Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MAISHA ya kabla ya KIMOBITEL a.k.a SIMU!

>> Friday, August 07, 2009

Ilikuwa KIJIJINI ukimtaka ZUBEDA,...

....HUHITAJI SIMU,.....
....wajua saa za jioni na ndoo hakosekani KisimaNI.


Na giza likiingia akikukubalia zako za kauli JITIHADA,...
...HUKUMBUKI DUNIANI KUNA SIMU,...
... na vile vile wajua hakuna gesti na mambo MPWITO ni VIchakaNI.

Na hata kama uko mjini na nia ni kukutana na KADODA,..
...HUKUHITAJI SIMU,...
...ulijua kama si KONTENA au KIOSKI, kilinge cha kwa fundi viatu HAkosekaNI.

Na yule ANNA totoz la kilokole lisokosa IBADA,...
...YA NINI SIMU,...
... wakati wajua waweza MPAKA liimbia kwaya KA nisaNI?:-(
Na yule MSONGO wa kitabu AHMADA,...
... YA NINI SIMU?...
...ulijua kama sio saa tisa ni saa kumi YU maktaba na sio kwenye mpira KIwanjaNI.

Na kama ni kwa mgonga kokoto Simoni wa MIDABWADA,....
...HUKUHITAJI SIMU....
.... ulijua midamida ukitaka utamkuta akishughulikia mawe huku akitoka jasho MtoNI.

Eti siku hizi kama huna SIMU hata ya kutongozea MWANADADA,...
.. WAWEZA JISIKIA WAHITAJI SIMU...

... la SIVYO wawezashindwa wasiliana na NDUGU na JAMAA achilia mbali kukosa WINDO bila kutumia akili MUKICHWA hata WIndoNI, sokoni na nimatumaini yangu angalau isije kuwa ni hadi NYUmbaNI.:-(




NIMEACHA WAZO MKUU na kama hujastukia , namisi enzi zile ambazo mie Mtakatifu Simon sikuhitaji Simu hata ya Ku-beep a.k.a KUMDIPU kishtobe nibane kwa kucha aninong'oneze nijisikie raha MOYONI !:-(
Swali:

  • Umestukia siku hizi kuna watu wanadai hawawezi kuishi bila SIMU?
  • Hivi nani ka kwambia ili kuishi MTU huhitaji simu?LIONE VILE!:-(
KUMBUKA hili ni WAZO tu MHESHIMIWA na nakutakia mafanikio IJUMAA na WIKIENDI HII chooni!

Hebu WANDA SYKES abadilishe hali ya hewa a.k.a atukane katika- SICK and TIRED[Tahadhari :usimsikilize kama mtoto au wewe ni MHESHIMIWA wa KUKWAZIKA kwa sababu kwa mtazamo fulani ni matusi!:-(]


Au twende tena Ivory Coast tukutane tena na MAGIC SYSTEM waongelee -Premier GAUO.


Au tu 113 na MAGIC SYSTEM walete- Un gaou oran

8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 6:39 pm  

Longi wakati hakuna simu, hata mapenzi yalikuwa matamu, mapenzi ya kuvizia.
Siku hizi mtu mzima unawekwa kwenye waiting list na hujishtukii, appointments zapangwa kwa simu.
Na watu hawawezi ishi bila simu.

Faith S Hilary 6:44 pm  

Technology changed, changes and will change out lives as we continue living.

LOL I absolutely love Wanda! She is so funny. Eti "detachable p****y" lol!

Na huo wimbo wa "Gauo" lazima ucheze even if you are in a bad mood lol! Nice one Simon...

Yasinta Ngonyani 6:44 pm  

Duh! Mambo yaenyewe ndo kama hivi kazi kwelikweli!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 12:05 pm  

umesema yoote niliyoyapitia mzee

Simon Kitururu 9:23 am  

@Papaa Fadhy!: :-)

@CANDY1: : :-)


@Dada Yasinta: :-)

@Mkuu Kamala: Hivi nimesema yote?:-(

Mzee wa Changamoto 11:41 pm  

Labda huwa hatuna mahitaji. Bali twayatengeneza ili wahitaji wahitajike kuhitaji tuhitajilo. Yaani kabla maisha yalisonga kiaina lakini sasa hivi ndio kama usemavyo. Eti sasa hivi wengi hawawezi kukumbuka Birthsay za ndugu zao kwa kuwa tu wana Digital Reminder. Eti hawawezi kukariri "makona" yooote kwa kuwa wana GPS. Na kwa sasa hawawezi kukaa siku nzima bila ku-text MUPENZI maana hiyo inawafanya wajihisi WAMEPUNGUKIWA kitu. Hivi hizi simu zilikuja kwa kuwa tulikuwa na uhitaji ama uhitaji ulikuja kwa kuwa kulikuwa na ulaji?
Nimeacha wazo mkuu

EDWIN NDAKI (EDO) 4:18 pm  

tupo pamoja mzee Duh! ndio maana hatuwasiliani siku hizi nimeamua kuacha kutumia simu ..lol

Simon Kitururu 11:14 pm  

@Mkuu Mubelwa na Papa Ndaki: DUH!:-) Tuko pamoja wazee wa shughuli!!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP