Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika kuoanisha MAANDISHI ya KIPENZI MTANDAONI, sauti yake kama MALAIKA na LISURA kama JIPU!

>> Saturday, September 24, 2011

Sauti na MAANDISHI  kwenye sura ya KISURA ambaye hujawahi kukutananaye  kwa kuwa penzi liko MTANDAONI,....

.... hujenga  pia SURA ya KISURA uitakayo,....
.... kwa kuwa  moja ya kikumbushacho  na kukamilisha sura ya MTU  labda wala sio SURA.:-(

Swali:
  • Ushawahi kustuka baada ya kukutana na mtu ambaye ulikuwa unamjua kwa maandishi  au sauti tu na kujikuta  unahitimisha hayuko kama ulivyomjenga akilini kimategemeo?

Ndio,...
.... kuna VISURA ambao ni wazuri  KIMAANDISHI na SAUTI tu ,...
.... ambao ukikutananao itabidi uanze kujifunza upya kuoanisha SAUTI , maandishi na SURA,...
.... ili MPENZI apendeke  kama ulivyowahi  kumpenda kwenye ndoto mara kadhaa kila siku ukilala ,...
.... kabla hujakutananaye!:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Jumamosi NJEMA!

Hebu TITI aanzishe upya kwa -Ilove U




Titi aongezee mnuso kwa - Sy Malick



Au tu Werrason arudishe tu -Likambo


3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Rachel Siwa 4:05 pm  

kaka yamekukuta nini? uwe na wakati mzuri.

Simon Kitururu 4:10 pm  

@Rachel: Yamenikuta mwayego ya mtandaoni na uso kwa uso sura MPAKA JINSIA YA MTU ukiachilia mbali yaongelekayo tofauti !:-(

Uwe na siku njema nawe Dada Yangu!

Rachel Siwa 10:46 pm  

hahahahahaha pole kaka wa mimi, Amina kaka nategemea Neno la kesho Kanisani litakufariji.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP