Harambee ya Kuchangia Wahangwa Ubalozini Nchini Uingereza
>> Tuesday, September 13, 2011
Jumuiaya ya Watanzania nchini Uingereza TANZ-UK ikishirikiana na TANZ-UK Jumuiya ya Wanzanzibar waishio Uingereza (ZAWA) Urban Pulse na Miss Jestina George Blog imeandaa fundrising maalum kwa ajili ya kuweza kuwasaidia waathirika wa ajali ya meli ya Spice Islander iliyotokea Nungwi njiani kuelekea Pemba. Fundrising hii itafanyika katika Ubalozi wetu hapa London tarehe 17 Septemba 2011 Kuanzia saa nane mchana.
Tunawaomba Watanzania wote mlioko hapa nchini Uingereza kutoka jumuiya mbalimbali,vyama vya kisiasa, wafanyabiashara, wanafunzi na hata wasio Watanzania mjitokeze kwa wingi ili kuweza kujumuika nasi na kufanikisha zoezi hili. Hivyo basi tunaomba mwenye fedha au chochote kile cha kuweza kuthamanishwa tunaomba tuweze kuja nacho na kitafanyiwa mnada. Mfano, wenye biashara wanaweza wakaleta bidhaa kiasi ambazo zitafanyiwa mnada ambapo ziada itakayopatikana itakuwa sehemu ya mfuko tutakaokuwa tunautafuta.
anwani ni; 3 Stratford Place, London, W1C 1AS. Muda ni saa nane mchana (2pm sharp).
Kwa maelezo zaidi tunaomba uwasiline na ............... Mwenyekiti Tanz-UK 07766856565, ZAWA 07538063536,TA London 07404332910
UKIONA TANGAZO HILI TAFADHALI MTAARIFU NA MWENZAKO. WOTE TUNAKARIBISHWA,
Mungu ibariki Zanzibar, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa . Zaidi sana Mungu wabariki Watanzania wote popote pale walipo duniani.
ASANTENI
MWENYEKITI,
TANZ-UK
5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mungu ibariki Tanzania/Zanzibar. Tupo ppamoja katika maombolezo haya.
kutoa ni moyo.kunakitu kinanichanganya,hapa kutokana na janga hili.kumekuwa na lawama,kibao,kwa Voda tanzania kuruhusu mashindano ya urembo yalivyo fanywa wakati kuna meli imezama.mnalionaje hil jambo je lawama nisahihi,kama ndiyo kivipi.kama siyo kivipi pia. kaka S.
@KakaS: Hili la lawama nafikiri wengi tu wanastahili kulaumiwa. Ingawa KITANZANIA wengi wanaona kuwa ilikuwa sio fresh sana kuendelea na mashindano ya urembo wakati Taifa laomboleza! Lakini pia kuna waaminio kutokana na gharama za maandalizi na utata wa ajali siku hiyo labda kulikuwa pia na sababu kwa nini voda waliendelea na shughuli zao.
@Kaka S. Nimeona mahali hiii pia,....
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
13 / 09 / 2011
YAH: KUOMBA RADHI KWA NDUGU ZETU WALIOPATWA NA MAAFA YA AJALI YA MELI HUKO ZANZIBAR .
Usiku wa kuamkia jumamosi ya tarehe 10 / 09 2011 tukio kubwa na la huzuni lilitokea huko Zanzibar ambapo wananchi wengi walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa wakati walipopatwa na ajali ya kuzama kwa MELI iliyokuwa ikitoka Unguja kuelekea Pemba.
Kwa bahati mbaya siku hiyo ya Jumamosi taaasisi yetu ilikuwa inahitimisha Fainali za Taifa za Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania 2011.
Kama waandaaji wa Mashindano haya na wenye Mamlaka kamili ya maamuzi juu ya ama kuendelea au la kuahirisha jambo hili, tulipatwa na mshituko mkubwa sana juu ya tukio hilo.
kamati yetu ilikaa na kutakafari katika tukio hilo kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
• Taarifa kamili ya maafa haya tuliipata rasmi saa tisa na nusu mchana ( 9:30 ) siku ya jumamosi ambayo ilikuwa ni masaa machache kabla ya Fainali za Miss Tanzania kuanza katika ukumbi wa Mlimani City.
• Wenzetu wa TFF waliendelea na mechi za ligi kuu ikiwemo ya Yanga na Ruvu Shooting.
• Katika kumbi za starehe ikiwemo mabaa na burudani za muziki wa bendi na kumbi za disco ziliendelea kama kawaida.
• Muda uliokuwa umebaki kuwakilisha jina la mshiriki wetu kwenye fainali za Miss World zilikuwa zimekwisha hivyo kulikuwa na hatari ya kupoteza nafasi hiyo
• Pia tamko rasmi la kusimamisha shughuli zote za burudani lilianza tarehe 11 septemba 2011 kuomboleza Kitaifa maafa hayo.
Hata hivyo kama waandaaji tulifanya shindano tukiwa katika maombolezo kwani kabla ya kuanza shindano Watu wote waliokuwepo ukumbini walisimama kimya kwa dakika moja na hata washiriki walipoingia kwenye jukwaa kwa mara ya kwanza walikuwa wamevaa vitambaa vyeusi katika mikono yao ikiashilia maombolezo.
Hali hii imetupa mkanganyiko na kujikuta tukiendelea na mashindano kitu ambacho tunaona tumewakosea Watanzania wenzetu.
Kama Waandaaji tunapenda kusistiza kwamba tunawajibika kwa hayo yaliyotokea na si Taasisi yeyote au Kampuni yeyote na tunaomba ichukuliwe kama ni makosa ya kibinaadamu hasa ukizingatia mazingira magumu tuliyokuwa nayo kwa wakati huo na mkanganyiko wa matukio na taarifa za tatizo hilo.
KUOMBA RADHI
Hata hivyo shughuli hiyo inawezekana imewakwaza watu wengi na kwa sababu hiyo na pia hali halisi ya janga hilo na kwa niaba ya viongozi wenzangu na wadau wa shughuli zetu tunatoa tamko la dhati kwa Familia za ndugu wote walikumbwa na maafa haya, wale wote walionusurika katika ajali hii na Watanzania wote kwa ujumla, kwamba TUNAWAOMBA RADHI KWA MKANGANYIKO ULIOTUTOKEA HADI KUFIKIA HALI HII. Hatuna neno zaidi ya kusema na kusisitiza “TUNAOMBA RADHI”
Mwenyezi MUNGU aziweke roho za marehemu mahali pema peponi,
Amina,
Hashim Lundenga
Mkurugenzi
Jamani mimi naomba nipishane na maoni yenu. Ni kwanini tusiseme Tanzania ilaaniwe kwa kuwaangamiza raia wake wasio na hatia kila kukicha. Mara ajali za barabarani, mara za majini, mara vibaka wanachomwa moto, mara askari polisi wanaua raia waliopaswa kuwalinda. Mungu ilaani Tanzania!!!!!!!!!!!!
Post a Comment