Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UKOMBOZI WA MTU MWEUSI DUNIANI KWA MTINDO WA SUN TZU

>> Tuesday, May 23, 2006

*All warfare is based on deception

*Hence, when able to attack, we must seem unable; when using our forces, we must seem inactive; when we are near, we must make the enemy believe we are far away; when far away, we must make him believe we are near.

*If your opponent is of choleric temper, seek to irritate him. Pretend to be weak, that he may grow arrogant.

*If he is taking his ease, give him no rest.

*Attack him where he is unprepared, appear where you are not expected.

*Now the general who wins a battle makes many calculations in his temple before the battle is fought.
[Chang Yu tells us that in ancient times it was customary for a temple to be set apart for the use of a general who was about to take the field, in order that he might there elaborate his plan of campaign.]

The general who loses a battle makes but few calculations beforehand.


- Sun Tsu.


Ukiwa unasoma historia inamaana kwa kiwango kikubwa unasoma mambo ambayo hayakuandikwa na mtu mweusi. Huhitaji kuwa mtu mwenye akili nyingi kugundua kuwa hili ni tatizo kubwa. Asilimia kubwa ya historia imeandikwa na watu ambao hawakumjua mtu mweusi. Baadhi yao walikuwa wanamuogopa mtu mweusi,wapo ambao walimuona kama ni chombo cha kufanyisha kazi, wengine walikuwa wanamchukia na bila kusahau waliokuwa wanampenda, lakini si kwa kumlinganisha na wao bali kwa kumuona ni kiumbe kifurahishacho macho na pengine kinogacho katika maswala ya uroda. Hatuwezi kuwasahau pia waandishi ambao waliandika kuhusu watu weusi kwa ajili ya serikali zao ilikuhalalisha mtazamo wa serikali zao na watu wao ilikumdhalilisha mtu mweusi.

Watu weusi ambao asilimia kubwa wanatokea Afrika tulitumia sana masimulizi zaidi ya maandishi kujua historia zetu. Na baada ya mkoloni kuna asilimia kubwa tumeacha kabisa kufuatilia historia zetu kama mababu zetu walivyokuwa wakiijua. Tumechukua historia iliyoandikwa na watu wengine kama ndio ukweli mtupu kuhusu sisi.Pia kuna asilimia kubwa ya historia yetu imepotea kabisa!

Kumbuka sio muda mrefu dunia nzima ilikuwa iko katika usawa kitekinolojia na hata kiuchumi. Ukifuatilia utakuta kuwa Mtu mweusi alikuwa si mtu wa kudharaulika. Ningependa ukumbuke, katika dunia yenye teknolojia moja changa au isiyo na tekinolojia, ni mabavu tu yanayotumika kuishi. Bila kufikiria sana, tabaka la watu ambalo lingeweza na liliweza kuhimili kirahisi mazingira ni la watu weusi. Tuchukulie mifano ya leo hii katika dunia iliyotawaliwa na Televisheni za Marekani. Bado michezo yote ya nguvu inatawaliwa na watu weusi.Kuanzia Futiboli ya kimarekani, Baseball, basketball,riadha nk. Ukirudi nyuma ndio kabisa, watumwa weusi walitumika zaidi kwa sababu ndio waliokuwa wakihimili zaidi shuruba za nguvu.

Sasa kwa nini watu wenye nguvu wakawa watumwa? Kuna sababu nyingi lakini mimi nasisitizia hizi mbili. Nguvu za mtu mweusi ndio zilizomletea unyonge mtu mweusi. Kwa kuwa na maguvu akachelewa kurahisisha vyombo vya kazi na pia silaha. Hii ikamsababishia kushindwa waliporudi watu wengine na silaha zilizo bora zaidi. Pili , hatukumjua adui na pia hatukujijua kuwa nguvu za misuli yetu zimepitwa na wakati.

Matokeo yake ni sasa mtu mweusi anaangaliwa kama mtu wa chini na jamii zote nyingine. Hii namaanisha Wazungu, Waasia wa jamii ya kichina, kihindi,waarabu na wengine wote. Sasa hivi wenye nguvu ni wao, hivyo kumbuka wakati sisi tunanguvu walifanikiwa kutupindua.Je unafikiri sisi tutashindwa kupindua meza? Haina haja ya kufanya kama wao . Lakini naamini kabisa tunauwezo wakulinganisha mambo.Si lazima tuwapindue, haiko katika silika ya mtu mweusi kwa mtazamo wangu.


Hapo ndipo tunapokuja kwa SUN TSU. Kitabu chake nilikipenda ningependelea ukisome kitabu chenyewe.Lakini hapa naweka kongoli upitie baadhi ya tafsiri ya kitabu hiki kwa kiingereza. Huyu mchina aliandika kitabu hiki muda mrefu sana kabla ya Yesu kuhusu vita. Kwa mtazamo wangu watu wote weusi tuko vitani kumkomboa mtu mweusi. Na kama ni vita basi lazima kuwe na mipangilio ya vita(Strategies).
Jambo la kwanza inabidi tuwajue hawa watu wa utaifa (race) mwingine.Ikibidi kila kitu juu yao kama inawezekana. Kongoli hapa The art of War kilicho andikwa na SUN TZU (Ingawa kuna baadhi ya wasomi wanahisi sio yeye aliyeandiaka). Some ukiweka mtu mweusi katika fikra zako.
Katika kitabu hiki jambo ambalo narudia kusema kuwa linanigusa sana ni umuhimu wa kumjua unayepigana naye na pia umuhimu wa kujijua mwenyewe. Ingawa kitabu hiki kimeandikwa miaka zaidi ya efu mbili iliyopita kinauwezo wa kumkomboa mtu mweusi leo hii. Kuna maswali ninayo jiuliza kila siku. Je sisi watu weusi tunajijua? Je tuna wajua hawa watu wenye utaifa (race) nyingine?

Hili si jambo la kivita tu. Usipo wajua hata mahusiano yako ya kimapenzi nao hayawezekani. Usipojijua hukawii kujikuta unatumika kisawasawa bila kujua , kwa maana nyingine unarudi Utumwani.


HEBU TUANGALIE WATU WEUSI TUMEFIKIA WAPI LEO:

1. Asilimia kubwa ya Wasomali(atleast in Scandinavia) hawakubali kuwa ni Waafrika weusi bali wao ni Waarabu.(Sisemi kuwa ni kila mtu katika kundi hili ila asilimia kubwa)

2. Waafrika weupe weupe kidogo kama Waithiopia na WaEritrea wengi niliokutana nao wanaamini wao ni Babu kubwa(Superior) kuliko Waafrika wengine weusi. Hii ni pamoja na Wasomali ambao walikuwa wana waonea Wasomali wenzao Wabantu. (Sisemi ni kila mtu katika kundi hili ila asilimia kubwa)

3. Tiger Woods hujaribu sana kujieleza kukwepa asilimia ya Uafrika aliyonayo.

4. Condoleezza Rice na Colin Powell wako kwenye timu ya George Bush.

5. Barry Bond achukiwa Marekani kwa kufikia rekodi ya Baby Ruth (mzungu) kwenye baseball.
6. Obasanjo alitaka kuendelea kutawala kwa muda wa tatu mfululizo.

7. Raisi Jakaya Kikwete asifiwa kwa jinsi aonyeshavyo maringo yake -dingili dingili mpaka chini.

8.Jacob Zuma ala uroda bila soksi na mtoto mwenye vijidudu vya UKIMWI
9.Tanzania bado hatuna uhakika na uwezo wakujilisha.
10. India, kwa weusi wa tabaka la chini hata kujulikana kisheria hawajulikani kama wapo.
11.Manyota wa hiphop kama akina P.Diddy wanaweza wakarekodi video wakiwa na wanawake weupe walioko nusu Uchi bila kunyongwa(Lynched) na Wazungu.

12.Asilimia kubwa ya watu weusi ndio walioathiriwa na vijidudu vya UKIMWI.(Ingawa hii inaweza ikawa ni porojo kutoka kwenye vyombo vya Uongo)

13.Simon Kitururu bado anaishi ulaya ambako Wazungu wenye msimamo mkali wameanza kuzidi kuongeza makali yao katika kuwashambulia watu weusi.

14.Bado Waafrika kibao tuna zama baharini tukijaribu kuzamia Uspaini kutokea Senegal na sehemu nyingine za Afrika Magharibi.

15.Oprah mwanamama mweusi atajirika kwa kuendesha shoo ipendwayo na akina mama weupe watu wazima Marekani

16..............

JE WATU WEUSI TUNAJIJUA? JE TUNAFANYA NINI?

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Jeff Msangi 11:33 pm  

Hoja hii ni nzito sana Simon.Lakini pamoja na uzito wake ni hoja halali kupita zote.Suala la kujitambua nadhani ndio mwisho wa reli-Kigoma wa maisha yetu.Kwa miongo mingi sana watu weusi tumepoteza muelekeo,hatujijui wala hatujui tuendako.Kama ulivyosema hili limechangiwa kwa kiasi kikubwa kwa masimulizi yasiyoandikwa kwenye vitabu.Wakoloni wakaja,wakatenda dhambi ambayo mimi binafsi nimeshindwa kabisa kuwasamehe nayo.Waka-colonize akili na pia habari za mwafrika.Wakaenda vichuguni wakaandika walivyotaka wao.Kwa upumbavu wetu tunakubaliana na mengi.Mimi nakataa yote,nahoji kila kitu huku nikiusaka ukweli.Lakini vita hii siwezi kuishinda peke yangu..ni yetu sote.Napata munkari nikiona watu kama wewe pia mpo mapambanoni.Lazima tujitambue,tuwafunze na wengineo.Historia tuiandike upya.Hatujachelewa.

Simon Kitururu 5:31 am  

Nakubaliana nawe kabisa Jeff.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP