LIKITOKEA NIGERIA ,LIMETOKEA KWA AFRIKA NZIMA.
>> Tuesday, May 23, 2006
"What do you want me to do?" Akin asks in pidgin English, explaining why he turned to a life of Internet crime. "It is my God-given talent. Our politicians, they do their own; me, I'm doing my own. I feed my family - my sister, my mother, my popsie. Man must survive."
- Ndio asemavyo mtoto Akin kama anukuliwavyo na CNN.
Inasemekana katika kundi la Waafrika watano kuna uwezekano kuna Mnigeria mmoja. Hivyo utaweza kunielewa umuhimu wa Nigeria katika picha ya Mwafrika ionekanavyo duniani. Kinachosikitisha mpaka sasa hivi Nigeria pamoja na utajiri wake ,wasomi wake, na idadi ya watu iliyonayo inahangaika kuweka mambo sawa. Siasa ya Nchi hiyo haijatulia bado.Nigeria hata siasa zizungukalo jambo la idadi ya watu ni gumu sana.Wakaskazini kule kwenye jangwa jangwa ndio wanasemekana wengi na ndio wana chukua rudhuku kubwa kutoka serikalini.Ruzuku inasemekana hutolewa kutokana na idadi ya watu.Hivyo unakuta kule kunakotoa mafuta ambako ndio kusini kutokana nakuonekana kuwa kuna watu wachache basi kuna pata ruzuku ndogo. Wengine wanadai kaskazini kutokana na kuwa na viongozi wengi wakijeshi waliopita ndio maana waliweka maswala kupendelea kwao.Kwani kila siku watu kusini wanajiuliza, inawezekanaje kule kaskazini kwenye janga kukawa na watu wengi kuliko sehemu zenye chakula na ardhi nzuri? Kitu kingine cha ajabu ni kwamba wasomi wengi wa Nigeria wametokea kusini, lakini viongozi wengi walioongoza nchi wametokea kaskazini. Babangida na Buhari ni miongoni tu mwa viongozi wazamani wakijeshi wanaotakakurudi.
Hivyo ukimchanganya na Atiku(pichani)aliyekuwa makamu wa Raisi wa Abasanjo basi mwakani tutasikilizia uchaguzi wake. Naombea uende salama. Ingawa habari kama hizi maranyingine huleta utata ,ila inabakia palepale kuwa Nigeria ikitulia kuna sehemu kubwa tu ya Afrika itafaidika.Ingawa imejitahidi siku za karibuni kulipa madeni ,bado kuna mambo kibao yanayo itengenezea nchi hiyo na Afrika jina baya.
Katika kitu kinachonishangaza ni kwamba zile e-mail za kutoka Nigeria zinazozunguka mtandaoni kumbe bado zinawadaka watu. Lakini kama hazikukudaka zile basi je, zile pesa ulizotuma kwenye Western Union ,au ile Moneygram ilifika? Kongoli hapa
Ibrahim Babangida
Mwanajeshi kutoka kaskazinni ya Nigeria anayesemekana anapesa kama vumbi. Usijeukashangaa siku moja kuambiwa tajiri kuliko wote duniani sio Bill Gates ila Mnigeria mmoja ambaye haijulikani alifanyakazi wapi.
8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Nimekusoma bwana Kitururu. Naona umekuja mzuri sana. Tupo wote
Simon, umekuwa kati ya wasomaji wa blogu zetu kwa muda mrefu. Sasa umeamua kutia mguu majini. Naamini wengine watakubaliana nami kuwa umeingia kwa nguvu na kishindo. Naamini tutafaidika kwa mawazo na maoni yako. Karibu sana.
Mzee Custo, nazidi kusoma na kufikiri. Shukrani kwa changamoto. Naona bado uko makini na macho yako bado maangavu kama mwana mbweha.
Ndugu, Nkya, Ndesanjo, Mwandani, tukopamoja. Imenibidi nijiunge nanyi kwasababu si utani mawazo yenu yamenifunza mengi. Najaribu kuchangia na mimi fikra zangu kwasababu naamini umoja ni nguvu.
Bwana Kitu karibu hadi ndani!
Ninaamini treni yako ya mawazo itatufikisha tuendako salama salimini.
Nina swali kidogo hapa, kuna picha kwenye ile habari ya Mnaijeria Akin ameshika tama, nilivyosoma kabla sijashuka chini kwenye habari zingine nikajua ndiyo Mtoto Akin mwenyewe, nilivyoshuka nikaiona tena, nikasema Bwana Kitu kaweka kiungo cha picha ya Akin kwa bahati mbaya..sijui hajaona?..nikashuka tena nikaona, sasa nikabaki najiuliza huyu ni Akin au ni yeye mwenyewe?
Karibu sana.
Mija Huyo si Akin. Huyo ni Simon akiwa katikatika Treni ya mawazo.
Simon,
Kwa mtizamo wako unadhani uhalifu unatokana na umasikini,mazingira,tabia au vyote kwa pamoja?Ninapoweka maoni haya hapa watanzania huko Texas nao wameungana kwa kishindo na kundi hili la wanijeria.Jumapili iliyopita kwa bahati mbaya niliangalia CNN(nasema bahati mbaya kwa sababu huwa siangalii CNN)nikaona kipindi cha CNN Presents ambacho walikiita How To Rob A Bank.Mambo yote yalikuwa juu ya wanijeria na mipango yao hii ya wizi wa kutapeli na kupora.Nini chanzo unadhani?
Jeff, mimi ninadhani vyote vinachangia sasa hivi. Kikubwa ni kwamba sasa hivi Afrika tunao role models wengi ambao wameonyesha unaweza ukaiba halafu usichukuliwe hatua au huwezi hata kushikwa. Wizi na ujanja vinafananishwa sana.Angalia akina Babangida, Ukimsikiliza Fela Kuti utasikia jinsi Obasanjo alivyofanya kipindi kile alivyokuwa Raisi mara ya kwanza.Turudi nyumbani pia.Wezi ndio wenye pesa.Hivyo haya mazingira yenyewe yanaonyesha watu kuwa ibeni.Umasikini unachangia vilevile.Kwani nikama catalyst katika kuwapa msukumo watu kujaribu,hasa katika jaribio la kwanza la kuiba.Baada ya fanikio la kwanza la kuiba kufanikiwa basi inakuwa ni tabia tena. Tabia inafunzika.Hivyo Mazingira yakiiruhusu tabia ya kuiba na kukatisha njia fupi basi inakuwa ndio utamaduni. Mimi naamini binadamu kwa asili ni wavivu. Angalia kilakitu mpaka tekinolojia hii tuitumiayo imelenga kurahisisha mambo.Ngazi,baiskeli,gari,trekta yote ni kwaajili ya kukidhi mahitaji ya binadamu kupata mahitaji yake kirahisi. Tatizo ni kwamba sasa hivi kutokana na utu kutothaminika basi watu wameingilia mpaka kujitajirisha kirahisi.
Post a Comment