Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

HIVI NDIVYO SOKO KUU LA MWANJELWA SIDO LINAVYO ONEKANA SIKU YA LEO BAADA YA KUTEKETEA KWA MOTO

>> Sunday, September 18, 2011

HITILAFU YA UMEME NDIO KILIKUWA CHANZO CHA MOTO


NA MWANDISHI WETU MAALUM KUTOKA ENEO LA TUKIO

ASUBUHI YA JANA TAREHE 16.09.2011 NCHI IMEINGIA KATIKA JANGA LENGINE AMBAPO SOKO KUU JIPYA LA SIDO MWANJELWA MKOANI MBEYA LILITEKETEA KWA MOTO MAJIRA YA SAA 9:50AM ASUBUHI, MOTO HUO AMBAO ULISIMAMA UKIWAKA KWA MUDA WA MASAA MAWILI BILA KUZIMIKA NA KUSABABISHA UHARIBIFU NA KUPOTEZA MALI ZA WATU WENGI. IKIWA NI MIAKA MICHACHE TUU KUPITA BAADA YA WAFANYA BIASHARA HAO KUPATA PIGO KUBWA BAADA YA SOKO KUU LA MWANJELWA KUUNGUA MOTO NA KUWALAZIMU WAANZE UPYA BIASHARA ZAO.

HABARI ZAIDI ZINASEMA BAADA YA MOTO HUO KUANZA ILICHUKUA MASAA MAWILI MPAKA MAGARI YA ZIMA MOTO KUFIKA NA KUANZA KAZI YA KUSAIDIA KUZIMA MOTO HUO AMBAPO WALIKUWA WAMECHELEWA HIVYO KUZIDI KUSABABISHA UPOTEVU WA MALI ZA WENYE MADUKA.

JESHI LA POLISI WAKISHIRIKIANA NA JWTZ PAMOJA NA MIGAMBO WALIKUA KATIKA ENEO HILO KUHAKIKISHA USALAMA KUTOKANA NA KUWA NA VIBAKA WENGI AMBAO WALIPATA NAFASI YA KUIBA MALI ZA WANANCHI.

KATIKA TUKIO HILO LA MOTO KUCHOMA SOKO LA SIDO MWANJELWA MBEYA BAADHI YA MAMBO YALITOKEA IKIWA NI PAMOJA NA MTU MMOJA KUGONGWA NA GARI ALIPO KUWA ANAJARIBU KWENDA KUOKOA MALI ZA WAFANYA BIASHARA HAO, PIA KULIKUWA KUNA MFANYA BIASHARA ALIKUA ANAZUIDA DUKA LAKE ILI WEZI WASIIBE KATIKA DUKA LAKE NA KUUNGUA KWA MOTO, INAHOFIWA HUYO NDIE MTU PEKEE AMEPOTEZA MAISHA KATIKA TUKIO HILO. PIA INARIPOTIWA KUWA KUNA MAMA MJAMZITO AMBAE ALIPATWA NA UCHUNGU NA KUTAKA KUJIFUNGUA KATIKA ENEO LA TUKIO LAKINI WASAMALIA WEMA WALIMWOKOA NA KUJIFUNGUA SALAMA.

WANANCHI WASIO NA MEMA AMBAO WAKATI JESHI LA POLISI LILIKUWA LIKIJARIBU KUWASAIDIA WATU, WANANCHI HAO WALIANZA KUPIGA MAWE MAGARI HAYO YA POLISI NA PIA KUWATUPIA MAWE MAPOLISI HATA HIVYO MAPOLISI HAO WALIFANIKIWA KUWASHINDA BAADA YA KUWATUPIA MABOMU YA MACHOZI.


AKIZUNGUMZA NA MMOJA WA WAFANYA BIASHARA JINA LAKE ANAITWA GODEN MWAKALINGA ALIELEZA KUWA CHANZO CHA MOTO HUO KILITOKANA NA HITILAFU YA UMEME KATIKA KIBANDA CHA BIASHARA CHA BWANA GHALIFA NA KUSABABISHA MOTO HUO KUWAKA NA KUSABABISHA HASARA KUBWA KATIKA SOKO HILO KUU LA SIDO MWANJELWA MBEYA


PICHA NA HABARI KUTOKA:




1.JPG
Haya ni mabaki ya mabati na vyuma  vilivyoteketea kwa moto

2.JPG
Moto bado unaendelea kuwaka  taratibu huku watoto wakiokota mabaki ya bidhaa mbali mbali zilizoungua na moto

3.JPG
Vibaka wakitoka na vyuma chakavu katika banda la sido lililoungua kwa moto

4.JPG
Mabaki ya majiko ya mkaa na vigae vyake

6.JPG
Jengo la sido mbeya nalo limeteketea kwa moto 

5.JPG
Soko limebakia kiwanja tuu hakuna kilicho salia, pia umati wa watu wakitazama soko baada ya kuungua kwa moto jioni hii


Nimetumiwa HABARI HII na:
Fredy Tony Njeje

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP