Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Subiria ANDAZI!

>> Monday, October 15, 2012

 Ila kumbuka tu ...
.....asubiriaye sana Maandazi,...
........ anaweza kirahisi kujikuta kaonja Kitumbua!:-(

Swali:

  • AU?Na katika kusubiria,...
...DAKIKA hugeuka SAA kimsikilizio!
Swali:

  • AU?


Subiria lakini,...
.... kwa kuwa ASUBIRIAYE wali,...
.... YASEMEKANA hata ubwabwa ambao haujaiva kwake unakuwa MTAMU sana tu!


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Nakutakia Jumatatu NJEMA NGULI!


Hebu Lionel Richie aingilie kati kwa- Stuck on YOU Kidum arudishe -Haturudi nyuma
 Stivu na Damiani walete tena historia kwa-Catch a FIRE


   
 Halafu sijui kwanini ...
 ....ila hebu tu Bob Marley azime tu...
....kwa kuweka orijino -SLAVE DRIVER


Ndio,...
........ NIPO!:-(
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:23 am  

Umekuwa kama mwana mpotevu kadoda..nashukuru kama kweli upo.."subiria andazi"..mmmhhh kaaazi kwelikweli

sam mbogo 12:25 pm  

wakati mwingine waweza hata kunawa ila ubwabwa/wali kuula ikawa kazi.Andazi/kitumbuwa kweli husubiriwa sanaa tu ila katika kusubiri kwake kuna mambo mengi tu yanapita mfano,labda unga bado hauja lainika vizuri,au hamila haija umuka!!? kwa kitumbua labda mchele haukusagwa vizuri au mchele bado unachuya,ilimradi subiri subiri ifike.ukipewa andazi/kitumbua kunajambo hujitokeza na kuwa kusubiri kooooote andazi lenyewe lina mafuta mengi? . asante mtakatifu kwa hakika andazi/kitumbua nitamu ila usisubiri sana likapowa linatakiwa kuliwa likiwa bado la motomoto. kaka s.

emu-three 8:27 am  

Ambiere, naona ulikuwa machimbo nini,haya wasalimiwa na wamilimani wote, TUPO PAMOJA

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP