Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Uhusiano wa WAHESHIMIWA na USIVYOVIHESHIMU!

>> Friday, August 28, 2009

Mara nyingi BINADAMU huheshimu mtu bila sababu MAALUMU.


Na BINADAMU anaweza akajikuta mpaka anaongozwa na AWAHESHIMUO bila kuchunguza wampelekapo WAHESHIMIWA ambao labda sio waheshimiwa kwa kuwa hawastahili HESHIMA.

Hili ndilo sababu kubwa isababishayo MTU kujikuta anaongozwa hata katika yale ambayo angetakiwa AONGOZE!

Na heshima labda ni kitu tokea UZALIWE huwa UNAKUWA na hamu nacho kitu ambacho kinaweza kukuponza ukajikuta wasio stahili heshima ndio wana chati katika HESHIMA YAKO kwa kuwa ndio wenye KAULI na MAPOZI uyazimiayo au jamii iliyokufunza kujali na kwa hilo WAMESHAKUTONGOZA na kwa hilo unasifiwa UNAHESHIMA.

Swali:

  • Unauhakika hufuati viongozi wakuongozao wakati labda huna sababu maalumu zikufanyazo uamini HAO wanajua waendako wakati WANAKUONGOZA?

NI WAZO TU MHESHIMIWA!


Twende kidogo ZAMBIA tukutane na Kachanana alete za -Mbululuka

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP