Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati siri ya kwanini hufanyi ni kuogopa tutastukia ukikosea au KUCHEMKA!

>> Thursday, August 20, 2009

LAKINI!.......


Wakati husemI,....
.... afadhali.....

..... iwe HUSEMI tu kwa kuwa katika tafsiri yako, kukaa kimya ni BUSARA na sio hofu ya ukisema utachemka na TUTAKUCHEKA!


Wakati hufanyI,...
....afadhali ....
....iwe ni kwa kuamua hufanyi kwa kuwa ukweli ni kwamba binadamu hakosi CHAKUFANYA kwa kuwa kwa yeyote mwenye ubongo vya kufanya VINABUNIKA na usipojazia muda na chakufanya unaweza UKACHEMKA kwa kutumia muda wako kusubiri siye WENGINE tukosee na kwa kufikiria ni ujanja eti utafurahia ukidhania tumekosea KUTUCHEKA!:-(




Na kama wakati KIKIFANYIKA huangaliI,.....
....afadhali....
....uwe mwangalifu na uwachekeao au kuwashabikia wanaoshabikiwa usiojua walifanikiwaje.
Kwa kuwa kunauwezekano majibu ya matatizo yako au tu maswali yako LABDA yanajibiwa zaidi na wajulikanao kushindwa na labda HUJIBIKA PIA kirahisi ukishuhudia wanavyoshindwa ingawa umuhimu wao na yao waliyoshindwa jamiii inaruka na JAMII pamoja na wewe kirahisi tu mnaweza mkawa KWENU ni kawaida KUWACHEKA!:-(


Ni hilo tu na ni WAZO tu KIBONGE!


Hebu basi OSIBISA wanisaidie tena kulainisha swala kwa kitu-CHECHE KULE



Au tu tena OSIBISA waifanye iwe siriasi katika kitu -Why

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 10:29 pm  

Kazi kwelikweli:-(

Simon Kitururu 9:33 pm  

@Yasinta: Si utani!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP