Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama BADO unataka kuanzisha KANISA, dini AU kutongoza ili ufaidi nanihii ,JIFUNZE saikolojia ya kitu fulani kiduchu!

>> Thursday, June 19, 2008

Udhaifu wa binadamu kichwani , unakautamukake katika swala zima la kuuchezea.
Tatizo ni kwamba , inawezekana anayechezewa MUKICHWA ni mimi na wewe , na ni yule mpendwa NANIHINO ndio anafanikiwa kutuchezea.

Utamu wa kuchezewa akili ni jinsi unavyopunguziwa mahangaiko ya kufikiria mwenyewe katika kufikia hatima ya kustukia kuwa inawezekana ni kweli Maisha ya amani na upendo yanakuwa rahisi zaidi kama katika UHUSIANO wenu na liMPENZI lako , mmoja wenu ni MJINGA .

Swali:

  • Si inasemekana mafahari wawili hawaishi zizi moja?
  • Si ni kweli kama ushaambiwa njia ya kwenda mbinguni ni nyembamba,huna haja ya kufuata njia pana ya ahera ingawa ushastukia njia pana imejaa nanii za kidunia tamutamu sana ingawa nyingine zinaweza zikawa zinanuka?

Sasaa....

Ngoja tujifunze kitu kidogo kutoka kwa James RANDI hasa kuhusu lile swala la kucheza na akili za watu hasa kama wewe unania kama yangu ya KUANZISHA dini....
cheki basi....


Tuendelee..


Nazimia kweli staili ya Peter Popoff ya kuwafisadi wafuasi fulani ambao kwa sababu za kisaikolojia fulani ukiwaelewa,nahisi wanaweza kukusaidia sana katika kupata wafuasi wa dini yako mpya mdau.
AU?

Hebu mcheki kazini....


Pata kidogo dondoo kuhusu BENNY HINN

Basi Mkuu, NAACHA hii topiki...
Lakini....

Swali:
  • Nani kakudanganya kuwa hupendi kudanganywa?
  • Unafikiri huchagui ukweli usiotaka kuusikia; kama ule wa labda umfikiriaye ni baba yako , ukweli ni kaka yako kutokana na kamchezo alikocheza babu?

DUH!
SAMAHANI!
Hebu tumsikilize huyu MVULANA tena akimsimulia mwenyeuke hali halisi...



Kwa wapenzi wa REGGAE MUSIC , jifunzeni ufanisi wa WAIMBA REGGAE kutoka kwa Clint THE DRUNK:-)

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP