Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MATATIZO ya kuwa huru wakati umeshazoea kuishi JELA!

>> Wednesday, August 19, 2009

Kuna wazoeao kuishi kijelajela na uhuru kwao ni ....

.....PRESHA!

Na kuwa huru kuna presha za kufikirishwa ufanye nini na uhuru ambao labda hata ukitaka kula WAWEZASTUKIA ghafla mpishi ni wewe na utajikuta tu unalazimika mpaka....

.....KUJIPIKILISHA!:-(



Na unaweza MPAKA kututangazia MAMBO kwa kuwa uko huru , ila kasheshe ni katika kutekeleza LA sivyo yatakushinda kama yalivyowashinda WATANZANIA hata baada yakututangazia wanuiayo kwenye lao .....

...... AZIMIO LA ARUSHA!:-(


Uhuru kitu cha ajabu kwa maana usipoangalia eti kwa kuwa tu uko huru waweza kujikuta kwa uhuru umeamua hata kidonda chako mwenyewe kwa kukosa vyakufanya kujazia uhuru....

....UMEKITONESHA!:-(

DUH!
Ni wazo tu MHESHIMIWA ingawa labda kuna ukweli kwenye hii HOJA!:-(
Swali:
  • Uko huru?
  • Unauhakika kuna aliye huru?

Hebu twende Gabon kidogo tupate Patience Dabany


Au tubaki tu Gabon tukutane na VIBRATION walete kitu -Mone Bone

Read more...

WAkati binadamu wanaendelea kumsingizia shetani VITU!

Kuna mambo binadamu anaharibu mwenyewe kibinadamu na LABDA wala shetani hausiki!

Na kuna mambo binadamu hahitaji baraka za Mungu kufanikisha, na LABDA ndio maana kuna wafanikishao mpaka umalaya , wizi, mauaji na ...... na kwa hayo labda MUNGU wala hausiki!


Swali:

  • Au?
  • Unauhakika kwa nini bado unaweza kukosea wakati unaamini Mungu na MUNGU yupo?

Ni wazo tu KINGUNGE na nakutakia siku KIBONGE!




Hebu TUENDELEE KUFIKIRISHWA kwa kumuangalia tena Saddam Hussein kabla HAJAUAWA NA WAHESHIMIWA , ambaye ni baadhi ya binadamu wachache waliofanikiwa KABLA YA KUFA kujua ni muda gani watakufa



AU ngojea JAGGED EDGE walainishe katika- Walk out of Heaven


Au tu tena JAGGED EDGE warudie wimbo huuhuuu- Walk out of Heaven katika hiii remix

Read more...

SHENZI mwanawane SHENZI![sentensi hii imebaniwa pua na msichana mwenye mafua:-(]

>> Tuesday, August 18, 2009

[Tahadhari: sina uhakika na maudhui ya taralira hii!:-(]
SHENZI mwaniwani SHENZI!!

LABDA kwa furaha umefurahishwa ,...
.... na kabla huja- NISONYA kama bado unaamini katika furaha wakati sifurahi unaweza tu mpaka kunitukana hata kwa zaidi ya SHENZI!:-(

SHENZI mwanawane SHENZI!

.... Halafu mtoto mzuri kama MALAIKA na kama unajua nakufananisha na MALAIKA unafikiri wakati UNANICHEKEA nitasikia au kujali yako ya KISHENZI?


SHENZI totoz SHENZI!

.....Na labda hata wakati tunachekeana yote ni UNAFIKI kama hatulengi nia na ingawa unajua wote sie katika tafsiri ni WASTAARABU bado nia yetu inaweza kuwa ni tufanye yatafsiriwayo kuwa ni USHENZI.:-(


SHENZI sista du SHENZI!
....sasa NTAFANYAJE wakati unajua chakukifanya labda ni kweli kimekunasia na tukileta jeuri ya kukitungua na kukifanya inaweza ikawa ni DHAMBI hata tukifanya kiustaarabu nafasi ikijitokeza na sio kwa kutaka kuhakikishia WATU ukweli KUWA kitendo chenyewe kama kilishafanikisha kuzalisha mtu labda si cha KISHENZI.:-(


SHENZI binti mrembo SHENZI!
... tukana tu KWA KUWA hata kama hupendi kubinuka au hata kutoa ukilala chali , hata ukiipigia magoti kwa afikiriaye kifanyikacho ni USHENZI hata umsomee ALBADILI atafanya akifikiria kuna uwezekano kifanyikacho hata kama kimebarikiwa na MZEE WA KANISA a.k.a SHEHE, bado HATA KAMA SIO WEWE bado kuna watakao kihusianisha na USHENZI!:-(

NALIKATIZIA WAZO HAPA na labda kama umenisoma mpaka sentensi hii kuna uwezekano ulichosoma ni USHENZI!:-(

DUH!




Hebu twende Angola KIDUCHU tukakutane na ya -BONGA

Au tu tubakie mpakani mwa KONGO na ANGOLA Ricardo Lemvo asemetena ya -MAMBO YOYO

Read more...

kama hata si kawaida unaamini MUNGU!

Swali:

  • Unauhakika wewe ni mjanja kuliko wasio amini MUNGU?

NI HILO tu na WALASIENDELEZI KUREMBESHA hoja!:-(


Hebu Sam Mangwana alainishe kwa kumsifia- KABIBI


AU tu twende tena Trinidad nimuachie CRAZY aongelee tena ya - CRUMBS

Read more...

MUNGU kama huwa kweli kunacho UNACHO BARIKI,kama inawezekana endelea KUBARIKI tena angalau hata KITOVU!:-(

Unajua imefikia mpaka kuna mambo tudhaniayo ni MAKUBWA,....


.... na inawezekana ikawa ni mpaka KWAKO KIKUBWA NI KULA na sie wengine WATU tumefikia KUFIKIRIA ingawa HATA katika kufikiria TUNASAHAU chakula cha kwanza hakikujua mdomo katika fikira na KATIKA kufikiria hasa KAMA sie kweli SI watoto wa chupa , tumboni kwa mzazi kumbuka HATA KAMA UNA domo kubwa SIKU HIZI kwa kula KOVU LA KITOVU ndio ulipo pata rutuba hata ya maharage na kwa kuwa hukumbuki ndio maana unasahau kwanini una KITOVU!:-(


Na labda siku hizi kuna wajifanyao wajanja na ukileta za kuleta wanaweza kukutisha eti yao ni MAKUBWA,....

...labda ndio maana KITOVU kimegeuka mpaka kudhaniwa ni KOVU na mengi hata YA wenye KITOVU wamesahau kwanini KWELI hata kama siku hizi una meno kama ngiri UMUHIMU au tu KWA NINI tuna KITOVU.:-(

Na katika KUBWA,...

... labda BADO wengine hawakumbuki hata KIDONDA ingawa tayari wana KOVU na labda bado wanafikiri kuwa wao ni SPESHO ingawa labda hakuna mtu spesho kama katika yote aliyonayo AJULIKANAYE KUWA NI MJANJA hata chini ya kitovu ukweli unabakia palepale kuwa HATUZIDI KITU KAMA YEYE kama sisi naye ana KITOVU.:-(


Swali :
  • AU

NI WAZO TU MHESHIMIWA usitishike na NIMEACHA!:-(

Hebu OASIS wabadili hali ya hewa kwa kitu - Wonderwalll



Au tu Tooots & Maytals wadai tena ya -54-46 was my NUMBER




ASANTENI WADAU WOTE wakiwemo hawa katika picha zangu za juzi ya jana....

Photobucket









Photobucket





Photobucket













Photobucket



Photobucket




Photobucket




Photobucket




Photobucket








Photobucket



Photobucket








Photobucket



Photobucket




Photobucket




Photobucket




Photobucket




Photobucket









Photobucket




Photobucket




Photobucket




Photobucket





Photobucket




Photobucket



Photobucket

















Photobucket




Photobucket



Photobucket

Read more...

Hivi NA HAMU kweli ya MWANAMKE au NA HAMU tu ya CHAKE kipengele hata kama sio UKE?

>> Sunday, August 16, 2009

Labda KATIKA hamu,...

..mara nyingi LABDA ukiwa na hamu ya MAGIMBI kunauwezekano huo ni msimu wa VIAZI!:-(


Na KATIKA hamu,...
....unaweza kula MAGIMBI kwa kuwa ni kweli unayapenda MAGIMBI , lakini LABDA ni ugali wa MHOGO unaoumisi mpaka KATIKA NDOTO na katika shughuli NI kweli ni UJI WA ULEZI UMEPEWA ambao NA bado upo INGAWA ni KWELI kuwa katika MAISHA YAKO na si katika NDOTO ZAKO huwa hupendi UJI achilia mbali UJI WA ULEZI, na kwa HILO hata usipotuuliza bado SISI twaweza JUA NINI KINAENDELEA na ukweli ni kwamba katika nyege zako za ugali wa sembe ukipata uji wa ulezi BASI katika hilo HIYO kama ni ndoto yako BASI hiyo ndoto ni JINAMIZI!:-(


Na KATIKA hamu,...
... hamu nyingine ni MATUSI ukizizungumzia INGAWA ukionja hata kiitwacho MATUSI unaweza kuguna kwa kunogewa na wakati umenogewa ukijaribu kuongea nasi hata kwa simu wakati unaendelea KUNOGEWA , .....SISI wengine tunaweza kudhani siku hizi WEWE una KIGUGUMIZI.:-(

DUH!
Mie Mtakatifu Simon KITURURU naachia hapa wazo na UKIENDELEZA WAZO SHAURI YAKO mie sikushiki KIBINDO!:-(



Swali:
  • Hivi ukiwa na HAMU YA MWANAMKE au MWANAMME huwa unafikiri unahamu yake MTU WOTE au unakuwa na hamu ya CHAKE tu KIPENGELE?

  • Hivi wewe kama MTU unauhakika kuwa MTU MWENYE HAMU YA MTU akimpata mtu anaukumbuka bado mwili wake wote na sio kama MIE MTAKATIFU SIMON KITURURU huwa anakumbuka baadhi ya vipengele vyake fulani kama vile roho na VIGANJA?[Kwani wewe ulifikiria mie MTAKATIFU ntapenda kipengele gani zaidi ya viganja? LIONE VILE!]

Hebu Mr Blue abadili hali ya hewa tena kwa kuongelea- MAPOZI


Au tu MANU CHAO aongelee tena- Me gustas tu

Read more...

WAKATI unaendelea KUJAZIA SIKU shughuli!

Ndani ya siku,...

.... ufanyayo ya muhimu ukifikiria sana ni machache na YANAHESABIKA!

Na uchache wa ya YA MUHIMU kwa siku,...
.... mengineyo siku ikiendelea ingawa uliyaanza vizuri labda nayo YAMESHAHARIBIKA!


Lakini hatuwezi kusikitikia tu ya siku,....
... ya mwezi na mwaka yanamkusanyiko wake wa usaha au asali hata kama kwa yaliyonyoka baada ya muda mrefu kuna siku yalikuwa YAMEPINDIKA.

Na labda uko kwenye zako siku,...
....lakini kumbuka kwa wenye mahitaji ya leo hata kama utachelewesha nanihii UTASAMEHEWA SIKU UKITIBU lakini kumbuka bado leo UNAHITAJIKA!:-(


Na shughuli ni nyingi ndani ya siku,...
... lakini bado ukweli ni uleule kuwa labda vya leo ulivyofanya katika yote cha muhimu ulichofanikisha ni KULA, KUNYA na kama ni mlalamishi angalau umefikiria cha muhimu kama hata sio HIKI NIANDIKACHO basi KINGINE katika YOTE ya katika kuchambua NI nini ukilenge hata baadaye wakati UKILALAMIKA!


DUH!
Naacha na NI WAZO TU kumbuka MHESHIMIWA !

JuMApili njEMA KInguNGE!

Swali:
  • Hivi ushawahi kufikiria kuwa labda udhaniacho ni cha muhimu labda ndio sio cha MUHIMU?
  • Unafikiri kuna BINADAMU ALIYEWEZA kujaza SIKU?

Ngojea tumtembelee dada Speech DEBELLE atutonye ya-The KEY


AU tu KRS1 aongelee tena ya URAFIKI katika kitu-A FRIEND


AU tu Lil Wayne adharaulishe watu katika- Lollipop

Read more...

WAKATI UNACHUNGULIWA!

>> Saturday, August 15, 2009

Kumbuka,...
... kama unachakuonyesha ,...
na unauhakika na upendavyo kilivyonuna unaweza mpaka ukakibenjua makusudi katika staili ya kukionyesha kama unajua UNACHUNGULIWA!

Kumbuka,...
...NDIO!Labda kuna kitu hutaki kukionyesha,...
...lakini moja ya sababu ya kutotaka kuonyesha ni jinsi utafsirivyo tu MUKICHWA maana yake nini ukituonyesha KITU CHAKO ambacho labda ni KIZURI KULIKO CHETU ndio isababishayo ukasirike au kuona aibu ukistukia UMECHUNGULIWA!


Kumbuka,...
... ukipewa sababu za kuonyesha,...
...kuna kitu utatubenjulia tukiangalie vizuri wakati kabla ya kupewa sentensi kadhaa ungeona aibu wakati unakikagua ukastukia UMECHUNGULIWA!


Kumbuka,...
...vingi ufikiriavyo unavionyesha,...
....kumbuka wengi watazamao hata bila kuchungulia huwa hawavioni na hata kama nia ni kuonyesha CHUCHU kuna uwezekano hata TITI halistukiwi INGAWA KIFUA KIKO WAZI wakati huo na hapa siongelei wakati UNACHUNGULIWA!:-(


Swali:

  • Unafikiri hata barabarani ni mangapi yaliyo wazi huwa unayastukia na kuyaona?

  • Unajua ni kweli asilimia kubwa ya wachunguliao hawaoni kitu na wakiona hawajakiona vizuri kidude?

  • Unajua wengi hata unao ongea nao uso kwa uso huwa hawakuangalii?


NI wazo tu na UNARUHUSIWA KUNIBISHIA KINGUNGE!

Hebu tupumzike kwa kwenda CANADA kumuangalia BINTI mheshimiwa wa KiMAREKANI kwa jina AMY G aonyeshe kipaji katika-The special and sexy talent of Amy G(TAHADHARI: Usiangalie kama mtoto au ni MZEE WA KUKWAZIKA kwa kuwa ni ujinga afanyacho kwa tafsiri fulani)



AU tu PAM HALL alete ustaarabu tena katika kitu-Late at NIGHT



Au tu MIRIAM MAKEBA alete kitu kiitwacho-POLE MZEE



Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP