Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KITU KIBAYA hata kama bado HAKIJAJIHARISHIA kinawafuatiliaji MIA wakati kitu kizuri KINA WAFUATILIAJI kumi!:-(

>> Thursday, August 06, 2009

Uwiano wa mvuto wa KIBAYA na KIZURI ukipima ni BALAA mpaka utafikiri kipimo kinakasoro na si KAWAIDA!

Na labda umeshajitahidi sana MHESHIMIWA MTU kwa wema na eti HATUJASTUKIA, na chaajabu ETI hiyo ni KAWAIDA!:-(


Unaweza KUBISHA!

Lakini kuna sababu kwanini hata MAREDIONI , mtandaoni au hata KWENYE TV kila iitwayo TAARIFA YA HABARI hujaa zaidi HABARI MBAYA mpaka inasemekana habari mbaya ndio HABARI na ukifikiria utastukia hiyo haitakiwi iwe ndio KAWAIDA.:-(


NA unaweza KUBISHA!

Maisha ya binadamu yamejaa MAMBO MAZURI mengi mpaka watu wengi PAMOJA NA kuwepo MABAYA wameyazoea MAZURI na NAYO yamekuwa ni KAWAIDA!:-(

Unaweza KUBISHA!

Ni pale watu WENGI wastukiapo jambo ambalo limezidi ubaya ndio wanaingia nyege ya UDADISI WA MTU WALIYETAFSIRI chake KIBAYA wakutaka kujua zaidi hata kama ni swala la kuwa eti leo MHESHIMIWA MTU twasikia kajinyea NA ETI ndio UDADISI WA MHESHIMIWA MTU utazidi NA utasikia ,''Nilikuwa nahisi kuna kakitu tu kila nimuonapo MHESHIMIWA MTU huyu'' . Na hata ukibisha , inasemekana hiyo ndio KAWAIDA!:-(


Na SIBISHI!

Kuna mambo pia mazuri KUBWA KULIKO ambayo yanamdaka aliyezoea MAZURI na kuyaona KAWAIDA na ukweli hayo mazuri kubwa kuliko labda ni kubwa kuliko kisaikolojia tu na MDHANIO na UKWELI ni ya KAWAIDA!:-(


NA HATA UKIBISHA!

Si kweli ni HAKIKA kila uwaonao ufikiriao wanacho KIKUNOGEACHO maana yake wananogewa nacho au WANANOGEWA ZAIDI mnogo. Na hiyo ndio KAWAIDA.:-(

Na tena UNAWEZA KUBISHA!

Hata ukimuuliza rafiki yake shetani au mdau wa Mungu labda atakujibu, kati ya KITU KIBAYA na KITU KIZURI ukistukiacho na kukifikiria kirahisi kama si KUKING'ANG'ANIA, utasikia ni kitu kibaya kikutesacho hata utake KUONGEZEWA MSHAHARA wakati pesa ya magimbi inatosha na wala hupendi UYOGA, na LABDA hiyo ni KAWAIDA!:-(




Swali:

  • AU?
  • Hujawahi kusikia dini fulani zinakiri mpaka MUNGU WAO kakiri atafanikiwa kuwadaka wachache wema wasionogewa na KIBAYA atakaowatranspoti kwenda mbinguni na KWA njia nyembamba halafu wengine wote wanao leta za kuleta mpaka MABAYA mengi wayastukia KINOMA na kuyashikilia mpaka kiuno KWA KUNOGEWA ndio shetani atawachukua katika bomba la haiwei?

  • Hivi wewe MHESHIMIWA huwa unastukia zaidi ukifanyiwa wema au ubaya?
NIMEACHA na ni WAZO TU KIBOSILE usitishike na wala hulazimiki KUNIELEWA!:-(

Hebu tubadili hali ya hewa kwa kwenda IVORY COAST tukutane na Joelle C alete tena kitu- Man Dinka



Au tupitie tu tena Trinidad tukutane na RIKKI JAI katika miondoko ya Soca Chutney alete kitu - The last Band

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mzee wa Changamoto 1:09 am  

Duh!! Ama kweli hili WAZO KIBONGE. Kama unabisha basi angalia picha za watu waliokaa robotatu uchi kwa mdau naniii zinavyopata maoni MWANANA kuliko za MSAMARIA anayejitolea kusaidia watoto wenye uhitaji.
Ama wanavyozungumzia Michael J kwa madawa kuliko rekodi yake ya kuwa mtoaji mkubwa wa Charities duniani na hata mpango wake wa ku-adopt watoto 2 kutoka kila bara.
Ama uone watakavyoshabikia kusikia Mubelwa kapatwa baya kuliko harakati za ujiinua.
Asante kwa wazo nono na kibonge.

Fadhy Mtanga 7:36 am  

Ahsante mkuu Mubelwa kwa maoni kingunge.
Kumbe nawe umeshtukia?

Simon Kitururu 4:33 pm  

@Papaa Fadhy Na Mkuu Mubelwa: Asanteni wote!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP