Dhamira ya Mtanzania Je Itafufuka?
>> Wednesday, May 17, 2006
Mimi siwezi kujiita mwanadini niliye kubuhu wala Mtanzania bora. Lakini katika kukua kwangu pale Tanzania nimeshuhudia jinsi gani Mtanzania alivyowezakubadilika tokea yule ambaye kuvunja sheria ilikuwa ni aibu mpaka yule ambaye imekuwa ni ujanja.
Kama mtu niliyekulia katika maadili ya kidini ni vigumu kuyakwepa maadili haya katika kuongelea swala hili, ingawa naamini mfano huu unaweza kutumika bila ya kunukuu dini yoyote . Katika maisha yangu nimefikia hitimisho kuwa kila siku unapoendelea kurudia kutenda tendo livunjalo maadili ya dini ndio jinsi moyo na ubongo unavyozidi kulitambua nakulipa uhadhi wa ukawaida au kulihalalisha. Kitendo cha ndoa nje ya ndoa kwa wanadini nijambo ambalo linatisha katika hatua za mwanzoni mpaka kinapozoeleka mpaka hata kile kijisauti cha pili(dhamira) kinachoingilia kutaka kukatisha maamuzi, kwa kumtaka mtu afikirie kwanza busara ya kuendelea na shughuli za uroda nje ya ndoa kinapokufa kabisa. Pale kile kijisauti kinapokufa basi mtu hasiti tena. Kila nafasi inapotokea maswala yote ruksa.
Dini inawezaikawa ni mfumo wowote ambao unamjengea mipaka mhusika katika kuonyesha ninini sahihi na nilipi potofu. Lakini dini ninayoiongelea hapa ni ile ambayo mwanadamu yeyote anakuwanayo ikilindwa na dhamira binafsi.
Tukiangalia kuanzia maswala ya rushwa mpaka uzembe kazini, utaonakuwa kuna wakati ilikuwa sio ujanja kufanya hivyo. Enzi za mababu zetu ilikuwa ukiwa mzembe kama ni mwanamume, hata mke inakuwa vigumu kupata. Kwa akina dada unaonekana unatabia mbaya hivyo sio mwanamke nona kwa ndoa. Sasa utashangaa imefikia wakati ambao ujanja ni kuwa laini au kulia ofisini. Ukiwa katika ofisi ambayo watu wanajua utaweza kirahisi kuiba fedha utasikia watu washaanza kusema naona uko jikoni, usipojenga wewe basi mjinga. Unakuta jamii nzima inategemea kuwa sasa utaonyesha mambo- maana uko jikoni. Na kuua dhamira au kile kijisauti haitakuchukua muda.
Sababu ziko nyingi ambazo zinabeba lawama yakuwa ni chanzo cha yote haya. Hali ngumu ya maisha, mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yameleta upungufu wa chakula, maswala ya ukiritimba katika mfumo mzima wa serikali na vikorokocho vyake nk. Jambo lakujiuliza ni kwamba je dhamira ya Mtanzania inawezakufufuliwa? Mara nyingi nirahisi kuwa tuna laumu tu bila ya kujaribu kupata majawabu ya matatizo yetu. Sheria pekee haiwezi kusawazisha mambo kama akilini mwa wananchi hakuna kijisauti kinacho wasuta kuwa wafanyalo si ujanja na si jambo lakujivunia. Mimi nafikiria kuwa Watanzania turudie kule tulikotokea , mafunzo ya maadili mema yapewe kipaumbele tokea shule ya vijidudu. Hata Propaganda za zamani zirudishwe.Mkabaila tulimuimba na hata yule Mnyampara. Propaganda za maadili mema zianzishwe tokea shule za vidudu tena. Nakumbuka niliimba kuhusu kaburu na ubaguzi wa rangi mbaya na nikamchukia kaburu tokea shule ya vidudu bila ya kujua ubaguzi wa rangi ni nini. Iliwezekana miaka hiyo itawezekana tena naamini.
Propaganda za kumwezesha Mtanzania kujiamini tena kuwa maisha yanawezekana kihalali ianzishwe tena. Mtanzania wa leo siye yule aliyekuwa anajiamini. Mtanzania wa leo anatakiwa ajiamini kuwa kuna mambo mengi tunaweza wenyewe. Kumbuka wenzetu kutokana na matatizo ndio wanapata ujasiri wakutatua matatizo. Angalia Brazili matatizo ya petroli wameyatatua kwa kuzalisha miwa anakutengeneza ethanol.
Nafikiri Tanzania ilikuwezesha kurudisha imani na Utanzania inabidi tujenge utamaduni wa kuwaenzi Watanzania mahiri na pia kujaribu kuwasaidia wale wanaoonyesha dalili za umahiri. Sioni sababu kwanini vyuo vyetu vikuu haviendeshi stadi za kuboresha mambo yajitokezayo nchini ambayo yakiboreshwa yanakuwa ni bora na ya Kitanazania. Sidhani kama kuna hata mkufunzi mmoja anaye wasoma mama ntilie kwa nia ya kuwawezesha kuboresha bidhaa zao zifikie katika hatua ya mbele. Sido haikuwasaidia akina mchaga kajitaihidi .Hivyo hata siku moja yule fundi viatu hakuweza kupiga hatua kuenda mbele.
Tunabidi tuwaenzi watu wanaoishi kihalali na wanaochangia maswala ya Taifa na kuletea sifa nzuri Taifa. Ningefurahi ikiwa tunaweza hata kuwaenzi watu hawa hata kwa ma sanamu na mapiramidi ikiwezekana. Na wale ambao wanavunja sheria hasa kwa kujinufaisha wao wenyewe wahadhirike mpaka wasiwe watu wa kuigwa. Serikali ni wananchi hivyo wananchi inabidi wajisikie kuwa wako pamoja na serikali yao na sio ukimuona polisi hata kama huna kosa unaanza kujihami. Kwa maswala ya polisi mimi na husudu mapolisi wa Skandinavia kwa jinsi wanavyohudumia watu wao. Tokea shule ya vidudu huwa wanatembelea kuelezea ni nini wanafanya. Ni wale watu ambao wagonjwa mpaka walevi waliozidiwa wanapata msaada wao.Ukizidiwa ulevi Unawezwa kupelekwa na nyumbani kama hawako na shughuli nyingi.Nakumbuka bongo mara nyingine hata rafiki yako akiwa polisi unaadha kujihami asije akakufanyia vibaya. Sasa katika kipindi ambacho Kikwete anasema kana kwamba analeta ari mpya basi tufufue na kadhamira ka zamani.
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Nimekubali.
Simon,
Usione kama naibukia kila kona ulipo kama mzimu,hapana.Majuzi tumekutana kwenye graduates.com na leo nakuona umetinga ndani ya blog.Ni raha ilioje.Karibu sana
Mapinduzi uliyoyaongelea kwenye makala yako ndio jambo ambalo nadhani wanakijiji wa blog tunajaribu kwa njia zote,kila siku kuyaamsha.Tunaamini kwamba ukombozi wetu uko kwenye fikra,utumwa wa fikra umetula kama kansa.Wakati umefika sasa tuseme basi.Turudi kwenye jadi zetu,sio kwa kuvua nguo na kutembea na vibwaya bali kwa kuzingatia yale maadili yaliyowajenga wazee wetu.Mwingine atasema wale ukoloni uliwatawala,mimi nitauliza kati yetu vijana wa leo na wazee wetu,nani ametawaliwa na ukoloni-fikra?
Ndio Mzee Jeff imebidi nijiunge katika kijiji. Nimekuwa nasoma blog yako kwa muda sasa. Nilikuwa natafuta sababu kuwa sina muda wa kublog mwenyewe. Bado sija imasta art ya kublog vizuri lakini yote mbele kwa mbele nimeamua kujifunza kwa vitendo.Tuendelee kupeana fikra ilitwendelee kwenda mbele
Post a Comment