Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama wewe ni MTANZANIA na hustukii NYERERE, Mkapa, KIKWETE bila kumsahau Mtukufu mwingine kwa jina Rais Ali Hassan Mwinyi kuwa ni SARE SARE MAUA!:-(

>> Thursday, August 20, 2009

Ngojea niseme kihivi....


Labda Rais Nyerere alieliMISHA,...
.... na ulipoaanza kujifanya mjuaji akakukata ULIMI!

Labda Rais Mwinyi akaruhusu ikawa RUKSA ingawa katika swala la kujiRUSHA,...
.... ukastukia viko dukani NA kuvikodolea MACHO ruksa lakini wawezao kuvinunua VIWARUSHE hawakuwa wewe wala MIMI.:-(


Na labda Rais Mtukufu Mkapa kama ulijaribu chake KIBIRITI kutiNGISHA,...
....alijitahidi kukusaidia kukuelimisha ujue nguvu ya DOLA au tu serikali NI NINI ingawa wakati huohuo pia UKIENDELEA kushuhudia jamii ikiendelea kufunzwa UPROFESA wa ya KIBINAFSI na sio tena YA KIJAMII KWA UJUMLA na hapa ni katika tu kujaribu kutoliita swala zima UMIMI!:-(



Na labda Rais KIKWETE yupo na unaruhusiwa fikra zake kuduMISHA,...
....ingawa kumbuka wakati unamlaumu kwa kutofanikisha isije ikawa wewe mwenyewe unaongea zaidi kuliko kutenda ukasababisha naye Rais Kikwete ukimbana kona akakuzidi hoja kwa kukuambia ulitegemea msosi AKUWEKEE kinywani na akakusuta ''Koma babu wewe mengine usinilalamikie MIMI!'':-(

Na kumbuka Rais ingawa huwa TUKIONGELEA YA RAIS huwa tunamuongelea MMOJA mtu, RAIS ni OFISI ingawa tukiichukulia kuwa kama gari , ajulikanaye ni RAIS ndio anaeNDESHA,....

..... ingawa kama gari ni bovu Rais AMBAYE NI DEREVA mwenye MENO akikuchekea WAWEZA KUONA tu MAPENGO na kwa hilo unaweza usistukie TU la maana afanyalo kama tu USIVYOSTUKIA MCHANGO WA MAENDELEO YA NCHI wa yule mwenzangu na MIMI!:-(

Na ya ZANZIBAR ya RAIS kama ni pombe basi HIYO POMBE yaleWESHA,...
... na katika YA ZANZIBAR mara nyingi hata ADAIYE ajua tofauti ya Rais Karume, Salmin , Karume na ... na kutaka tuamini majibu yake na pamoja na MASWAHUBU , mie kwa hilo sina MAJIBU ukiniuliza MIMI!:-(


NIMEACHA!
Na, kumbuka MIE NAWAZA tu hapa KIBONGE au tu wewe ZEE la FACTS!

Swali:
  • Hivi unauhakika Rais HUWA anafanya nini ofisini?
  • Unafikiri Ofisi ya Rais ikiwa vile vile nini kinabadilika hata ukibadili aitwaye RAIS?
  • Hivi unajua hata kazi ya Balozi wa Nyumba kumikumi ni nini hata kama akitokea unamchunga hausigeli wako?

DUH!

Ngojea twende NIGERIA kidogo tukakague hali ya UKIMWI tena katika ...-HIV couples WEDS



Au tubakie tu hapa hapa Nigeria LAGBAJA alainishe tena kwa kitu- Nothing for U





Au tu LAGBAJA alete tena kitu-Feyine




AU tu nimuache tena katika kitu LAGBAJA live

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 10:30 pm  

Mmmmhh sina la kusema ila tu tupo pamoja na tutafika tu.

Anonymous 3:50 am  

Maoni yetu unayabana, lakini ya Yasinta, ewaaaa. Haya tu wewe Simon!!!!

Lakini sisi ndo wenzako katika mengi. Shauri yako wewe haya tu!!!

This Is Black=Blackmannen

Simon Kitururu 4:21 am  

@Yasinta: Haya bwana!
@Mkuu Black a.k.a Papaa Blackmannen: Mbona mie hapa kwenye hii blogu sijawahi kuzuia comments tokea nianzishe blogu hii?

Inawezekana kulikuwa na tatizo tu kidogo katika internet kwa kuwa nilivyo seti blogu hii ni ki RAis Mwinyi a.k.a Kukomenti Ruksa!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP