Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Utamaduni Wa Ombaomba kama ni Fani basi Tanzania ni Kiboko

>> Friday, June 02, 2006

PICHA KWA HISANI YA ISSA MICHUZI
(ombaomba wakiiga viongozi wetu wa Taifa katika fani)








Nilipokuwa nacheki picha za Issa Michuzi. Picha ionyeshayo ombaomba imenifanya nikumbuke kuwa hawa ombaomba tuwaonao barabarani ni wale ambao wadogo sana katika nchi yetu. Wakubwa ni wale viongozi wetu wazungukao dunia kuomba misaada. Kuomba si kitu cha ajabu lakini nafikiria kuwa Tanzania au Afrika kwa ujumla tumefikia hatua kuwa ni jambo ambalo tunalitegemea kabisa. Tutalalamika kuwa walichukua mali zetu wakati wa ukoloni. Lakini tusipojikwamua wenyewe hata siku moja hatuta thaminika.Ukisoma hoja na maoni yaliyotolewa wakati Michuzi alipoibandika picha hii hapo juu, utakuta ni sawa tu na maoni ambayo watu katika nchi tajiri wazungumzayo kuhusu
viongozi wa Afrika. Sijui kama Mwandani unakumbuka. Kunakipindi ulienda kufundisha darasa la wanafunzi Wakifini ,ulemuda uliokuwa ukiishi Finland. Mandela alikuwa katika ziara mwalimu mwenzio akauliza unafikiri Mandela amekuja kufanya nini Ufini? Mwanafunzi akajibu kuomba misaada. Ningefurahi Afrika tukifikia walipokuwa Wachina. Maana sasa hivi hawapewi misaada kizarau .Kila mtu anajua kuwa jamaa wamefikia kiwango ambacho si muda mrefu ndio watakua katika nafasi ya kusaidia nchi magharibi zikiteteleka. Sasa hivi hakuna anayetaka kuwa na chuki na China. Sasa sisi huku bongo kila siku tunaona tu jinsi gani bila misaada mambo hayafanyiki. Angalia mpaka AU(African Union) inashindwa kuandaa mikutano labda mpaka misaada itolewe na mgharibi. Mambo haya yananifanya nisishangae nikiona ombaomba wakifuata mifano ya viongozi wetu ambao ni lazima wazunguke dunia kuomba misaada na mwisho wa siku hata kule misaada inako kwenda isijulikane. Ni sawa kabisa na jinsi Ombaomba wasivyojulikana wameenda kulala wapi. Tofauti ya picha ya juu na hizi za ViooNgozi wetu ni kwamba hawa Vioo Ngozi wetu wana pasipoti na pia wanaomba huku wamevaa suti.


PICHA KWA HISANI YA KRISANNE JOHNSON
(Mkapa akiwa katika fani)












PICHA KWA HISANI YA FREDDY MARO
(Kikwete akiendeleza fani)

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mija Shija Sayi 12:23 pm  

Kama ni maksi basi leo Kitururu nakupa mia kwa mia. Uliyosema ni kweli kabisa, hata sijui kwa nini tumekuwa tukiwashambulia ombaomba wa kitaifa na kuwaacha wa kimataifa (viongozi).

Yule mwanafunzi aliyesema Mandela kaja kuombaomba hakukosea, hapo ndipo tulipofikishwa na viongozi wetu. Nina uhakika nao wanalijua hili ila kwa sababu misaada yenyewe wanaitia mifukoni mwao hivyo hawana budi kufunga macho na kuendeleza fani.

Christian Bwaya 7:01 pm  

Tunawafukuza akina matonya wakati viongozi wenyewe ni daraja hili hili? Hii si haki ingawa wakiambiwa wanakuja juu. Kuna gazeti moja hapa nyumbani liliweka katuni moja iliyokuwa imebeba maudhui haya haya, yaliyowapata hawatasahau. Ukweli unauma!

Kikwete hana jinsi inabidi aiendeleze fani. Lada sijui muujiza gani utokee.

Lakini nafikiri tunakuwa ombaomba kwa kujitakia. Uwezo wa kujitegemea tunao. Tatizo liko mahala naogopa kupataja.

Habari hii imenifurahisha.

Simon Kitururu 12:39 pm  

Mija, Bwaya , inasikitisha sana!Lakini ningependa tuache kuogopa kuongelea haya mambo

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP