Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MAHUSIANO YA UBINADAMU NA NGONO

>> Thursday, May 18, 2006

Niliposoma jinsi Mzee Zuma pale mahakamani Afrika Kusini alivyojitetea nilichoka mwenyewe. Maana mzee mzima akanitolea kuwa baada ya kupata uroda na mwanadada mwenye virusi alioga kupunguza bahati nasibu ya kupata bingo ya ukimwi.nimejiuliza maswala mengi tokea kipindi hicho. Sentensi hiyo iliniwezesha kupata majibu mengi kuhusu Zuma hata bila ya kusoma historia yake. Miongoni mwa mengi ilinifanya nionekuwa hasingenifaa kuwa Raisi wangu. Nilipozidi kuangalia habari za Afrika kusini nikakuta kuwa huyu bwana bado anaendelea kuwa na mashabiki wengi sana wanaomfuata. Kwanza nikaanza kuhisi kuwa labda ni kwasababu ya ukabila. Nikaanza kuamini kuwa Wazulu wengi wanategemea kuwa yeye ndio atakaye wawakilisha katika makorido ya nguvu za kiserikali pale Serikalini. Inawezekana kunaukweli katika hilo, lakini bado kuna kitu kingine kikaanza kunikera. Nikajiuliza, hivi katika maisha yangu ni watu wangapi ambao najuananao ambao wanajua madhara ya ukimwi lakini huwabado siku ya siku wanasema potelea mbali ajali kazini? Je hakuna ka ukweli kuwa kama ni kweli Zuma anavyosema, watu kibao wakipewa majaribu mitaa ya chumbani wanaweza kufikia hatua yakusema potelea mbali liwalo na liwe. Maana Zuma anadai kuwa yule kidosho alikuwa anamwonyeshea maringo yake dingilidingiri katika anga nyeti. Mimi nianaamini kuna kaudhaifu katika binadamu na maswala haya ya ngono. Bill Clinton alipogundulika kamchezo kake anakofanya ofisini, mshauri wake wakidini Bill Graham akasema , ebwanaee viumbe viwili , cha kike na kiume ambavyo havina hitilafu kama inawezekana visiwe ndani ya chumba wakiwa pekee. Inasemekana kila binadamu ana siku yake ya udhaifu na mtu wake anayeweza kumdhaifisha akibonyeza vifumgo muhimu basi baadhi ya topiki za baolojia zinaweza kufanyiwa eksiperimenti. Kinachotisha ni kama Raisi Mwinyi alivyosema, haka kaugonjwa kamekalia mahala pabaya au alisema mahali patamu hata sikumbuki vizuri.

Hili jambo limenifikirisha sana. Nikaanza kuangania nijinsi gani ngono inavyopendwa na binaadamu. Na je bianaadamu nimjinga kiasi gani kuweza kuchezea moto kila siku hata akijua kuwa moto unaunguza. Kusema ukweli kutokana na mashuhudio yangu, Zuma anachekesha na kusikitisha kutokana na wadhifa wake ,lakini hayuko peke yake. Kunakaudhaifu sana katika swala hili la ngono. Nirahisi kusikia du , nisingempata leo ndio ingetoka hiyo, hivyo ilibidi tu nifanye. Halafu bado utasikia lakini umemchemki mtoto mwenyewe , yule haiwezekani akawanao.......Hizi si kauli anazoongea mtu asiyejua madhara, bali mtu mwenye elimu ya madhara yaletwayo na ngono kabisa.Haya yanaweza kuwani mawazo yanayozunguka katika vichwa vya wengi tu. Mimi siwezi kujitoa katika haka kakona kaubinadamu. Lakini ningependa tujiulize sana wakati mwingine je kwa sababu sisi ni binadamu ni haki yetu kuanguka katika huu mvutano wa taamaa za mwili na chaguo la busara?

Kuhusu swala la Zuma tunaweza tukaliacha likawa ni siasa za Afrika kusini. Tunawezakulichukulia kuwa ni udhaifu wa mwanamume mweusi. Maana kuna baadhi ya watu weupe wenye siasa kali wanaodai kuwa katika baadhi ya mambo ambayo mwanaume mweusi hana breki nayo hili la ngono ni mojawapo. Au tunaweza kujiuliza katika maisha yetu wenyewe tunajifunza nini kutokana na tukio. Kila mtu atakuwa najibulake . Wenye kutaka kuishi muda mrefu, lao na wale wanaoishi kila siku kama ndio mwisho wa dunia, lao. Jawabu ulipatalo jaribu kuangalia litawaathiri vipi watu wa karibu yako. Ikibidi jiandae kwa hilo pia. Maana huwezikujua, baadhi ya watu washamaliza mambo yote yanayoleta maana katika maisha yao hapa duniani.

Ndio matamanio ya ngono ni jambo ambalo halikwepeki kwa kiumbe asiye na kasoro .Hii ndio njia inayotufanya binaadamu tuwepo duniani mpaka leo hii. Labda ni kweli kuwa katika kila janga wapo wale watakao shinda majanga na kuendelea kuishi. Lakini je katika hao watao kuwemo katika kikundi cha survivor of the fittest na sisi tutakuwepo?Du ngoja nikaoge! Sijafanya Zuma staili lakini, nimetoka mazoezini:-)

8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Reggy's 1:12 pm  

KARIBU SANA KITURURU. Nimefurahia kitendo chako kujiunga na jumuiya hii ya wana magazeti tando. karibu sana, ujisikie nyumbani. Cha maana zaidi ni kuwatembelea wenzio na kuchangia hoja zao ili nawe upate wageni na kufahamika zaidi.

HOJA:
Kuhusu Ngono, nijuavyo, binadamu ana uhusiano mkubwa na ngono. Ni sehemu ya maisha yake na ngoni ni yeye mwenyewe.

mloyi 1:57 pm  

Kitururu, sio Ras Kitu, nakumbuka jina kama hili miaka ya tisini!
Unaongelea saikologia, vizuri kupata mawazo haya. Tunazidi kukua na inawazekana sasa tuna kila aina ya mawazo kwenye mtandao wetu. Mwandani katutambulisha kwako ndio maana nimekuja hapa nikuone unachoandika. Karibu sana tutaendelea kutembeleana.

Simon Kitururu 11:58 pm  

Asante Reginald , najitahidi kuingia hapa.Mzee Mloyi ni mimi kuna anga nyingine watu huniita Ras Kitu au Kit.Tukopamoja.

boniphace 1:08 am  

Karibu mzee naona umekuja kikweli kweli maana ulishavaa kombati na kila kitu umeweza kuanza nachp. Umenikumbusha wakati naanza kusaka kufungua Gazeti Tando languilivyokuwa tabu kuweka picha lakini wewe umeanza nayokabisa. Nitakuwa nikipita hapa kupata usafiri wa mawazo maana treni yako naamini haitakuwa kama ile ya Kati ambayo niliapa sisafiri tena na treni ile baada ya usafiri wabngu wa kwanza kunitoa Dar hadi Moro kuchukua 12 hours.

Simon Kitururu 1:59 am  

Boniphace Umenikumbusha mbali! Nilishawahi kusafiri kwa Treni kutoka pale dodoma mpaka Morogoro katika daraja la tatu, nikakoma mwenyewe:-) Lakini afadhali sisi Nilikuwa naongea na Mnigeria mmoja leo kaniambia huko kwao sasa hivi hazifanyikazi kabisaa.Treni hii ya mawazo haina mushkeli lakini.

Christian Bwaya 1:34 pm  

Hili suala la ngono lina upana wake.

Kwamba kibaolojia kila kiumbe huvutiwa nalo hasa "hasa Homo sapiens" mwenye utashi na ufahamu ambaye hulitumia tendo hili, si kwa uzao tu kama wafanyavyo viumbe wengine, bali hata kwa starehe.

Starehe hii bahati mabay hufanywa hata kama inaeleweka kwamba inaweza kuleta matatizo fulani fulani kama UKIMWI na mimba zisizotarajiwa.

Inasemekana mawazo kuhusu tendo hili yanatawaliwa na homoni zenye kumbadilisha mtu kutoka "hiari" mpaka "si hiari". Inapokuwa hivyo basi maswali yanayokuwa yanahusiana na hatari yanakuwa hayana nafasi.

Lakini pia nguvu ya homoni hizi zinamtegemea mhusika. Akijiendekeza sana, zinamkong'ori sawasawa na anavyojichukulia mwenyewe. Anajikuta akiendeshwa zaidi ya anavyoendeshwa mdudu katika hili.

Nadhani tunaweza kujidhibiti tukitaka.

Rama Msangi 10:42 am  

Natumai na ninaamini kabisa kuwa Treni hii sio ya makaa ya mawe au ya Umeme, maana na huu mgao wa umeme nadhani ingekuwa shida sana kuipanda. Ila naamini Treni hii ya Mawazo, inatumia zaidi Busara, fikra thabiti, ishara za nyakati na maono yatokanayo na namna tunavyoitizama historia yetu, kwahiyo nina imani nayo sana

Simon Kitururu 11:10 am  

Ndugu Msangi nashukuru kwa kuwa na imani na Treni hii. Kama ulivyosema treni hii inamatatizo yake katika jitihada hii ya kufika katika safari yetu ya kuelimika, kuelimishana na kwa ujumla katika utanuaji wa mawazo ilikufikia matatuzi ya matatizo yatukabiliyo katika maisha yetu ya kila siku, na pia kuwa na busara katika kufurahia majawabu yanayopatikana katika safari hii. Umeme ukikatika itahitaji makaa ya mawe, nayo yakiisha, madiseli, hataikiwezeka kusukumwa na watu.Tukopamoja Mzee!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP