Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

BAADA ya KUKOSEA!

>> Thursday, August 13, 2009

Kuomba msamaha ni KAWAIDA,...
... lakini haifuti kuwa kwanza ULIKOSEA.

Na uwaombao msamaha hata kama wanafikiri wanastahili na ni KAWAIDA,...
....labda wao ndio WALIOCHANGIA kusababisha ukosee au ufikirie UMEKOSEA.


Ingawa kuna wadaio ukikosea kusingizia wengine ni KAWAIDA,...
....labda SI KAWAIDA chaguo lako LA ni nani WAKUMLAUMU au eti tu kachangia kachumbari katika UBWABWA wa lililo kufanya kama sio juzi au jana ,BASI labda leo lililokufanya UMEKOSEA.


Na kabla hujaomba msamaha si lazima hujastukia kosa na labda ni KAWAIDA,...
.... lakini uwaombao msamaha labda wakati huo huo nao ndio kwanza wanaendelea KUKOSEA!:-(

DUH!

Swali:
  • Hivi WAKATI unaombwa msamaha HUWA unajisikia vizuri eeh hata wakati kwa sauti unakiri hutaki kusamehe aliyekukosea ?

  • Unauhakika hukosei kwa kuomba MTU msamaha?

Samahani ni wazo tu MKUU WA MASWALA na NIMEACHA!:-(

Ngojea Dr Alban abadili hali ya hewa kwa kuzungumzia kitu -Born in Afrika



Au tu Dr Victor aturudishe afrika kikweli katika kitu - Kalimba

9 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 9:59 pm  

karibu tena kwani ulipotea sana lakini kwa kawaida watu huwa wanaiga wapoondoka:-(

Yasinta Ngonyani 9:59 pm  
This comment has been removed by the author.
Fadhy Mtanga 10:49 pm  

"This post has been removed by author"
aombe msamaha maana inaonesha alikosea anapoandika.

Mkuu, ukikosea huwa unajishtukia ama unashtukiwa?

Simon Kitururu 4:41 am  

@Dada Yasinta : Kweli kabisa usemacho:-(

@Papaa Fadhy:
Huwa najitahidi kujistukia NA NILIFIKIRI KUWA HUWA NAJISHTUKIA lakini imetokea kuwa huwa nashtukiwa zaidi hata ambayo nafikiri ni kawaida lakini eti NAAMBIWA nimezidisha na eti si kawaida:-(

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 12:28 pm  

the way u see the problem is the probem. there fore no mistake but you mistake yourself

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 12:28 pm  

the way u see the problem is the probem. there fore no mistake but you mistake yourself

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 12:28 pm  

the way u see the problem is the probem. there fore no mistake but you mistake yourself

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 12:28 pm  

the way u see the problem is the probem. there fore no mistake but you mistake yourself

chib 8:18 pm  

Kamala unajaza nafasi ya comment bwana. Au ndio siku ya kukosea. Ukiomba kamsamaha nawe nafikiri Kitururu atachekelea :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP