Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KATIKA staili ya kuvutiwa na mtu KWA SABABU TU TAYARI unajua yeye ni NANI!

>> Saturday, August 22, 2009

Unaweza kubisha LAKINI kuna watu unawasikiliza kwa kuwa unajua TU wao ni akina NANI!

Kuna USOMAO mpaka waandikayo kwa kuwa tu unadhani unajua wao ni akina NANI.

Labda pia kuna mpaka UWATAMANIO na kudhani ni wazuri KUBWA KULIKO kwa kuwa unajua tu wao ni akina NANI.


Na mpaka katika ya UJINGA WAO hao akina nani, utawatafutia sababu za nini ni busara ZA WAFANYAYO na kwa nini umati hauelewi yao wasemayo , waandikayo au tu yaliyo kwenye picha zao hata za uchi KWA KUWA TU unadhani unajua wao ni AKINA NANI.


Na LABDA usingejua ni akina nani WAO,...
.... yao ni UPUMBAVU na wala hayapandishi mdaDI.

Na kuhusu huo mwanya WAO,...
... kwako ungekuwa ni MAPENGO au UKIBOGOYO na wala haupandishi mdaDI.:-(

Hata ule mwendo wa maringo wa kudunda WAO,...
...wewe ungehakikishia watu kuwa ni kuchechemea kwa sababu mguu wao mmoja mfupi na wala si mwendo maridaDI.

Na wangecheka hata kuhusu yao WAO,...
...ungekunja uso kwa kufikiri wanakuchekea WEWE na ungedhani unatakwa au kwako wanajipendekeza kwa kuwa unadhani wewe BABU KUBWA na maridaDI.




DUH!

Swali:
  • Unadhani hakuna angalau hata BLOGU uzitembeleazo hata za kipuuzi kama HII YANGU si kwa liandikwalo au picha za uchi ila ni kwa kuwa unajua mwenye blogu ni nani?

  • Unadhani hakuna watu unawaheshimu au kuwadharau kwa kuwa unadhani unajua wao ni AKINA nani?

  • CHA KUSIKITISHA NI KWAMBA ,si kuna watu hata huwasikilizi hekima na busara zao kwa kuwa tu hujui wao ni AKINA nani?
Samahani NALIKATIZIA WAZO HAPA Mheshimiwa, Msela au tu wewe Kiruka njia!

Jumamosi njema MKUU wa MASWALA!


Hebu basi tubadili hali ya hewa kwa kujifunza tena jinsi wanawake wabadilishavyo nguo katika-NANIHIII


Au tu twende South Africa kukutana tena na Soul Brothers walete kitu -Usemncane


Au tu turudi tu tena Tanzania MATONYA aongelee tena ya -TAXI BUBU

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 4:30 am  

Umejuwaje mkuu?
Kama ambavyo mimi huwa naitembelea blog hii pasipo kujali pameandikwa nini kwa sababu tu ni ya mtakatifu Simon. We huwa huoni hata Sista Yasinta anavyopenda kuitembelea blog hii kwa sababu tu ni ya mtakatifu Simon a.k.a Simion wa kwanza.

Kuhusu kutamani, hata mi mdadi unamdondokeaga binti maringo fulani kwa sababu tu ni yeye.

Kuwa na Jumapili mdokonyole.

Mzee wa Changamoto 4:47 am  

Duh!! Ujumbe delivered kwishnen!!
Ila umetusema wengiiiiiii!!!

Yasinta Ngonyani 1:12 pm  

Simon:-(, :-(

Simon Kitururu 7:33 pm  

@Wote: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP