Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UDHAIFU wa MATUMAINI ya ya KESHO,....

>> Tuesday, September 27, 2011

.... ni  ile HALI ya  kutufanya tusiinjoi ya LEO kwa UKAMILIFU,...
.....KISA,...
....tunatumainia ya KESHO yatakuwa BOMBA zaidi!:-(

Swali:
  • Si labda ya LEO  yangekuwa matamu vyakutosha kama tusingetarajia TUYATUMAINIYO ya baadaye ya hata KESHO  yatakuwa BOMBA zaidi?
  • SI LEO haijirudii MAISHANI na labda leo  ndio LEO?

Ndio,...
..... labda  MATUMAINI ndiyo YASABABISHAYO mpaka walioelimika vyakutosha DARASA LA SABA  WASIRIDHIKE na kuendelea  mpaka na vyuo ambavyo WATAJIFUNZA wasiyoyahitaji MAISHANI kwa matumaini tu kuwa  WAJUAVYO hayatoshi na siri ya FURAHA ni kuendelea na SHULE ya hata yasiyowafunza kitu MAISHANI!


Swali:
  • SI nasikia ni mengi tu yafunzwayo MADARASANI huwa hayamsaidii MTU na ni matumani tu yafanyayo watu kibao KUKOKOTOA sana tu MAKALUKULASI wakati  hawatayatumia hata siku moja MAISHAI?

MATUMAINIIII!

Ndio,...
.... MATUMAINI ni KIBOKO,....
.... na yanamsaada mpaka wa kufanya baadhi wasiwe MALAYA wala MAJAMBAZI ili kukwepa tu dhambi  kwa kutumainia ya MBINGUNI.

Ni wazo tu hili MUUNGWANA!





Hebu Jaguar aanzishe upya kwa - Kigeugeu




Sijui kwanini lakini turudi HAWAII ,...
.....ili J Boog airudishe palepale kwa - Lets Do It Again



J Boog aungwe mkono na Richie Spice warudie-Got To Be Strong


Halafu tu tena KIDUM na Lady Jay Dee wazime kwa -Nitafanya


3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 10:18 am  

Matumaini!!! ni vizuri kuwa na matumaini lakini usiwe na matumaini sana....

emu-three 11:41 am  

Leo ndio leo msema kesho muongo, au sio mkuu. Tupo pamoja ndugu yangu. HECHA, HESWA

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 2:38 pm  

kesho au mbinguni baada ya kufa = illusion

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP