Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kuna KUJISIKIA VIZURI na KUFANYA VIZURI!

>> Sunday, September 18, 2011

Na KUJISIKIA VIZURI,....
.... kunaweza kuwa ndi kisa ajisikiaye vizuri kaacha KUFANYA VIZURI,...
... kwa kuwa kihisia tu kashafikishwa.:-(

Hebu tupate kamusi kimbenjuko:
KUJISIKIA VIZURI: Feeling Good
KUFANYA VIZURI: Doing GOOD

Swali:
  • Si kwa kujisikia vizuri tayari na ya DARASA la saba kwaweza kufanya mtu aone KUENDELEA na vidato kwa KUFANYA kitendo cha kuendelea shule ni usumbufu?
  • Si kujipodoa ni USUMBUFU kama KIGOLI anajisikia kashatoka mchelemchele bila VIPODOZI kimfanyo?

Ndio,....
..... kuna ambao WAJALICHO,...
... ni KUJISIKIA VIZURI na kwa hiyo kama watajisikia vizuri angalau kwa MANENO kukemea VITA hiyo huwa inatosha hata kama suluhisho ingekuwa ni mpaka wao WAFANYE KITU na sio kupiga tu taralila ili vita IISHE.

Swali:
  • Unabisha?

Ndio narudia,....
..... kuna ambao WAJALICHO ni KUJISIKIA VIZURI na sio KUFANYA VIZURI,...
.... kitu ambacho hufanya kama wanajisikia vizuri basi hawana MSUKUMO TENA wa kufanya vizuri hata ya mtu.:-(

Swali tena:
  • Si unakumbuka kutonielewa RUKSA?

Okei,...
....NIMEACHA!:-(





Hebu Gloria Estefan aanzishe upya kwa - Conga



 SHAKIRA ahamishe kwa-WAKA WAKA



Shakira aongezee zaidi kwa -LOCA



Halafu sijui kwanini lakini hebu amalizie tu tena kwa- HIPS DON'T LIE


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP