Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika UJEMADARI wa wasioogopa SIMBA ambao ni waoga wa MENDE!

>> Thursday, September 22, 2011

Ndio,...
...... labda kuna wakati NI MENDE  na wala sio SIMBA,...
.... afaayekuogopwa na MTU ,...
.... hasa kwa kuwa    katika MAZINGIRA  saa nyingine ni  MENDE atakaye kudhuru kwa kuchafua chakula chako na kukufanya UUGUE   ndiye afaaye kuogopwa  kuliko  SIMBA ambaye  kwa ulipo NDANI YA GARI  hata bila  gobole lako  hunahaja ya kuogopa sana .:-(

Swali:
  • Si unakumbuka labda  NI BUSARA kuogopa  kitu  kwa kusoma kwanza  nini  ni sababub kiogopwe ?
  • Na si inawezekana  si kila MAZINGIRA kiogopwacho  kinamakali YALEYALE yake yaogopwayo?
  • Si nasikia kuna mpaka KIMBWA  kuna mbwa waogopao uume  kwa UTANUZI WAKE KWENYE MAZINGIRA na kusahau labda wahitajicho kukihofia ni shahawa  za MBWA ambazo  kiutanuzi  ni rojorojo isiyo na ujazo sana  katika hayo MAZINGIRA mwanzoni ingawa  ndio siri ya ujauzito asioutaka mbwa pamoja na magonjwa kemkem?
  • Na si labda  bado JEMADARI asiyeogopa SIMBA  kiboko yake bado yaweza kuwa ni  INZI  tu?
Ndio,...
........ bado simba ni MKALI  hata kwa MAJEMADARI wasioogopa SIMBA ,...
.........ingawa labda  hainahaja ya kuhofia SIMBA kila MAHALI  wakati INZI anatosha  kutekeleza kitendo ahofiwacho  SIMBA  mtu alipo  ,...
.... kile cha kuua MTU.:-(



Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!




Hebu Arrested Development waanzishe upya kwa - People Everyday



Chaka Demus & Pliers waingilie ghafla kwa - Tease Me




Au tu Pliers amalizie kwa - Sweet Memories


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP