Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NI NINI SILIKA YA TANZANIA?

>> Monday, May 22, 2006




Nimejaribu kutafsiri kichwa cha habari hapo juu kutoka kwa Kiingereza.'What is Tanzanian National Character?'. Nimependa kuingiza kiingereza chake kuonyesha ni jinsi gani lugha za watu zinavyoathiri hasa ukizitumia kusoma kwa muda murefu. Unaanza kujikuta unababaika kupata maneno ya lugha yako ya asili. Narudi kwenye hoja.

Tanzania tunapenda kuamini kuwa kunakitu kimoja kinachotuuunganisha, nacho ni Utanzania. Lakini kuna mambo mengi tu ambayo yanafanya Watanzania wawe na majibu tofauti waulizwapo kuhusu Tanzania na Utanzania. Kuna maswali mengi Waislamu na Wakristo hutofautiana majibu, Wasomi wa shule za vitabu na wale wa shule za kitamaduni hutofautiana majibu. Wanawake na wanaume hutofautiana majibu, Wazanzibar na Watanganyika hutofautiana majibu, pia watu wa makabila tofauti hutofautiana majibu.

Katika safari zangu Ughaibuni na hata bongo ni mara nyingi nimejikuta na jizuia tu kuingilia hoja kutokana na kusikia mtu akielezea Tanzania na Utanzania tofauti na ninavyouelewa mimi. Mara nyingine nimejikuta na mtambulisha mtu kuwa ni Mtanzania, halafu yeye akakataa nakusema yeye ni Mzanzibari. Pale Zanzibar pia nisha kuwa naongelea kuhusu sisi Waafrika nikakanwa na mtu tuliye fanana naye akiniambia yeye ni Mpersia. Siku nyingine nilikuwa na ongelea usawa Tanzania nikajikuta naambiwa Waislamu bongo hawajapewa usawa kielimu. Nika ongelea jinsi Watanzania walivyozoea kuwa na viongozi wa kike tofauti na nchi nyingine za kiafrika. Nikichukulia data za Wanasiasa wanawake ambao wako katika serikali, nikaambiwa wale nimapambo tu hawana nguvu. Kitu kibaya tu ni kwamba maswali kama haya mara nyingi yanazuka muulizaji akiwa ni wakutoka nchi za kigeni. Halafu kuna kile kitu ambacho sikipendi ambacho hujitokeza. Dalili ya kwamba tunapingana. Ingawaje nawezakusema sisi tuna nafuu katika Afrika Mashariki ,ukilinganisha na Kenya na Uganda, lakini hili swala bado ni la kutupia jicho.

Sasa Je ni nini maana ya Utanzania kama tunauelewa tofauti tofauti namana hii. Mimi nafikiria kuna mambo yafuatayo ambayo yanaweza kufungua macho kwa nini Watanzani pamoja na Utanzania wetu , mara nyingi hatuna majibu sawa. Kwa mtazamo wangu hizi ni baadhi za elementi zinazochangia silika ya Mtanzania, na pia kuwepo kwa majibu tofauti tofauti mengi. Ningependa kupata nyongeza kwa wanamagazeti wa Mtando.

1.Watanzania wako ororo (sensitive) na swala la Utaifa. Hili linatokana na historia ya kutawaliwa na pia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao mpaka leo unamushkeli. Kazi ya kujenga identiti ya Mtanzania haijafikia upevu.


Picha kwa hisani yaISSA MICHUZI
Usingeweza kujua kua tokea siku hii ya muungano pichani mpaka leo swala la muungano bado linamushkeli.



2.Watanzania ni watu wenye vichwa ngumu kisirisiri.(passively stubborn people). Mpaka leo ni rahisi sana watu kudindisha kufanya jambo ili tu kupruvu jambo. Bado maoni ya wakoloni yana nguvu katika mawazo ya Watanzania.Kuna mawili yanaweza yakatokea, kukubali kirahisi kwasababu Taifa linalosema limeendelea au kudindisha bila ya sababu maalumu. Yote haya huweza kutokea bila ya mtu kukuambia usoni. Bosi Mkaburu anaweza akadindishiwa hata kama anasema ukweli ili tu kumwonyeshea hapa sio Zimbabwe. Maoni kwa wawekezaji- epuka kuweka mazingira ya kazi yako kutoa picha ya Mnyampara na Mtumwa.Kwa Watanzania utashindwa wewe.

3.Watanzania ni watu wanaoathirika na dini sana. Mtu hata kama sio Mkristo au muislamu , kuna kitu tu kina muathiri kiimani. Lazima kuna imani fulani anaifuata na ambayo ina mambo yanayomtisha. Kwa Wakrristo na Waislamu ni jehanamu , lakini kwa wengine wote kuna kakitu tu katakacho kueleza ebwana msitu huu usiingie usiku au du ukifanya hivyo, jasho litakutoka nk. Halafu katika Waislamu na wakristo bado kuna katatizo au kamvutano ambako kako kwa chinichini. Kwa mtazamo wangu bado waislamu wengi bado huamini kuwa Wakristo hufaidika zaidi na Serikali. Na Wakristo wengi huona waislamu kama hawachuki muda kurizoni baadhi ya mambo kabla ya kuchukua hatua.

4.Watanzannia kwa ujumla wanapenda siasa. Siasa tokea kabla ya uhuru imechangia kujenga silika ya Watanzania. Lakini Siasa za Nyerere za chama kimoja bado zihazijaweza kuwatoka watu akilini. Uzuri wa siasa za Nyerere zimekuza umoja wa Watanzania. Lakini kuna uwezekano wakuvunja umoja bado hasa kupitia mambo ya husuyo dini. Siasa ya vyama vingi bado ni changa sana kuonyesha makucha yake bado.

5.Asilimia kubwa ya Watanzania hawajaelimika vya kutosha. Hii husababishwa na mfumo wa elimu ambao bado umeshindwa kumkomboa Mtanzania kutoka katika utumwa wa kifikira na pia kushindwa kumuwezesha Mtanzania kujikomboa kiuchumi hata pia kiafya.

6.Tanzannia ni bado ni nchi yenye ukabila.(Tribal Nation). Bado ukabila umeshikilia mambo mengi. Kuna baadhi ya makabila bado yananufaika zaidi ya mengine, kielimu ,kiuchumi, nk. Kuna sababu nyingi kweneye hili. Kuna maswala ya idadi ya watu kwenye kabila,mahala lilipo kabila,udini, elimu , nk.

7. Kiswahili ni Jambo moja ambalo linaunganisha Watanzania. Katika Jambo moja ambalo Watanzania huwa na jibu moja ni katika umuhimu wa Kiswahili Tanzania. Lakini kiswahili kinakuwa butu kwa wasomi wengi kutokana na kutotumika sana katika elimu ya juu. Hivyo asilimia kubwa ya wasomi hawana maneno ya kiswahili ya kuyatumia kuelezea taaluma zao.

8. Kwa mtazamo wangu watanzania ni watu wachapakazi lakini ni watu wafanyao kazi polepole.



Ongezeeni au kosoeni wana mtandao.........................

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

mwandani 4:34 pm  

Passive stubborn - pamenikuna kidogo hapo

Simon Kitururu 6:16 am  

Kwa mtazamo wangu wako hivyo.Wanadindisha lakini si rahisi kuwaona wakidindisha kama mitaa ya Uarabuni wakiona katuni fulani fulani:-)

Jeff Msangi 11:42 pm  

Mimi nadhani watanzania tu wavivu.Hatupendi kazi,hatuheshimu kazi badala yake tunakesha tukiota utajiri,ufalme na umalikia wa kirahisi rahisi tu.
Pengine hii ni mojawapo ya yale madhara ya minyororo ya kikoloni ambayo Naim Akbar anaizungumzia katika lecture zake na vitabu vyake.
Watanzania hatuna moyo wa kujitolea.Tunataka kulipwa hata kama ni kwa ajili ya maendeleo yetu.Mtu akijitolea kupeleka maji safi kwa bomba kwenda kijiji fulani akaomba nguvu tuya vijana,hatopata mtu kwani wote watamuuliza.."unalipa bei gani"?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP