Baadhi ya Dondoo kuhusu Tanzania Leo Hii Kwenye Kitabu Cha CIA
>> Friday, May 26, 2006
Kitabu hiki cha CIA hua kinanizingua sana wakati mwingine. Kwa sababu kuna watu wengi ndio hukichukulia kama ndio ukweli mtupu usio na dosari hata kiduchu.
#Mzozo wa Kimataifa: Mzozo na Malawi juu ya mpaka kwenye ziwa Nyasa na Mto Songwe
#Namba ya Meli: Tanzania ina meli kumi tu.
#Watumia intaneti: Kuna watu 333,000 tu watumiao intaneti Tanzania
#Stesheni za TV: Kuna stesheni tatu tu za TV.
#Simu za nyumbani: Kuna 149,100
#Wakulima: Wakulima ni asilimia 80%
#Ardhi ilimikayo: Ardhi ilimikayo ni 4,23% tu.
#Watanzania kiumri: Umri wa kati ya miaka 0-14 ni asilimia 43.7% ya Watanzania wote.
wwavulana ni 8,204,593 na wanawake ni 8,176,489. Hii inamaana baada ya muda kutakuwa na upungufu wa wanawake 28104 wa kuoa kama kila mwanaume katika kikundi hiki atahitaji mke.
7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
jumlisha toa, watanzania wanatarajia kuishi hadi umri upi? Hizi takwimu matata sana.
Mzee karibu
Mwandani hizi takwimu zinamaanisha kuwa wengine karibu tumefikia ukingoni mwa kuishi.Ned asante , nimekaribia
Bado tungali tukiambiwa na viongozi wetu eti kilimo ni uti wa mgongo???
Takwimu ya wakulima, ardhi inayolimwa na ukubwa wa ardhi inayofaa kwa kilimo Tanzania ukizioanisha nadhani utapata kichekesho kimoja kizuuuuuri sana hapo. Ni kwasababu hawa wakulima ni wavivu au ni kwasababu hamna uwezeshwaji wa kuitumia hiyo ardhi yote ambayo inafaa kwa kilimo? Chemka
Mi nadhani hata kukisia kuwa hawa wenye umri wa 0-14 ambao watakuwa na upungufu wa wanawake tuwafundishe self-service na man-to-man friendship ili wasipate frustrations na kuchangia wanawake...
On a serious note: Data za wavulana kuzidi wasichana sio sahihi
Simon my brother, we were together in MG and Dom, TZ.. And I knew back then you were gonna do something to influence the thinking of mankind.. and it has come true!!! Keep it up. I will be a big fan of this blog that I only found out today
Post a Comment