Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UKIPATIA!

>> Saturday, August 15, 2009

Ukipatia,...
...kwa kawaida TUTASIFIA!

Na labda wakati tunafikiri umepatia,...
... unaumaumivu kwa tuchukuliacho ni ushindi na ni kwa sababu tunakusifia ndio maana na wewe unaanza kuamini UMEPATIA na ushindi wenyewe labda hauna maana ila unauhalalisha kwa kuwa TUNAKUSIFIA!


Ukipatia,.....
... uliyokosea MENGI ni rahisi wengi kuyasahau hasa kama ni kweli tulio wengi bado hatujapatia na wala hatuna astukiaye yetu madogodogo katika jicho la wengi tunayopatia lakini hakuna ANAYETUSIFIA!


Na kwa kawaida jamii imfikiriaye kapatia,...
...jamii huwa haihitaji kujua sana kafanikishaje kupatia ALIYEPATIA kabla haijaanza KUMCHEKELEA ingawa labda kaliza MTU KIBAO katika kufanikisha, na atachekewa na TUTAMSIFIA.

DUH!

Ni wazo TU MKUU!

Swali:
  • Unauhakika ulivyopatia leo itadumu mpaka KESHO?

NIMEACHA wazo!

Hebu tumpate BINTI MACHOZZI a.k.a MANKA a.k.a Lady JAYDEE azungumzie ya -SIWEMA(shebe v mix'd)



Au tu Marquis du Zaire kwa hisani ya TZBOY walete ya -KARUBANDIKA




ASANTENI WADAU WOTE mkiwemo Papaa Hassan na Frateline a.k.a Kada wa CHAMA mliopo katika picha zangu za juzi ya jana...



Photobucket



Photobucket



Photobucket




Photobucket




Photobucket




Photobucket


Photobucket


Photobucket



Photobucket




Photobucket




Photobucket



Photobucket

Read more...

BAADA ya KUKOSEA!

>> Thursday, August 13, 2009

Kuomba msamaha ni KAWAIDA,...
... lakini haifuti kuwa kwanza ULIKOSEA.

Na uwaombao msamaha hata kama wanafikiri wanastahili na ni KAWAIDA,...
....labda wao ndio WALIOCHANGIA kusababisha ukosee au ufikirie UMEKOSEA.


Ingawa kuna wadaio ukikosea kusingizia wengine ni KAWAIDA,...
....labda SI KAWAIDA chaguo lako LA ni nani WAKUMLAUMU au eti tu kachangia kachumbari katika UBWABWA wa lililo kufanya kama sio juzi au jana ,BASI labda leo lililokufanya UMEKOSEA.


Na kabla hujaomba msamaha si lazima hujastukia kosa na labda ni KAWAIDA,...
.... lakini uwaombao msamaha labda wakati huo huo nao ndio kwanza wanaendelea KUKOSEA!:-(

DUH!

Swali:
  • Hivi WAKATI unaombwa msamaha HUWA unajisikia vizuri eeh hata wakati kwa sauti unakiri hutaki kusamehe aliyekukosea ?

  • Unauhakika hukosei kwa kuomba MTU msamaha?

Samahani ni wazo tu MKUU WA MASWALA na NIMEACHA!:-(

Ngojea Dr Alban abadili hali ya hewa kwa kuzungumzia kitu -Born in Afrika



Au tu Dr Victor aturudishe afrika kikweli katika kitu - Kalimba

Read more...

TANGAZO LA KONGAMANO LA KITAIFA LA WANABLOGU TANZANIA









Je wewe ni mwanablogu (Blogger) au mdau wa habari na mawasiliano kwa umma kwa kutumia mtandao? Kama jibu ni ndio, tafadhali unaombwa kujiorodhesha kwa ajili ya maandalizi ya Kongamano Maalumu la Kitaifa kwa ajili Wanablogu (Bloggers) na wadau wa habari na mawasiliano wa Tanzania (Tanzanians Bloggers Summit) linalotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu jijini Dar-es-salaam,Tanzania.

Dhumuni la kongamano hili ni Kuelimishana, Kufahamiana, Kuamsha Utambuzi Rasmi Kuhusu Tekinolojia ya Blogu na Mawasiliano ya Umma kwa Kutumia Mitandao, Kusaidia Utambuzi Rasmi juu ya mchango wa blogu nchini Tanzania kama chombo muhimu cha habari na mawasiliano, Kuelimishana jinsi gani blogu zinaweza kutumika katika kuleta maendeleo katika nyanja za kijamii, kisiasa na kiuchumi, kuburudisha, kukuza utamaduni nk.

Wataalamu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wataalikwa kutoa mada na mafunzo mbalimbali kuhusiana na tekinolojia ya kublogu, zana nyinginezo za mawasiliano mtandaoni kama vile mitandao jamii(social networking), online forums nk.Kutakuwa na vipindi vya maswali na majibu.

Ili kufanikisha maandalizi ya Kongamano hili la kihistoria, kujiorodhesha kwako ni muhimu sana. Muda wa kujiodhoresha ni kuanzia tarehe 12/8/2009 (Jumatano) mpaka 12/9/2009 (Jumamosi) tu.

Kinachohitajika ili kujiandikisha ni :

Jina Lako, Anuani yako ya barua pepe (E-mail), Mahali Ulipo au unapoishi (Nchi,mji nk),Namba ya Simu (sio lazima) na Anuani au URL(Universal Resource Locator) ya blogu yako (mfano www.kongamano.blogspot.com/wordpress.com/.com/typepad nk). Vyeti vya Ushiriki vitatolewa kulingana na habari utakazoziorodhesha hapa.

Unaweza kujiorodhesha kwa kutuma ombi lako kwa barua pepe kwenda; summit@bongocelebrity.com.

Zingatia tarehe za kujiandikisha.

Ni mwezi mmoja tu! Asante kwa ushirikiano.

UMOJA NI NGUVU!

Read more...

Tangazo- ONE GAME PROMOTIONS PRESS RELEASE



TUZO ZA VINARA WA FILAMU 2009 KUWASHIRIKISHA WANANCHI


Mchakato wa kutafuta vinara wa filamu Tanzania kwa mwaka huu utawahusisha wananchi kupitia upigaji kura.

Wapenzi wa tasnia ya filamu nchini watapendekeza filamu ambazo wanaona zinastahili kuingia tuzo za vinara wa filamu. Mbali an wananchi pia kuna taasisi mbali mbali kama vile kampuni ya uhasibu inayotambulika kimataifa litasimamia zoezi la mapendekezo ya filamu. Filamu zenye kura nyingi ndizo zitakazoingia katika tuzo hizi. Pia filamu zitakubaliwa kutokana na mapendekezo ya waandaaji na majaji.

Kuteua filamu ni kwa njia ya ujumbe mfupi ambapo mpenzi atatakiwa kuandika neon vinara kasha jina la filamu anayoipenda na kutuma kwenda 15551 kwa gharama ya Tshs 300.

Vipengele vitakavyowaniwa mwaka huu katika tuzo za vinara ni Mwigizaji bora wa kiume na wa kike wa mwaka, Mwigizaji chipukizi wa kiume na wa kike, Filamu bora ya mwaka, Muongozaji bora wa Mwaka, Mwandishi bora wa filamu, Adui bora, Msanii bora msaidizi wa kiume na wa kike, Mhariri bora wa mwaka, Mtunza Sauti bora, Mtunza Mwanga bora, Mpiga picha bora wa mwaka, Mtayarishaji bora wa filamu, Mtunzi bora wa filamu, Mapambo na maleba bora, msanii maarufu wa kiume na kike na Tuzo ya heshima.

Vipengele vilivyoongezwa ni mtunza taa bora, mtayarishaji bora wa filamu (producer) na wasanii maarufu wa kike na wakiume (People’s choice Award).

Mwaka huu kampuni mbali mbali zimejitokeza kudhamini mashindano haya lakini yatatajwa baada ya upigaji kura

Filamu zinazostahili kupendekezwa ni zile zilizotengenezwa kuanzia januari 2009. Filamu zitakazo ingia moja kwa moja ni zile ambazo bado hazijaingia sokoni lakini yatawasilishwa na watengeza filamu wenyewe.

Zoezi la kupendekeza filamu litafanyika hadi septemba 30 kabla ya kupatikana wahusika kwenye kila kipengele kabla ya wananchi kupiga kura kuwapata washindi.

Khadija Khalili
Mratibu

Read more...

Kuhusu SWALA la uzito wa MOYO!

>> Wednesday, August 12, 2009

Mara nyingi KUHUSU UZITO wa MOYO,...

....huwa kinachozungumziwa ni UZITO wa kukubali HALIHALISI ajisikiayo MTU hata kama kwa hilo itasingiziwa mpaka ROHO!:-(


Na amini USIAMINI wengi waongeleao MAUMIVU YA MOYO,....

....hawaongelei unaodunda MOYO , kwa kuwa kama wanazotuziitazo dini katika maelezo yao watasingizia KWA HILO mpaka ROHO!:-(

Na wakati unaongelea MOYO,...

... kumbuka kwa binadamu humchukua muda kuelewa tokea akizaliwa kidundacho kifuani ni MOYO na hata baada ya kujua atachanganya katika kwake kuapia hata maswala yasiyo husiana na MOYO akaapia kwa moyo KUWA hata HAJAWAHI KUJINYEA wakati hata nia yako YAKUTAKA UKWELI ILIKUWA si YA kumtoa ROHO!:-(



Na usishangae kuwa bado kuna waongeleao ya ROHO wakiwa wanatoa stori za maumivu ya MOYO,....

...... kwa kuwa LABDA wanajua au hawajui kuwa hata wewe katika JEDWALI hujui nini tofauti ya YA MOYO na YA ROHO!:-(




DUH!
NIMEACHA MHESHIMIWA!

Swali:

  • Kwani ulikuwa na miaka mingapi ulipostukia una MOYO?
  • Hivi wewe UNA MOYO KWELI?

DUH!

Ngojea SANCHEZ abadili hali ya hewa kwa kitu -Love is POWER..




Au tu Toots & Maytals ft SHAGGY waongelee- BAM BAM

Read more...

Kuhusu swala la UZITO wa CHUPI!:-(

>> Sunday, August 09, 2009

Kuhusu swala ZIMA la kulalamikia yote ingawa ETI HATA mjanja BADO kunauwezekano hajastukia hata kwenye eneo kuna UZITO wa CHUPI kwenye UCHI!!:-(

NDIO!
Katika maisha ya binadamu kuna mengi MAZITO na unaweza kustukia uzito wa GAUNI kabla ya kugundua hata CHUPI ina uzito hata kama hausikilizwiii na UCHI:-(



Kuna uwezekano mwenye UCHI bado anawasiwasi na HATA yajaayo kwenye UCHI hata kama haijulikani au hatuongelei sasa hivi UJAZO ununiao chupi hata kama kilichonuna sio UCHI:-(




Na kuna uwezekano wasiwasi wote HUU ni kama jeuri tu ya ambaye eti anafikiri wake UCHI NI MZURI ambao ni kweli HAJASTUKIA ukiupa muda HATA MDOMO utanuka ZAIDI kwa kuwa KIPENGELE ukitafsiri ni UCHI!:-(



Hivi unauhakika kwa nia yako ya kuninyima au tu KUTUNYIMA kipengele maana yake SI angalau unataka kujazia angalau UTOKO kwenye kigawio kwa kukisahau kipo au tu kwa kukitunza bila sababu na LABDA HAPA wala hata hatuongelei KIPENGELE , ingawa UNARUHUSIWA KUFIKIRIA hapa labda tugusiacho ni wako UCHI?
Swali:
  • Unauhakika umewahi kufikiria kuwa pamoja na kuuvalisha UCHI KIFUNIKO kwa siku nyingi na hata kama sio SIKU tu leo au tu siku nyingine, ingekuwa wewe si msikiliziaye uzito wa chupi unauhakika ungesikilizia hata UZITO wa KAPTULA kwa kuwa CHUPI YENYEWE TU tayari ni NZITO ingawa unaweza KAMA tu udaivyo kibinadamu LABDA bado hujastukia hata uzito wa MATITI YAKO HATA YA KIUME au chako KICHWA?
  • Unauhakika kuna mtu awezaye kukaa uchi?

DUH !Samahani kwa WAZO!

Hebu nimuachie Bob Marley afanye tena mazoezi katika -Bad CARD



Au turudi tu tena Ivory Coast ALPHA BLONDY aongelee- Brigadier SABARI



ASANTENI WADAU WOTE ingawa baadhi ni hawa kwenye picha zangu....



....MUZEE wa ARUSHA a.k.a DJ Blac ASANTE!

Photobucket


Photobucket


Hariet samahani kwa kukuzidishia Togwa....

Photobucket



Photobucket







Photobucket










Photobucket











Photobucket






Photobucket



Photobucket



Photobucket




Photobucket








Photobucket


Photobucket


Photobucket



Photobucket




Photobucket



Photobucket




Photobucket

Read more...

MAISHA ya kabla ya KIMOBITEL a.k.a SIMU!

>> Friday, August 07, 2009

Ilikuwa KIJIJINI ukimtaka ZUBEDA,...

....HUHITAJI SIMU,.....
....wajua saa za jioni na ndoo hakosekani KisimaNI.


Na giza likiingia akikukubalia zako za kauli JITIHADA,...
...HUKUMBUKI DUNIANI KUNA SIMU,...
... na vile vile wajua hakuna gesti na mambo MPWITO ni VIchakaNI.

Na hata kama uko mjini na nia ni kukutana na KADODA,..
...HUKUHITAJI SIMU,...
...ulijua kama si KONTENA au KIOSKI, kilinge cha kwa fundi viatu HAkosekaNI.

Na yule ANNA totoz la kilokole lisokosa IBADA,...
...YA NINI SIMU,...
... wakati wajua waweza MPAKA liimbia kwaya KA nisaNI?:-(
Na yule MSONGO wa kitabu AHMADA,...
... YA NINI SIMU?...
...ulijua kama sio saa tisa ni saa kumi YU maktaba na sio kwenye mpira KIwanjaNI.

Na kama ni kwa mgonga kokoto Simoni wa MIDABWADA,....
...HUKUHITAJI SIMU....
.... ulijua midamida ukitaka utamkuta akishughulikia mawe huku akitoka jasho MtoNI.

Eti siku hizi kama huna SIMU hata ya kutongozea MWANADADA,...
.. WAWEZA JISIKIA WAHITAJI SIMU...

... la SIVYO wawezashindwa wasiliana na NDUGU na JAMAA achilia mbali kukosa WINDO bila kutumia akili MUKICHWA hata WIndoNI, sokoni na nimatumaini yangu angalau isije kuwa ni hadi NYUmbaNI.:-(




NIMEACHA WAZO MKUU na kama hujastukia , namisi enzi zile ambazo mie Mtakatifu Simon sikuhitaji Simu hata ya Ku-beep a.k.a KUMDIPU kishtobe nibane kwa kucha aninong'oneze nijisikie raha MOYONI !:-(
Swali:

  • Umestukia siku hizi kuna watu wanadai hawawezi kuishi bila SIMU?
  • Hivi nani ka kwambia ili kuishi MTU huhitaji simu?LIONE VILE!:-(
KUMBUKA hili ni WAZO tu MHESHIMIWA na nakutakia mafanikio IJUMAA na WIKIENDI HII chooni!

Hebu WANDA SYKES abadilishe hali ya hewa a.k.a atukane katika- SICK and TIRED[Tahadhari :usimsikilize kama mtoto au wewe ni MHESHIMIWA wa KUKWAZIKA kwa sababu kwa mtazamo fulani ni matusi!:-(]


Au twende tena Ivory Coast tukutane tena na MAGIC SYSTEM waongelee -Premier GAUO.


Au tu 113 na MAGIC SYSTEM walete- Un gaou oran

Read more...

Sababu za BINADAMU kwa ya kibinadamu kumuonea MTU mwenye kasoro za kibinadamu aibu!:-(

Lazima kuna kitu au umefananisha KITU,....
.... la sivyo kubali labda ni udhaifu wa kitu kama wajua hata kama si kiharage wala njegere kuna kitu UNACHO na ANACHO,....

..... sasa aibu yatoka wapi?



Na labda pia kwa kuwa HUNA na ANACHO kitu,....
.....hudhani si utaahira kwa binadamu ajuaye hakuna MTU mwenye yote KUONA haya na hataki tuongelee HATA lisilotia aibu swala la kama HANA au ANACHO ingawa ni kweli hakijamnasia,...

.... hivi hii aibu inatoka wapi?



Kama tu tuumizwavyo na tusi lisilo na maana KAMA LILE limfananishalo MTU na mbwa au KITU,...
....Hudhani swala zima la binadamu kumuonea MTU haya laweza mkosesha BINADAMU raha akakosa la BEBERU kunusa YA MBUZI MIKOJO na kwa hilo LABDA hata mbuzi ambaye haja balehe BINADAMU hatuoneiGELE ,....

..... LOH hivi hawa wanyama HAWANA AIBU au aibu zao ziko wapi?




Na labda aibu za BINADAMU ndio zimfanyazo awe MTU na sio KITU,...
.....Lakini wajua kwanini MARA NYINGI kuna WAONAO HAYA bila mpango na kwa kisichotia hata aibu,...


..... na hivi kweli hizi aibu zatoka wapi?


NIMEACHA wazo na KUMBUKA Kijeba /Kishtobe /Mkuu wa Maswala , HILI NI WAZO TU wala usitishike!


Hebu twende kupata kitu cha enzi hizo kutoka kwa Carl Douglas kiitwacho -KUNG FU FIGHTING


Au tu Gibson Brothers walete kitu cha enzi hizo kiitwacho-Cuba

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP