Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Hivi NA HAMU kweli ya MWANAMKE au NA HAMU tu ya CHAKE kipengele hata kama sio UKE?

>> Sunday, August 16, 2009

Labda KATIKA hamu,...

..mara nyingi LABDA ukiwa na hamu ya MAGIMBI kunauwezekano huo ni msimu wa VIAZI!:-(


Na KATIKA hamu,...
....unaweza kula MAGIMBI kwa kuwa ni kweli unayapenda MAGIMBI , lakini LABDA ni ugali wa MHOGO unaoumisi mpaka KATIKA NDOTO na katika shughuli NI kweli ni UJI WA ULEZI UMEPEWA ambao NA bado upo INGAWA ni KWELI kuwa katika MAISHA YAKO na si katika NDOTO ZAKO huwa hupendi UJI achilia mbali UJI WA ULEZI, na kwa HILO hata usipotuuliza bado SISI twaweza JUA NINI KINAENDELEA na ukweli ni kwamba katika nyege zako za ugali wa sembe ukipata uji wa ulezi BASI katika hilo HIYO kama ni ndoto yako BASI hiyo ndoto ni JINAMIZI!:-(


Na KATIKA hamu,...
... hamu nyingine ni MATUSI ukizizungumzia INGAWA ukionja hata kiitwacho MATUSI unaweza kuguna kwa kunogewa na wakati umenogewa ukijaribu kuongea nasi hata kwa simu wakati unaendelea KUNOGEWA , .....SISI wengine tunaweza kudhani siku hizi WEWE una KIGUGUMIZI.:-(

DUH!
Mie Mtakatifu Simon KITURURU naachia hapa wazo na UKIENDELEZA WAZO SHAURI YAKO mie sikushiki KIBINDO!:-(



Swali:
  • Hivi ukiwa na HAMU YA MWANAMKE au MWANAMME huwa unafikiri unahamu yake MTU WOTE au unakuwa na hamu ya CHAKE tu KIPENGELE?

  • Hivi wewe kama MTU unauhakika kuwa MTU MWENYE HAMU YA MTU akimpata mtu anaukumbuka bado mwili wake wote na sio kama MIE MTAKATIFU SIMON KITURURU huwa anakumbuka baadhi ya vipengele vyake fulani kama vile roho na VIGANJA?[Kwani wewe ulifikiria mie MTAKATIFU ntapenda kipengele gani zaidi ya viganja? LIONE VILE!]

Hebu Mr Blue abadili hali ya hewa tena kwa kuongelea- MAPOZI


Au tu MANU CHAO aongelee tena- Me gustas tu

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:31 am  

Me gustas tu:-(

Mzee wa Changamoto 12:28 pm  

Duh!! Labda nina hamu ya kusoma ili kujua baadhi ya niliyoyasoma na sio uliyotaka niyasome na kuyaelewa. Ama ninapoingia MAWAZONI nawaza kile nilichowazishwa na mazingira lakini si kile ambacho nilistahili kuwaza. Hivi unapotamani kusoma blog, una hamu ya maandishi au ni ile ya mwandishi hata kama hayakufai yake maandishi? Basi tutaanza kuweka picha za kwenye makasha ya sabuni ili kuvutia uandishi.
Naacha hili wazo, kwani naona naanza ku-create tatizo kwa namna nilionavyo TATIZO

Christian Bwaya 8:43 pm  

Mzee wa Changamoto, kwa nini unadhani huenda unasoma baadhi ya yaliyoandikwa? Unajuaje kuwa unachotaka sicho usichotaka? Je, nini mipaka ya mazingira?

Simon Kitururu 3:08 am  

@ WOTE: DUH!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP