Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Sababu za hamu ya mtu KUMCHUNGULIA mtu!

>> Saturday, August 29, 2009

Kunakitu unataka jua,....
Wadhani utafananisha ukijua,....

au wataka ujue ili ufananishe na usicho na uhakika unajua,...
Lakini labda hata KUKU umeshawachungulia FARAGHA bila kujua,...
....ndio maana bata wakiwa katika shughuli za FARAGHA huhitaji kupiga chabo mara mbili kwa kuwa wafanyacho TAYARI unajua.


Tatizo ni kwamba binadamu wote kuna kitu hujifanya wanajua,..
....ingawa wote hufa wakati kuna kitu hawajui ingawa labda ya mbinguni ni moja wapo ya waliotaka kujua.:-(

Na chakuchekesha kuna akuchekaye kwa kutokujua KWAKO hili wakati KIRAHISI ATATAKA KUKUCHUNGULIA kwa kuwa kisiri tayari kwa UBINADAMU ANAJUA kuna kibao kumzidi unajua.

Kwahiyo naweza kusema hamu ya KUCHUNGULIA ni moja ya jinsi ya KUKIRI HUJUI au huna UHAKIKA kama ni kweli UNAJUA.

Kumbuka tu pamoja na wengi kusifia wanao jua , KUNA MAMBO WENYE AFADHALI ni WASIOJUA.


Lakini:

  • Unauhakika unajua?
  • Na unauhakika wajifanyao wajuzi ni kweli WANAJUA?
  • UNafikiri usingejua kuna sukari na chumvi usingenogewa tu na AISHIKIRIMU YA UKWAJU isiyo na sukari au tu MLENDA usio na chumvi?


NI HILO TU na ni wazo tu MHESHIMIWA!


Au tumtembelee tena mwanadada aongelee YA MBWA anayojua chini ya kichwa cha habari[Tahadhari: Usiangalie kama mtoto au ni Mkuu wa kukwazika au tu unakwazika kirahisi!:-(] -Bestiality Woman



Ngojea tusikilize tena maswali aulizwayo mchungaji na watoto kuhusu NABII ISSA au tu kama kwa wengine ajulikanavyo kama YESU katika-Awkward Questions about Jesus

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Faith S Hilary 2:23 am  

Hii post inakufanya unajiuliza maswali mengi bila kupata jibu au unapata multiple answers then you don't know which one is relevant lol.

And the kids! Oh My God they made me laugh so hard!!! Hahahahhaha...wangepata mchungaji kutoka Tz or something...lol

Simon Kitururu 3:35 am  

@Candy1: :-)

Yasinta Ngonyani 9:42 pm  

Simon, Kazi kwelikweli. DUH!

Anonymous 9:42 am  

mpaka unatamani uwajibu vibaya.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP