Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa MPENZI SERIKALI Vinduna a.k.a SERIKALI YA WAJANJA!

>> Sunday, August 23, 2009

Vinduna MPENZI wangu,....

.... wataka niua MOYO?


Kama WEWE ni wangu,....
....kwangu usiwe mchoyo

Tunza KIHARAGE changu,...
... usiniumize MOYO.

Nikiogopa na changu,...
....ni shinikizo la moyo.

Wengine usionjeshe, kwanza hudumia YANGU.



Wasahau ya WADOGO,...
... katika mwili husika.
Huridhisha ya VIGOGO,...
....yale yote wanataka.
Kujazia ya KIGOGO,...
.....kwa PANYA waweka PAKA.

Nyumba yetu ilo NDOGO,...
... wataka ijae TAKA?
Vinduna mpenzi WAMO, kilicho kidogo TUMO?


Lione tu kubwa hivyo,...
...mpenzi mwendo KA bata.
Nikikasirika hivyo,....
... na hamu LIKATAKATA.

Naongea hata hovyo,...
...ya uchungu penzi TATA.

Ningenogewa vilivyo,...
... wafikiri ninge BWATA?
Tako kubwa lina kubwa, na wadogo hatupati?


VINDUNA kipenzi changu,...
...mwenzio MI nina HAMU.
Ya kukiri we ni wangu,...
... na umeshika HATAMU.

Kutetea hamu yangu,...
...lete tibabu la HAMU.

Ondoa naya KIWINGU,....
... kwenye yale ya MUHIMU.

Sasa kama WE mpenzi, basi lete hilo penzi!


DUH!

Nakatizia wazo hapa!

Swali:
  • Hivi unaipenda au unaiogopa serikali yako ya KIBONGO NYOSO?
  • Hivi kama wewe si mfanyakazi wa serikali yako ya BONGO NYOSO unaamini serikali ni ya watu wake na SERIKALI YA NCHI YAKO ni yako?

NIMEACHA!

Ngojea COMMON asibadili kwa kitu-A letter to the LAW




Au tu Eddy Grant arudie kitu-Living on the frontline

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 10:31 am  

Haya Mtakatifu Simon:-(

Simon Kitururu 2:28 pm  

@Yasinta: DUH!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP