Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati kitumbua kinapendwa , MWENYE KITUMBUA huweza kuwa bado ni USUMBUFU!

>> Saturday, September 17, 2011

Na katika MSUMBUFU,...
.... bado kwaweza kuwa ndiko kwenye KITUMBUA!

Sasa wakati unapenda KITUMBUA,...
..... yasemekana inabidi uvumilie mwenye KITUMBUA ,...
..... kwa kuwa labda kitumbua upendacho kitanuka au kuoza kabisa bila MWENYE KITUMBUA ambaye labda ndiye mtunzaji mkuu wa KITUMBUA!:-(

Swali:
  • Unapenda KITUMBUA?
  • Unauhakika naongelea nini kama niongeleacho sio KITUMBUA?
  • Na siunajua mwenye kitumbua naweza kuwa namaanisha ni mwenye FIKIRA na fikira yenyewe ikawa ndiyo KITUMBUA? 
  • Na si wenye kufikiria UTOKO  wa mbwa jike wanaweza fikiria KITUMBUA ni utoko?

Ndio,...
.... labda wakati tuna penda ALMASI kuliko mwenye MGODI wa ALMASI,...
.... labda moja ya sababu almasi TAMU ni kwa kuwa kuna wenye migodi hata wale WACHAFUUUU!:-(

Ndio,...
... wazo limepinda ingawa bado ni WAZO tu hili MKUU!
Tutakutana KESHO hapa kijiweni kwa TARALILA zaidi kama MOLA au tu IKIWEZEKANA!:-(


Hebu ghafla Jackson 5 waanzishe upya kwa - The Love You Save



The Jacksons 5  waongezee- Who's Loving You




AU tu Michael Jackson abakie pekee na aendelee kwa - Don't Stop 'Til You Get Enough




Michael Jackson arudishe mdinyo- Remember The Time




Aingizie tu na -The Way You Make Me Feel



Halafu amalizie kwa - You Rock My World


7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 1:43 pm  

:-(

Simon Kitururu 2:12 pm  

@Yasinta: Nini tena unahuzunika?

Yasinta Ngonyani 2:18 pm  

kumbe umestukia kuwa nimehuzunika?Hivi kwa nini kinaitwa kitumbua na sio andazi? au bumunda?

Simon Kitururu 2:20 pm  

@Yasinta : Unaongelea nahisi kitu kingine. mie kwenye kitumbua nilikuwa naongelea KITUMBUA.

Na si andazi ni ANDAZI na BUMBUNDA ni BUMUNDA na hayo hayawezi kuwa KITUMBUA?

Kwani kwako kitumbua ni nini?

Yasinta Ngonyani 2:37 pm  

Mmmmmhhh najua naongelea nini.au unaongelea nini ila....ntafufute ntakuambia hapa naona ....naacha na samahani kwa kutoka nje ya mada:-(

Rachel Siwa 4:23 pm  

Huku kwetu kitumbua hakiaribiki mapema, @ tunaweka kwa jokofu.

SAM MBOGO 4:51 pm  

HAYA TENA JUMAMOSI YA KITUMBUA.SIFA YA KITUMBUA LAZIMA KICHOMWE,NA SI KUKAANGA KAMA UJUWAVYO.PIA KITUMBUA KIKICHOMWA NI LAZIMA UPANDE MMOJA KIUNGUE ,AMAKWA BAHATI MBAYA AU HUSABABISHWA NA MKONO WA MCHOMAJI.LAKINI HATA ULE UPANDE ULIO UNGUA HULIKA,NA NI MTAMU HASA.MWISHO KITUMBUA KIKISHA CHOMWA,KWA KAWAIDA, HUWEKA PEUPE KIONEKANE NAKILIWE.CHA WEZA KUNUNULIWA,WAKATI MWINGINE HATA KUKOPWA,NAKAMA UNAELEWANA VIZURI NA MAMA MUUZA,ANAWEZA KUKUFICHIA KITUMBUA CHAKO ILI MTEJA ASIKITAMANI NA KUKINUNUA.KAKA S.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP