Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kuna ya LAZIMA kama kwenda MSALANI na yatafutiwayo ULAZIMA mpaka inasahaulika kuwa hayo sio LAZIMA!

>> Friday, September 16, 2011

Na kula kwa mpenda ngono ,...
....  ni LAZIMA lakini  bado ukweli ukawa uko palepale kuwa,...
.... ngono kwa mpenda NGONO sio lazima.

Swali:
  • SI inasemekana  kuna hata wacheza KABUMBU ambao hufikiria kucheza kabumbu ni uhai wao  kitu ambacho huwasahaulisha kuwa KABUMBU sio lazima mpaka wavunjike mguu na kustukia kuwa maisha huweza kuendelea bila KABUMBU?
  • Kwani MASISTA na MAPADRE wa kanisa la Katoliki hawakukumbushi kuwa kuzaa WATOTO au hata tu maswala ya chakula cha usiku kuwa kwa BINADAMU sio LAZIMA?
  • Na si kuna mpaka walevi wasahauo POMBE sio lazima?


Na kwa kuwa kuna mambo hutafutiwa ULAZIMA,....
..... labda kumbuka  ukichoka vizuri popote pale  hata kama ni choo cha stendi utalala na KITANDA wala sio LAZIMA!


NI wazo tu hili MKUU!


Hebu Pathy Patcheko au kwa jina jingine Nsunda Luyindula Nzinga arudie - Tchaku




Au tu Tabu Ley arudie tu - Sacramento


4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

sam mbogo 11:43 am  

Yawezekana, kwa asilimia mia uyasemayo.Binaadamu nikiumbe wa ajabu sana,kunavitu vingine hutendeka/hutokea/hufanyika si kwa matakwa /mapenzi ya binaadamu.mfano kiafya kuna ulazima wa kwenda kujifungua chooni(haja kubwa) ulazima wake unakuja,pale mfumo wa kutoa uchafu anapokuwa unafanya kazi yake barabara,ulazima unakuwepo.uchovu,ukiambatana na usingizi,haukwepeki,kama binaadama,kwa kutumia akili waweza kutaka zuwia uchovu,kimawazo tu,kiukweli huwezi,nimoja katika taratibu za mwili kupumzika,ndiyo maana watoto, ukifika wakati wamechoka,hatakula inakuwa ngumu,na waweza kumkuta kalala chini ya uvungu wa kitanda.kuna usemi kwamba,mtoto halali na hela bali na nepi yenye mavi. Kaka S.

Simon Kitururu 4:36 pm  

@Kaka S: Huo msemo ``Mtoto halali na hela bali na nepi yenye mavi´´- ndio kwanza nausikia aisee! Ntaomba kuutumia kwenye taralila zangu siku moja MKUU

sam mbogo 4:59 pm  

Ruksa kuutumia,mkuu .kaka S.

Simon Kitururu 6:31 pm  

@KAKA S: Asante Mkuu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP