUU!:-(


Hebu turudi nakuanzia kwenye ma-JAZZ ili Ben Williams aintrojuzi -State Of Art



Ben Williams aaingie tu kazini kidogo na-The Lee Morgan Story



Au tu Lupe Fiasco aingilie kati na kuachia tu ``I Gotcha ´´ akiwa na The Robert Glasper Experiment



 LUPE FIASCO aongezee tu na ``DUMB IT DOWN ´´ akiwa na hawahawa The Robert Glasper Experiment



 Bilal ajaribu tena kutuliza kwa- Get Out of My Hair



Halafu tu Q-Tip airudishe palepale NAKUMALIZIA akiwa na walewale The Robert Glasper Experiment katika-Electric Relaxation


11 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:44 am  

Ni kweli watu tupo tofauti na tunawaza tofauti pia:-)

Simon Kitururu 12:14 pm  

@Da YASINTA:
Unafikiri ninini siri ya watu walewale katika LILELILE kuwaza tofauti?

sam mbogo 12:19 pm  

Kusimangwa,kunauma sana.Mtakatifu mtu asimangae ni mdhaifu wa kutupwa.kama ulivyo sema katika kusimanga,siyo lazima iwe uso kwa uso.ila ya usokwa kwa uso ndo mbaya zaidi kwani msimangaji ana kuwa amefikia hatua yakuji dhalilisha mbe yako ,kwa kuhesabu yale yote aliyo kufanyia,mfano,nilikusomesha,ulikuja hapoa huna hata nguo ,nakulisha bure,napoteza hela zangu kukujengea maisha.,nk kwa kweli sikuzote napenda kusma tenda wema usingoje shukrani,tofauti nahili utajikuta una anza kuhesabu, nilikufanyia hili nalile ,nk. ila ningumu sana bila kukusudia waweza msimanga mtu.muhimu kila wakati kujishitukia usitoe /tusitowe masmango na kumbuka kila mara,tenda wema usingoje shukurani. kaka S.

Simon Kitururu 12:23 pm  

@Kaka S: Ila hata asiyemaanisha labda tatizo ni hapo uliposema ``...muhimu kila wakati kujishitukia usitoe /tusitowe masmango na kumbuka kila mara,tenda wema usingoje shukurani´´.

Kujishtukia naanza kujifunza siku hizi kuwa labda sio rahisi sana Mkuu!:-(

Halafu umeniwazisha upya sana tu kuhusu hili swala kwa jinsi ya ulivyogusia kwenye oni lako Mkuu.

sam mbogo 12:35 pm  

Labda kwa kuongezea tu,mtu yeyote hebu kumbuka nilini uli simangwa, ama na mzazi wako, mlezi wako,rafiki yako,ndugu yako,kaka au dada.pata picha, iwewe usokwa uso,ulijisikiaje wakati unasimangwa na baada ya kusimngwa. kaka S.

Simon Kitururu 12:38 pm  

@Kaka S: Yani wee acha tu ! Halafu ukizingatia kuna akina sie ambao hatuna mchezo wa kusahau kirahisi basi huwa kama mie huzinguka mpaka na wale waliosimanga sana halafu ukikutananao wanakuwa wamesahau hilo halafu inabidi usamehe tu wakati moyoni unastuka labda msamaha wako sio wa kweli kwa kuwa bado unakumbuka kitu.:-(

Yasinta Ngonyani 12:41 pm  

Kaka Simon...Sijui kama kuna siri ya walewale...na kama ipo:-(
Kama alivyosema kaka S kusimangwa ana kwa ana kunauma sana lakini hata hivyo ukweli lazima siku moja utakuwa wazi...Ila sijui kwanini watu wanasimangana??

Yasinta Ngonyani 12:42 pm  

Simon! kumbuka kwamba MTENDA HUSAHAU HARAKA SAna kuliko MTENDEWA...

Simon Kitururu 1:35 pm  

@Yasinta: Halafu nimekumbuka ulishawahi kusimulia kuna mpaka ndugu aliyekuwa anakunyima hata kanga halafu kasahau!:-(

Yasinta Ngonyani 2:35 pm  

DuH..una kumbukumbu wewe..... ni kweli kabisa Simon na siwezi kusahau najaribu lakini bado inaniuma sana:-(

sam mbogo 3:50 pm  

Tuko pamoja,ila wewe kitururu,Simon,Mtakatifu hoja yako ni pambanifu sana hongera sana. kukumbuka masimango ni muhimu na inakusidia katika kupambanua ukweli wa yale uliyo simangiwa.Pia nikpimo tosha kwa msimangwaji kutoa msamaa na kusonga mbele,ila kwa msimangaji huwa ana hali ngumu anaweza hata wakati mwingine atake kukubeba. ila yote nimaisha,kusamehe toka rohoni nidawa tosha yakuishi hapa duniani raha mustarehe. naomba nishie hapa kwaleo,sio naenda kupika hapana namfuamtoto shule. kaka S

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP