Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KWENDA SHULE SI KUELIMIKA

>> Wednesday, May 17, 2006

Mpaka itakapofikia kuwa mfumo wa elimu wa Tanzania unaomwezesha Mtanzania kuweza kusoma na kuandika utakapomwezesha kuelimika ndio maendeleo ya Mtanzania yatakapo kamilika. Mtanzania akielimika Tanzania tulivyozungukwa ma Maziwa na mito hatutakufa njaa.Misri inakatizwa na mto mmoja tu na hawafi njaa. Watanzania tukielimika usindikaji wa mazao utaboreshwa, kwani tokea mababu walifanyahivyo. Lakini Watanzania si tunaenda shule?
Okei, nawezakukubali si wote wanaenda shule, lakini je wanaoenda shule wanaelimika?

Ninaamini kuwa mfumo wetu wa elimu Tanzania ambao mpaka sasa hivi haujafanikiwa kumwezesha kila Mtanzania kusoma na kuandika bado unachangia kuwafanya watu walioenda shule wasiweze kuelimika. Mfumo wetu waelimu unamfanya mwanafunzi kusomea mitihani. Nakumbuka Kutokea shule ya msingi mpaka kidato cha sita Bongo nilikuwa miongoni mwa kundi la wanafunzi ambao cha msingi ilikuwa ni kuhakikisha unafaulu bila hata kuwa na uhakika na mambo unayosoma. Na nina mifano mingi inayonizihirishia kuwa sisi hatuwa peke yetu. Tulikuwatunasomea mitihani. Unakuta mtu ana maswali na majibu ya mitihani ya miaka mpaka ishiri iliyopita. Halafu si ajabu ukifungua kitabu ukisoma, mshikaji akatokea akuulize, je unajua sehemu hiyo haitoi maswali kwenye mtihani? Basi hapo ndio inakuwa mwisho wa kuendeleza kuusoma ukurasa ua hata topiki hiyo. Unajikuta kila siku unasoma lakini hauoni hata maana ya baadhi ya mambo unayosoma yanavyoweza kukusaidia maishani. Matokeo yake hata kuchagua nini cha kusoma unategemea na ninini unasikia kitakupeleka kwenye kazi inayolipa. Utasikia chukua PCB hapana chukua PCM unajua ndio yenyewe. Mwingine anakuja kukuambia unajua viongozi kama akina Nyerere walisoma Arts na ndio hata akina Prinsi Wiliamu kule Wingereza ndio wanachukua masomo kama hayo, basi ilimradi tu mtu unajikuta unahangaika kuchagua. Chakujiuliza ni kwamba kwanini mfumo wetu wa elimu hautujengi kujiamini kusoma kile mtu akipendacho kutoka moyoni bila ya kutishika kuwa du , nikisoma hiki nawezakujikuta niko hatarini? Ndio tumekopa mifumo ya kigeni ilikujenga mfumo wetu wa elimu, lakini utasikia Uingereza ambako bado hawajaridhika na mfumo wao wanajadili kuubadili. Utagundua Wajerumani , Wamarekani, Waskandinavia, Wajapani ...nk wote ambao tunaweza kusema mifumo yao ya elimu iliwanufaisha ilitengenezwa kukidhi mahitaji yao. Je mfumo wetu wa elimu Tanzania unakidhi mahitaji ya kiellimu ya Mtanzania?

Mfumo ambao unashindwa kumwezesha mwanafunzi wa kiTanzania kujitegeme akimaliza shule, unaoshindwa kumwezesha Mtazania kujua haki zake na kumfanya mwanafunzi kupasi mitihani kwa kukariri, kwa mtazamo wangu unakasoro. Mfumo wa elimu ambao unatuacha kila mwaka kushindwa kutatua matatizo yajulikanayo mwaka nendarudi unamatatizo.

Kama elimu inapanua mtu mawazo basi elimu hii ifikie kutuwezesha sisi Watanzania kupanuka mawazo na kuweza kutatua matatizo yetu. Huko ulaya kwenye baridi waliweza kugundua vipashajoto nyumba, kwenye sehemu ambazo wanahali ya hewa inayowezesha kilimo kwa muda mchache waliweza kujaribu kulima kwa muda huo mchache( Ingawa kunaukweli kuwa mazao mengi wanayatoa nchi za dunia ya tisa). Sisi Tanzania bado hatujaweza kukuza tamaduni zetu za kuhifadhi mazao ingawaje tunajua tokea mababu walikuwa wanafanya hivyo. Utasikia bado upande mmoja wa Tanzania kunanjaa halafu upande mwingine chakula kinaoza. Elimu yetu basi au mfumo wa elimu wetu ukazie maswala haya. Kila mwaka sasa unasikia tuna upungufu wa vyakula. Je kuna utafiti wowote unaondelea wakukuza hata njia za kijadi za kusindika mazao? Haiwezekani ikawa kila mwaka tunakumbwa na tatizo hilo hilo. Hivi zile nyama za kukausha, viazi, mihogo ya kukausha inakwenda wapi? Hivi mbona ni zamani wavuvi waligundua kutumia chumvi kuhifadhi samaki sasa hivi zile akili zilizowafikisha kwenye hatua hiyo haziwezi kupewa changa moto tutuvuta mpaka katika kutatua matatizo ya sasa?

Halafu utashangaa nchi kavu kama Misri inayo pata maji kutoka mto Nile unaotokea kwetu hausikii wakilalamika njaa. Sisi Waafrika tunaotokea sehemu yenye maziwa makubwa Afrika tunakufa njaa. Sasa elimu hii tunayopewa kweli inatupeleka wapi ikiwa hata matatizo ya kila siku haitujengi kuyatatua? Utashangaa nchi nyingi za magharibi zina kijisehemu katika vyuo vikubwa kinachoshughulikia kutusoma sisi waafrika. Hutakawia kukuta kuna researcher aliyekubuhu kwa maswala ya siasa au kilimo cha Tanzania aliye Muingereza ,Uingereza. Tukikumbwa na njaa anaitwa BBC kuelezea matatizo yetu! Wanafanya hivyo sio kijinga tu, ili kuhakikisha wanatujua. Sasa Kama elimu yetu haitufanyi hata kuwajua hao watu wa nchi za nje na mazingaombo yao, basi si itufanye tujijue wenyewe na ituwezeshe kujitatulia matatizo yetu ? Siongei hapa kutaka kusema kuwa Tanzania ijitenge, ila ningependa elimu yetu ituelimishe basi. Maana kwa sasa inatufanya tuwe katika hali vuguvugu, nikimaanisha haituwezeshi kujijua ilikutatua matatizo yetu wenyewe na pia naona haijatuwezesha kushindana na mataifa mengine. Hata kidini vuguvugu si sehemu nzuri kubobea kwa muda mrefu. Ni heri Uwe joto au baridi ililijulikane moja.

Ningependa mfumo wetu wa elimu tuuangalie tena. Ninaamini elimu haina mwisho,vilevile elimu inaotakutu kama haipigwi msasa. Hivyo hata walienda shule na kuelimika ni lazima kupiga msasa elimu hiyo kwa maana baada ya muda inaweza kugeuka kuwa zilipendwa. Usitupe vile vitabu baada ya kumaliza kozi:-)

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

John Mwaipopo 5:35 am  

Karibu Kitururu.

Heri sasa tutapata mawazo mapya kutoka kwako.

Karibu.

Christian Bwaya 1:17 pm  

Hili suala la mfumo mbovu wa elimu yetu nimekuwa nikilifikiri mara kwa mara na hata kuliibulia mjadala na vijana wenzangu.

Pale kwangu niliandika kitu kidogo kwamba tuamue kubomoa bomoa kila ukuta na mapaa na kila kitu katika mfumo tulionao. Tuanze upya!

Kwangu mimi kuanza upya ni kuamua kabisa kufuta utaratibu wa ovyo wa kutunikiana vyeti, eti uthibitisho kwamba umekwenda shule. Wazo hili kwa haraka haraka linaweeza kuonekana ni la kiwenda wazimu fulani hivi.

Lakini hivi kweli cheti kinaweza kuthibitisha kwamba kilichoandikwa mumo ndicho kilichomo kichwani mwa mwenye nacho? Mbona hata hivyo vinapatikana siku hizi kama karanga? Mbona vinafanya wanafunzi wetu kukariri maadamu tu wakipate?

Aidha, umefika wakati tukaachana na kamtindo cha kusoma masomo fulani, si kwa sababu tunayaweza na ndiyo yaliyoshikilia mstakabali wetu, bali eti kwa sababu yanatija kwa maana ya ajira yenye fedha na heshima kwa jamii. Tumepoteza vijana wengi wenye uwezo, kwa mtindo huu wa kuwalazimisha kusoma masomo kwa sababu fulani fulani.

Baada ya porojo hizo, Bw. Kitururu karibu sana kwenye ukumbu huu wa mawazo huru.

Simon Kitururu 2:13 am  

Nakubaliana na wewe kabisa Bwaya na asante kwa kunikaribisha

Jeff Msangi 11:50 pm  

Kwa kuongezea tu,
Kabla wakoloni hawajaja na hiki kitu chao wanachokiita "elimu" hakuna mwafrika aliyekuwa anakufa kwa njaa.Kulikuwa hakuna magereza nk.Nini kilitokea?Hapo ndipo utakapogundua kwamba tunachokiita elimu hivi leo ni utumwa na msukumo wa umasikini,maradhi na kero zingine zote.Mababu wa mababu zetu ambao hawakwenda shule walikuwa wameelimika kutushinda sisi.Hoja nzito?

Simon Kitururu 8:06 am  

Mimi naamini kuwa kuna umuhimu wa kujua hii elimu yao.Hili nisawa na kumsoma adui yako.Tatizo naloliona ni kwamba tumeua elimu ya kwetu hivyo hatuna msingi wakujijua sisi wenyewe kama Waafrika. Kwa hiyo hata tusome vipi mambo yao bado tuko katika udhaifu kutokana na kwamba hatujisomi wenyewe.Kumbuka kila nchi ya ulaya ina Chuo kikuu chenye kitengo cha African Studies. Hivyo wao bado wanatusoma tu mpaka leo.Tusipobadilika hakuna ushindi tutakaopata kama Waafrika. Nakubaliana nawe Jeff kuwa mababu zetu walikuwa wameelimika, ila kwa mtindo huu hatutaweza kujua. Tutabaki tu kusikia,Ilikuwa mtu akivunjika mfupa, inachuku chini ya wiki mbili mfupa unaunga, na stori nyingine nyingi za namna hii.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP