Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ikizimwa TAA sina AIBU,....

>> Tuesday, September 20, 2011

 .... gizani naogopa GIZA!


Jua likiwaka naungua na sipendi joto,...
.... na MVUA ikinyesha  sipendi MATOPE.

Njaa ikiniuma nanywea kwa kukosa nguvu,...
.... nikishiba  nazembea nakusikia usingizi kwaajili ya SHIBE.

Swali:
  • Si umestukia chochote kile BINADAMU anaweza kukilalamikia ?
  • Nachochote kile KIBINADAMU huweza kukosolewa?

 NI hilo tu!
 JUMANNE NJEMA MKUU!

Hebu Bamboo na Archapello waongelee - Tabia Mbaya




Au tu Bamboo amalizie kwa - Mama Africa

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 8:30 am  

Ni bonge la ujumbe...Ahsante sana uwe na siku/jumanne njema nawe pia

sam mogo 11:40 am  

baadhi yetu kulalamika jadi,hakuna kizuri kwetu.huyo ndiyo binaadamu wa ajabu.umetukumbusha ujumbe kabambe. na wewe juma nne njema.kaka S

Rachel Siwa 4:47 pm  

Binaadamu hatuna jema kaka, Ahsante kwa ujumbe mzuri.

Simon Kitururu 8:46 pm  

@Wote : Asanteni wote kwa kutoacha kunitembelea! Tuko Pamoja!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP