Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

TAMUTAMU nyuma ya kauli;''JAMAA LINAPENDA SIFA HILO!''

>> Wednesday, June 25, 2008

TATIZO la kusifiwa ni jinsi utamu wa sifa uwezavyo kufanya ASIFIWAYE kuanza kusahau kuwa binadamu wote duniani kuna kitu washawahi kusifiwa hata kama ni sifa za jinsi wajuavyo kufunga breki ya baiskeli kwa KISIGINO.

Ni udhaifu tu usababishao KASTAREHE au KAUTAMU upatako UKISIFIWA.
NA...
.....ni vigumu kukutana na binadamu asiyependa kusifiwa.

Lakini.....
....INAWEZEKANA mimi na wewe ni wastaarabu ambao hatuwezi kukiri TUNAPENDA SIFA.
Lakini.....
... INAWEZEKANA, anayedai hapendi sifa, hajastukia afurahiavyo sifa hata kama sifa yenyewe ni ya mashavu yake murua kama embe dodo.
SWALI:

  • Hujawahi kufurahia ukisifiwa sifa za uongo?
  • Una uhakika sifa zako usifiwazo ni sifa?

Labda,....
... chochote afanyacho binadamu ni sifa.

Si ulokole, wizi , ufisadi au hata MENO KAMA NGIRI vyote ni sifa vikiwekwa kwenye sentensi fulani?

Chakusikitisha ni kwamba unaweza kujikuta unalazimika kuishi kwa kujaribu kujilinganisha na sifa usifiwazo ambazo hauna.

SAMAHANI!
Nawaza tu hapa!:-(
Hebu tumsikilize I -WAYNE akikiri katika CAN'T SATISFY HER

au tuwasikilize tu Bascom X ft I Wayne, Richie Spice, Chuck Fender & Capleton

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Unknown 12:38 pm  

Sifa ni sifa ila huwezi kulingana na SIFA...

Unknown 12:38 pm  
This comment has been removed by the author.
Simon Kitururu 2:53 am  

@FEDE:Kweli mkuu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP