Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Hadithi hii NIMESIMULIWA na MTOTO![stori ya kweli!]

>> Thursday, August 20, 2009

Hadithi hadithi!


Hapo zamani za kale kulikuwa na SUNGURA!

Asubuhi moja Sungura aliamka na njaa akaamua kwenda kutafuta uyoga ale.

Basi akaenda weeeee AKAENDA weeeeeeeee AKAENDA weeeeee halafu akakata kona.

AKakata kona halafu akaenda weeeeeee AKAENDA weeeeeeeee mpaka msituni.

Hapo msituni akakutana na FISI, fisi akataka kumla Sungura.

Sungura akagundua hawezi kupigana na FISI kwahiyo akaamua kukimbia.

Akakimbia weeeeeeeeeee AKAKIMBIA weeeeeeeeeeeee AKAKIMBIA weeee mpaka akakuta shimo ambalo akaingia kujificha kusubiri Fisi akate tamaa aende zake .


Basi akajificha weeeeeeee Akajificha weeeeeeeeee Akajificha weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!

Ingawa aliumwa njaa shimoni akasubiri weeee akasubiri wee mpaka Fisi akaondoka kwa vile alijua akiumwa njaa si lazima atakufa lakini akipambana na Fisi atakufa.

Anko Simon Mwisho wa HADITHI!
------------------------------------_______________-------------------

Mazungumzo yetu baada ya Hadithi!

Mie Mtakatifu Simon: Hadithi nzuri sana!
Mtoto: Anko unajua hii hadithi inatufundisha nini?

Mie Mtakatifu Simon: Niambie basi Anko inatufundisha nini?
Mtoto: Inatufundisha kuwa akitokea mtoto mtukutu anayekuzidi nguvu au kitu cha hatari kimbia si lazima upigane nacho halafu ukiumwa na njaa vumilia kumbuka sio lazima utakufa!

Mie Mtakatifu Simon kwa mara nyingine nikawa nimekatwa kauli na kwa sababu fulani mpaka sasa hivi hiii stori niliyosimuliwa na mtoto wa miaka sita INANIFIKIRISHA!



Basi ngojea tubadili hali ya hewa kwa kwenda NEW ZEALAND kuangalia tena hii kesi ya jamaa kula MBWA katika kitu -Man COoks a family Dog



AU tu turudi KAMERUNI kwa Manu Dibango aseme tena ya-Woa

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 10:28 pm  

Hadithi hadith kuna sehemu moja kulikuwa na vyumba saba katika hivyo saba sita viliruhusiwa kufungua ila kimoja kisifungulie lakini kuna siku binti mmoja alifungua na alipofungua alikuta chumba chote kimejaa nyoka. Alipotaka kufunga nyoka akamwambia usifunge ingia. Tangu siku ile yule binti akawa mke wa nyoka....mmmhhh ngoja niache isije watu wakaogopa!!!!!

Simon Kitururu 4:29 am  

@dada Mpenzi::-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP