Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Limtu LIKIFANYA vibaya BILA kukuambia unashuhudia MFANYO mbaya, UTASTUKIA kanyau?

>> Friday, June 27, 2008

Inasemekana unazaliwa na machale!
Kibaya wakistukia.

Inasemekana kitu kizuri hakihitaji kujitembeza iliutamani kukiiba.
Hata hukohuko chini ya uvungu, waweza kukistukia kama wewe muinamaji au muinamishwaji.

SIKATAI!
Labda ni kweli.

Lakini je ni kweli?


  • Wakoloni walipofika kututawala kuna waliostukia pipi na lawalawa nyama zao kuwa si bomba na kuna walozipenda kama KUBWA JINGA.Kuna waliofikiri wanakuwa wakarimu kwa wageni , wakati waliokuwa wanakarimiwa wakitafsiri ni UJINGA.

  • Kuna watu wakamuua YESU ingawa mpaka kesho ya mwaka fulani wapo watakaokiri YESU alikuwa anawafunza mazuri.

  • Kuna wanaona MFAlme MTUKUFU MUGABE anafanya mazuri kupigania kuikomboa nchi yake tukufu ya ZIMBABWE kutoka kwa wakoloni mwaka 2008 , wakati wengine wakimuona nikatili ingawa anabomba la mustachi kiduchu.


Lakini.....

HELLO TANZANIA !

MWALIMU Nyerere mzuri......

...... hivi mtoto azaliwaye leo, atakumbuka alifanya nini ikiwa wakirio kuwa alikuwa mwalimu wao hawakumbuki aliwafundisha nini?

RAIS Mwinyi mzuri.....
..... kwa aliyezaliwa miaka kadhaa iliyopita, anakumbuka aliruhusu nini kama hivi sasa mpaka UFISADI ruksa?

RAIS MKAPA mzuri...
......si tutakumbuka alijenga uwanja wa mpira kwa sababu sisi ni mashabiki wa mpira wa timu za UINGEREZA?

Rais KIKWETE mzuri....
... si nasikia anasura nzuri ?


SASAAA....

Swali:
  • Hivi ni kweli kila mtu anatamani akumbukwe?


Labda ni kweli waliosema TENDA mema na usingoje shukurani walikuwa wana busara ya kustukia kuwa MAOVU yako+ kutenda VIBAYA ndio vyaweza kuamsha MORI wa UMATI wa kutoshukuru .

AU

Labda tutende mema na twende zetu msalani, na kama tutakumbukwa basi isiwe kwa sauti tuzitengenezazo msalani. Si nasikia tuko wengi hatupendi kuonekana tukitoka msalani tukihisi kuna sauti zimesikika katika kuku wengi?


Lakini...
.....napenda jinsi TELEVISHENI a.k.a LUNINGA inavyo tusaidia kutukumbusha kitu kwa kututangazia matangazo yatukumbushayo ngwagulo au HATA NANIHII ni vizuri kwako kununua.SASA nasikia mpaka unaanza kununua mayayi ya kuku wakati mpango wako ulikuwa ni kula MAYAI ya BATA kama kawaida yako.

Nashukuru pia TELEVISHENI , magazeti NA bila kumsahau kipenzi wazamani REDIO vilivyotusaidia mpaka KUGUNDUA MSICHANA GANI NI MZURI kutokana na MASHINDANO ya UZURI ya MISS MBAGA MANKA. Labda sasa hata yule KIGOLI niliyekuwa nammezea mate, sitaki hata kuonekana naye tukifanya shopingi za mitumba.

CHAKUJIULIZA tu .....
  • ....ni vibaya vingapi twafikiri ni vizuri kwasababu tumevisoma kwenye KAMAsutra au tumeambiwa ni ujanja kula mshikaki?
  • Je kuna binadamu ambaye machale yake ni sahihi tu?

Lakini...

Naogopa wasomi!

COMMON SENSE yao ina kuja na shule na uonapo banda yeye anaona gorofa.

Naogopa walioenda shule!
Wanaweza wakafanya wanayofikiri waliyasoma shuleni hatakama hawakuelewa kitabu na mwalimu.


NAACHA
hapa hii topiki nisije nikaanza kukuambia blogu yangu nzuri ,halafu ukaanza kuamini kuwa ni kweli ina ladha ya NYANYA MSHUMAA:-(

DUH!
Nammisi kipenzi changu kingine katika BASS , Mwanadada MESHELL NDEGEOCELLO, msikilize kidogo kama FUNK inapanda akupe SLAP FUNK

Unaweza kumsikiliza Graham Norton kama hutatukanika kama maneno yanaweza kuwa si matusi kama yanaaminika kuwa si matusi(Usicheki kama matusi ni matusi kwako.Na unaweza usijifunze kitu katika kideohiki SAMAHANI!:-(

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP