Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ukitafuta- mpaka KUKU wana MATABAKA inasemekana kwa ayatafutaye!

>> Tuesday, September 13, 2011

Swali:

  • SI nasikia mpaka kwenye kuku kuna KUKU waitwao ni kuku wa KIZUNGU?
  • Na hata tukiachana na maswala ya KUKU na kurudi  kwa BINADAMU -si inasemekana mengi tu TUNAYO kwa kuwa ndiyo TUJITAFUTIAYO?

Ndio,....
...... inasemekana kama tu kwenye wenye AKILI  ukitafuta uwezavyokustukia wajinga wao,....
...... inasemekana  ukitafuta  kwenye bata  unaweza kustukia bata zeruzeru,...
.... wakati labda  cha muhimu katika utamu wa nyama ya BATA MTU AIPENDAYO   hakihathiriwi na uzeruzeru wa bata.:-(




Ndio,...
..... hili ni wazo tu MHESHIMIWA!


Lenny Kravitz aanzishe tena upya kwa - Heaven Help




Lenny Kravitz aendeleze dozi kwa-Fly Away



Kabla Yellowman hajaingilia na kubadili mchezo mzima kwa - Nobody Move, Nobody Get Hurt



Halafu Cocoa Tea aendeleze shughuli kwa kumbushia-She loves me now




Au tu Cocoa Tea amalizie tu kwa - Young Lover

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Sam mbogo 6:58 pm  

matabaka hayakwepeki ,kimtazamo.tumezaliwa tumeyakuta,japo nyerere(samahani kwa wasio mfagilia) kwa kiasifulani alikuwa anajaribu/alitaka kusiwe na matabaka,miongoni mwetu.japo hata yeye aliyashitukia matabaka hayo,ambapo hata ikafika kwafira zetu kuona kiazi cha mviringo kukiita,kiazi ulaya,mayai ya kizungu ,nk na hii ni kwa vyakula .matabaka hayohayo,bado tunayo pia ambayo katika usafiri,wa gari moshi,mpakasasa,kuna daraja la kwanza,lapili nala tatu.sasa sisi tulizowea kupanda daraja la tatu(kajambanani) natuliona sawa tu.napia katika matabaka hayohayo katika usafiri wa ndege matabaka yapo,jaribu sikumoja kusafiri first class huko nako ni mwisho.kwamaana hiyo uwezo wa mtu huleta matabaka haya tuyasemayo,mfano mbwa akikondeana huitwa mbwa koo!!. kaka S.

Simon Kitururu 9:22 am  

@Kaka S:Kuna kipindi nilitoka DODOMA nilikokuwa nasoma high School kwenda Morogoro tu katika daraja la kajambanani kwenye garo moshi. Basi nikatengana na begi langu bwana shughuli ya kulipata bado kidogo inifanye nishindwe kushuka Morogoro kwa kuwa tu tulivyojazana hata hatua tatu ili nilidake begi langu ilikuwa haiwezekani siku hiyo.


Lakini Kaka S hudhani kuwa labda siye binadamu wenyewe ndio tunaendekeza matabaka?


Kwa maana hata ukiwacheki kama WAINGEREZA hapo Uingereza ulipo mie nafikiri unaweza kustukia labda hata hawahitaji kihivyo kuwa na hata akina Prinsi William ingawa hao akina Prinsi na Malkia wao labda hata wasipojikweza kuna watakao wakweza tu hata kama kigezo ni wametoka familia gani!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP