Cheka nuna.
>> Friday, February 14, 2014
Na ukinuna,..
Je moyowo watabasamu?
Na ukicheka,..
Je moyo ununao ni wa kibinadamu?
Cheka nuna na ikibidi lia,...
Na si mwisho wa cheko yalizayo ni utamu?
Cheka nuna,...
Na wala usijilazimu.
Cheka,..
Ili nasi tudoee wako utamu.
Nuna,...
Ila usilize mpaka mizimu
Cheka nuna,...
Je si hata kulia ni ubinadamu?
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Ni bonge la wazo ambalo ni ngumu kuchagua kucheka au kununa...Karibu tena katika dunia hii ya kublog..
Post a Comment