Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama HUJIAMINI ,mwingine ndiye atakuwa MUAMUZI WAKO hata katika yako ya NGOMA kuinengulia MAUNO au kutonengua!

>> Saturday, September 17, 2011

Ndio,...
.... ukijiamini ,..
...... unaweza mpaka KUINJOI kivyako dagaa KIAFYA kabisa,....
....... na sio UKAWARUKA huku unawapenda  kwa sababu  kuna iaminikao ni wajanja wadhaniao DAGAA chakula cha kishamba!:-(

Swali:
  • Si unajua sababu zako binafsi za kupenda hata MAKANDE unazo tayari na kama UNAJIAMINI huhitaji kutishwa na mpenda NGUNA ili UJIVUNGE kula MAKANDE kisa wapenda UBWABWA na NGUNA wamejazana kwa MAMANTILIE?
  • SI nasikia kwa kutojiamini kuna wakosao MCHUMBA?

Ndio,...
..... kama HUJIAMINI,...
.... unaweza kujikuta unaenda VICHAKANI wakati CHOO na MALIWATO kwa ujumla VIPO.:-(


NI wazo tu hili MKUU,...
....na kutokujiamini kuna watu kwao INALIPA pia kifulu kujiachia!

Turudi GHANA tena REGGIE ZIPPY na NIGTHMARE warudie-Virgin




Mighty Shadow arudie - Shadow Ting



Halafu Mutabaruka azime tena kwa - Whey Mi Belang



7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 12:31 pm  

nukuu "Ndio,...
..... kama HUJIAMINI,...
.... unaweza kujikuta unaenda VICHAKANI wakati CHOO na MALIWATO kwa ujumla VIPO.:-("mwisho wa nukuu:-na pia kwa kujiamini unaweza kustukia umevaa suruali bila chupi ndani...Jumamosi njema Simon

Simon Kitururu 12:41 pm  

@Yasinta: Nafikiri kuvaa suruali bila chupi sio tatizo sana kwa kuwa kunauwezekano pia kuwa CHUPi kwa wengine ni lakshari. Tatizo tu labda ni pale mtu akijiamini mpaka kuacha kuchamba baada ya haja kubwa!:-(

Yasinta Ngonyani 12:56 pm  

haya bwana! nimekuelewa....

Simon Kitururu 1:05 pm  

Tuko pamoja Yasinta!

Yasinta Ngonyani 1:24 pm  

Kujiamini,kuamini na kumwamini...je ni vizuri kujiamini kwanza dipo uuamini na kumwamini/kuamini?...Hivi kwanini kuna wengine huwa huwaamini kama mtu anasema kuwa kwa mfano NAKUPENDA au labda SINA HELA...

SAM MBOGO 5:10 pm  

KUJIAMINI,NIMUHIMUSANA,USIPO JIAMINI WEWE KWANZA ITAKUPA SHIDA SANA KATIKA MAISHA YAKO.KUJIAMINI NI KUTHUBUTU KUTENDA JAMBO.KWA UPANDE MWINGINE KUJIAMINI HUKO,BILA KUWA NA KIASI,PIA NITATIZO,HUWEZA KUWA KERA WENZIO.MFANO KWADI WA KUTONGOZA,LAZIMA AWE ANASIFA YA KUJIAMINI.KWAMAANA HIYO WAWEZA KUKUTA WOTE TUNAJIAMINI,ILA KATIKA MZINGIRA FULANI KUJIAMINI KWETU HUKO HUATHIRIKA. KITENDO CHA KUMUOMBA KWADI AKUTONGOZEE DEMU NIKUJIAMINI,JAPO MAZINGIRA YA KUMUONA HUYO DEMU MOJAKWAMOJA KWAKO NI MAGUMU.PIA NIVIZURI KUJISHITUKIA UNAEPUKANA NA MENGI.KUMBUKA ULIVYO KUWA MDOGO/KIJANA,KULIKUWA NA MANENO HAYA,SHAPU,GANGWE,CHEKI BOBU,MSELA,NDULA,WENGINE WAKAJIITA BUTI JIWE,NK YOTE HAYA NIKATIKA KUTAFUTA KUJIAMINI,ILI KUFICHA UDHAIFU FULANI ULIOKUWA NAO KWA WAKTI ULE.KAKA S.

Simon Kitururu 4:22 am  

KAKA S umemaliza somo hapo!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP