Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Jamani USIPENGE MAKAMASI mezani wengine tunakula! LOH!

>> Saturday, September 17, 2011

Kuna TABIA ,....
...... na tabia nyingine hata kama ni tamaduni huchefua!

Na hapa wala siongelei  kujambia chakula,....
...... kwa kuwa inaweza kuwa ni mpaka kutembea nusu uchi KANISANI au tu kisimani pale unafua!:-(

Swali:
  • Umestukia eeh?
Ndio jamani ,...
.... hasa kwa kuwa MAISHA hapa DUNIANI ni KUSHEA sawa na wanywa MATAPUTAPU / pombe ya kienyeji kwa kushea kigaloni hichohicho  kimoja,...
.... kwa hiyo jamani labda tuwafikirie na wenzetu ili kwa pamoja TUSICHEFUANE kama kuchefuana si lazima au kwa bahati mbaya,...
....kama  iwezavyo kuwa NI  KWA BAHATI MBAYA ajali ya kijambo cha mheshimiwa  mezani  huwezakutokea bila kupangwa ambacho KINASAMEHEKA kama  kimeporochoka kwa bahati mbaya.

Ni wazo tu hili la UJUMLA,...
.... lakini MAISHANI kuna TABIA mbaya za MAKUSUDI ambazo ni NISHAI jamani!!:-(

Lakini hebu turudi MWANZO:
  • Hivi TABIA MBAYA ni nini vigezo vyake ?
  • Hivi TABIA mbaya ni ipi?
Ndio,...
..... labda kama hatuna kigezo ,....
....... wengine tunamchezo wakunyoshea wengine vidole kuwa wanatabia MBAYA wakati na wengine wanavigezo viwaambiavyo kunyoshea mtu mwingine kidole ni TABIA mbaya!:-(

NIMEACHA!


Hebu EDDIE MURPHY akumbushie baadhi ya tabia zawatu hata mezani ,.....
...... ambazo kuna watakaostukia labda kuanzia KUONGEA mpaka kiongelewacho ni TABIA mbaya





2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

SAM MBOGO 5:20 pm  

KUWA NA UTARATIBU NA KUUHESHIMU NI MUHIMUSANA.KILA JAMII ZINA TARATIBU ZAKE,WENGINE HUITA TAMADUNI.NDIYO MAANA WASWAHILI WALI SEMA TEMBEA UJIONEE,UNAPO SAFIRI UNAJIFUNZA MENGI.USICHO KIPENDA WEWE MWENZIO ANAKIPENDA,VIVYOHIVYO UNACHO KITAKA WEWE MWENZIO HAKITAKI.KAKA S.

Simon Kitururu 4:20 am  

@Kaka S : Ndio hapoooo napokwazika ni kwanini Rais wa PWANI asile Ubwabwa kwa mkono mbele ya wageni wa kimataifa!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP