Wakati wa shida raha ipo tu ingawa imezidiwa na shida. Wakati wa shida ingekuwa ni bomba la ujanja kwa mjanja kustukia raha iliyoko chini kidogo ya kipele isubiriayo umalize kuteseka na shida.
Labda Kisaikolojia , inawezekana kuna shida unaipendelea .
Labda....
Ukiona mwenye maumivu anacheka, kuna visekunde kaondoa fikirani katika kiini cha maumivu.
Kuna kipindi masikini hakumbuki umasikini wake kama tajiri awezavyo kutostukia utajiri wake wakati anakufa na kastukia haondoki ng'o na ligari lake mkweche au lile jumba la fedha za wizi.
Kuna kipindi unaweza kucheka baada ya kuanguka kitu ambacho ni kinyume na matarajio ya washuhudiao jinsi ulivyoanguka pale sokoni.
Kuna kipindi unaweza ukamcheka mtu kaanguka kabla ya kustukia kuwa amekufa baada ya muanguko.
BAHATI mbaya......
Kila mtu anashida na labda shida yako ni kubwa kuliko yake kama YEYE aonavyo shida yake ni kubwa kuliko yako.
POLE kwa shida yako!Mwenzio chamoto nakiona na shida yangu!
Baadaye basi!
Tulia na Morgan Heritage wakukumbushe Jamaicakama unaweza kufananisha na hali yaTANZANIA katika wimbo KUNA KITU CHAKUKUFANYA UTABASAMU au Nothing To Smile About
MaDJ wakitanzania waliobobea katika fani ya upigaji muziki (U-DJ) watazindua rasmi kundi ambalo litakuwa linatoa kipaumbele suala zima la U-DJ nchini. Uzinduzi huu wa aina yake unatrajia kuleta mageuzi makubwa katika fani ya muziki na burudani nchini Tanzania. Kundi hili limejifunza na makosa ya baadhi ya makundi ya Ma-DJ nchini na kuunda umoja wa aina yake. Kundi hili la Ma-dj litakalojulikana kama C4 linaundwa na Ma-dj waliobobea na wenye ujuzi wa siku nyingi na wanapania kuuteka na kuleta mabadiliko nchini. Ma-dj hawa kuonyesha kuwa wanayodhamira ya kuuendeleza U-Dj na kuleta mabadiliko, wamenunua vifaa vya kisasa vinavyotumika kimataifa kama vile SERATO na VIRTUAL DJ MIXING SOFTWARE, NUMARK HDX TURNTABLES, Pioneer CDJ1000 MK3, Technics 1200 Turntables na Denon. Kundi hili pia lina maktaba ya muziki iliyosheheni muziki mbali mbali kwa ajili ya wateja wao.
Uzinduzi wa Ma-DJ wa C4 inatarajiwa kufanyika jumamosi 1 Novemba 2008 kwenye Ukumbi wa Little theatre kuanzia saa nne usiku.
Kutakuwa na burudani mbali mbali bila kusahau ma-dj wa C4 watadhihirisha uwezo wao wa kukamua santuri. Kiingilio katika shughuli hii ya kukata na shoka ni kwa 10,000/- tu Kwa maelezo zaidi wasiliana na C4 kwenye barua pepe c4unit@gmail.com. UONGOZI WA C4 DJs UNIT
Tanzania DJs set to launch a DJ Unit in Dar es Salaam
Tanzania is soon to experience the launch of the most versatile local DJs who will take Djing to another whole new level. This most anticipated launch will mark a turn in entertainment and DJ culture in Tanzania. This is the launch of C4 Entertainment Unit in Dar es Salaam. C4 Entertainment is a highly selective, hand-picked group of self-driven individuals yielding vastly specialized talent as DJs. C4 Entertainment diverse roster of outstanding DJs includes both established and emerging talent representing the whole spectrum of the club scene. C4 Entertainment aims to revolutionize Djing in Tanzania and has already acquired the latest DJ Equipment and software. For a start C4 boasts of SERATO and VIRTUAL DJ MIXING SOFTWARE, NUMARK HDX TURNTABLES, Pioneer CDJ1000 MK3, Technics 1200 Turntables and Denon. With a music library that cuts across all the genres, C4 are fully equipped and possess the expertise needed to successfully take over DJing in Tanzania.
The launch is scheduled for Saturday 1st November 2008
at the Little Theatre from 10:00pm.
There will be a Special DJ Showcase by C4 DJs and more entertainment.
All these for only 10,000/- per head For more information please contact C4 on Email:c4unit@gmail.com. C4 DJs UNIT MANAGEMENT
Sinauhakika na tofauti ya utamu wa MCHUMBA wa KUJITAFUTIA ulivyotofauti na MCHUMBA wakutafutiwa.
Labda uzuri wa umuitaye mchumba, ni ile tofauti isababishayo uweze kumtambulisha kirahisi kwa watu fulani kuliko mchumba hausigeli/hausiboi au lile tu limpenzi ambalo unanogewa nalo lakini nishai kuonekananalo mchana.
Swali:
Unafikiri kwa nini umuitaye mchumba anatambulishika kirahisi kwa WANOKO?
Unajua tofauti kweli ya mchumba wa kujitafutia na wakumtafuta mwenyewe?
Lakini... Utamu wa mchumba ni akusaidiavyo kisaikolojia kwa kukutuliza kirohochako kwa kuwa KAKUKUBALIA au UMEMKUBALIA.
Mchumba huyo huyo anaweza asiwe mtamu kama alivyokuwa mpenzi tu kwa kuwa unauhakika amekukubalia na labda hata uoga wa kujamba mbele yake hauna maana sana.
Mchumba wako unaweza hata kutomuonyesha sana yale mapenzi kwa sababu ushamvika pete au ushakuwa na ushaidi kutokana na alivyokupa mpaka siri yake ya kale kaugonjwa kake ka kifafa afanyako siri kwa wengine , na ni vigumu kukugeuka kama tu ulivyomsimulia kaugonjwa kako ka herpes.
Mpenzi wako hata bila kumtambulisha kwa maneno, unaweza kustukiwa na umati kwa jinsi ulivyokuwa huru kumfuta aliponyewa kidogo na bundi , karibu kidogo na pasipoguswa na marafiki wa kawaida ambapo umepagusa kwa uhuru kama wa RAIS KIKWETE kufanya ziara nchi za nje.
DUH!
Mchumba aliyetayari kutambulishwa kwa wakwe na marafiki NI MTAMU kwa sababu kwa kawaida hapendi kufanya kosa la kuaibishwa , kitu kimfanyacho awe MKARIMU ili usije kubadili mawazo.
Kisaikolojia, mtu yeyote aliyekubali uchumba anakaudhaifu ka kwamba amekubali na kwa muda mfupi ni vigumu kukageuza kaudhaifu kwa kukataa.
Swali:
Mchumba ni nini?
Unafurahi eeh ukiitwa mchumba?
Binadamu ni kiumbe cha ajabu! Tokea binadamu ajue kuongea anajaribu kutafutia vitu majina na kujifanya yeye anajina. Swali:
Unajua ingawa unajina lako na unatafutia vitu majina lakini ukiitwa mbwa unaweza kugeuka?
Naacha basi mkuu!Unajua na waza tu hapa!:-(
Wikiendi njema na kama tutajaliwa kinamna, basi tutakutana tena hapa baada ya siku kadhaa !
Kama unanafasi mpate kidogo mgombea umakamu wa rais Marekani, SARAH PALIN
Au rudi kidogo miaka ishirini iliyopita umpate MANU DIBANGO akiwa na binti yake GEORGIA wakikumbuka wimbo uitwao Qui est fou de qui? (Chouchou), waliourekodi wakati GEORGIA akiwa na miaka 7
Unaweza pia ukajikumbusha miaka ya 1950 na JIM Reeves akikuambia FLY AWAY
Basi mkuu ngojea turudi kwa LUCKY dubeatukumbushe BACK to my ROOTS!
Jumatatu basi MUNGU akipenda! Nakutakia kwenda msalani kwema!Read more...
Jambo lako binafsi zuri si lazima likae uchi kwa jamii kushuhudia , kwa jamii matunda yake kushuhudia.
Kitu ambacho hata hakijulikani, chaweza kuwa ni chanzo cha wewe kunichekea au hata kuwa na muda wa kunisaidia , kumsaidia ,kama sio kunionyesha chumba cha kujisaidia.
Tusichojua kikusumbuacho , chaweza kusababisha uwe mkali bila sababu katika kiwanja cha penzi .
Unawezaficha siri kwa kujifanya mzuri, lakini mficha siri hufanikiwa kuficha siri kwa yule tu ambaye si makini.
Siri yako ya KUBANA KIJAMBO, yaweza kujitokeza kwa utofauti wa staili yako ya mkao kwa akujuaye. Siri yako ya kubana mkojo , yaweza kujitokeza katika mwendo wako wakwenda msalani kwa akujuaye. Siri yako wakati unaongea na mpenzi wa siri , inaweza ikawa katika staili yako ya kunong'ona kwenye simu huku ukijichekesha katika visivyochekesha.
Siri yako wakati unadanganya , inaweza ikawa jinsi tu unavyosisitizia hoja kwa akujuaye.
Sasaaaaa.......!
Aina ya siri ni muhimu katika kugundua hata faida za ukubwa wa sehemu za siri.
Cha ajabu.....!
Tanzania mpaka yajulikanayo hunekana kama siri , ingawa wenyenavyo hawafanyi siri kutuonyesha ukubwa wa maeneo wayazungushiayo uwigo kuficha siri.
Pamoja na ustaarabu wa binadamu wengi katika ya faragha kuyaacha faraghani, huhitaji kuvua mtu nguo kugundua walio wengi hawana kificha sehemu za siri au hata imeshindikana kuvaa chupi nzuri.
Cha kutisha ni kwamba , kwa mwendo huu walio wengi watafikia kubakia na siri moja ambayo sio siri ,kwa sababu tayari unaona MATAJIRI na WANASIASA wanajijengea ngome ili wengi wasione kifichwacho kwa siri.
Na...... Wanasiasa wako makini , kutuibia mpaka maini Nasi kwa matumaini , twategemea matatizo yetu watakabili
Labda tuwakumbushe...
Kitu tusichokijua kwa mtu tusiyemjua tunayepishananaye , chaweza kuwa ndio kilichotuhakikishia usalama au kukabwa hata pale sehemu tunapopajua.
Na inajulikana.....
Matajiri wanaogopa masikini na wanahitaji kujua SIRI ya furaha ya MPWEKE apatayo kwa kuiangalia chupi yake yenye rangi nzuri hata kama haitashuhudiwa na kipenzi katika kibanda cha faragha.
Na inajulikana .......
Wanasiasa wanajua kuwa sasa hivi waliowengi wanastukia kuwa hawafaidiki na siasa zao ingawa bado wanadanganyika kirahisi kwa stori za danganya toto ambazo zinakubalika kutokana na kitu ambacho sio siri chenye uhusiano na elimu na umasikini huohuo.
Muhimu kukumbuka kuwa , wenyenavyo hawataweza kufaidi walivyo kuwa navyo kama WASIONAVYOwataendelea kusahauliwa na kuendelea kutembea na siri ya machungu ya kukosa na kuwa na uhakika kuwa wenyenavyo ndio tatizo.
Wanasiasa na matajiri kumbukeni kuwa mtafaidi sana kwa kuhakikisha angalau na wengine wanapata mpatavyo hata kama vyenu bado ni vya dhuluma.
Hakuna atakaye taka kukuvamia na kuhatarisha maisha yake ili akuibie TV yako ya inchi 120 kama angalau anako kaTV kake ka nchi 32.
Utafaidi kutembea na LIFERARRI lako ikiwa angalau na wengine wana vi RAV 4.
Hata pesa za EPA labda hakuna ambaye angefuatilia sana kama watu wangekuwa wamejazwa mapesa angalau ya kuwa na uhakika familia itakuwa poa tu kesho na kesho kutwa, na hata vijipesa vya kuongezea maisha kutokana na kale ka UKIMWI, zipo.
Labda....... Inategemea unaficha nini , kwa umahiri wako wa chaguo la ukubwa wa sehemu za siri kuwa mahiri. Kifichikacho leo , kucha yake yaweza kukiumbua kesho . Ikiwa huna ili, labda lile au kile chaweza kukahidi kuingia kwa ulaini katika pango hilo la siri.
Ukubwa wa jambo la siri waweza kugundulika SIKU ya KUFA kwa NYANI ambapo miti yote huteleza. Swali:
Hivi umevaa chupi nzuri ee?
Hivi unataka chupi yenye rangi nzuri kutokana na yule akusaidiaye kuivua atakavyokujaji kutokana na kificha faragha au pale uianikapo mbele ya macho ya jamii?
Binadamu wenye AKILI TIMAMU ni waoga na ukiwawezesha kuchagua wakuonea, wataonea VIBONDE.
Ni vigumu kwa mwenye akili MUKICHWA kukiri mbele ya NJEMBA afikirialo halitapenda lichukiwe kuwa analichukia. Hata iwe ni kale kabosi kako tu kenye umbo dogo na kwa kisiri unahisi ni kajinga lakini kanaweza kakakufukuza kazi ikupatiayo vipesa vya kutesea binadamu wenzako na kagari kako Mkweche , ikibidi itabidi ukasifie kuwa unakapenda kama sio kukahonga sehemu zako za haja ndogo.
Wapo ambao wanaweza kumtukania MUNGU kama tu wawezavyo kukutukana WEWE na MIMI. Wapo ambao tunaamini hata kumtukana binadamu mwenzako ni UJINGA.
Lakini wengi wapo ambao hata mapenzi ya MUNGU hatuyaelewi lakini hata kujiuliza sana kuhusu Mungu tunaogopa kukufuru.
DUH!
Basi bwana ,labda ni kweli UNAMPENDA MUNGU wako na ni kweli anakupenda ndio maana anakuacha uwe hai halafu MAISHA MAGUMUUUUUUUUUU!
DUH!
Swali:
Si kuwahai ni jambo la kushukuru na wote wajiuao Wajinga?
AU?
Unaweza kumuogopa na kumpenda mtu?
Nawaza tu MKUU na usichukie kama kweli unadai wewe ni MTU wa UPENDO hata kwetu wenye dhambi!
DUH! Naacha!
Ngoja Yvonne CHAKA CHAKA atusimulie jinsi jinsi anavyompenda DJ katika I am IN love with THE DJ Read more...
Upendo wako LABDA unaashiria kuna kitu UNACHUKIA. Upendo wako unaashiria kuna kitu chenye uhusiano na ukipendacho ambacho UNAKICHUKIA. Upendo wako wa vita kama tu nyege yako ya kumfunza adabu NANIHIINO, kuna umlengaye na si kweli kuwa itaondolewa UKAME kwa kumpiga yeyote tu apitaye mbele yako.
KUNA umCHUKIAYE, kuna ukichukiacho ambaye au ambacho ndio kipele kikuwezeshacho kugundua siri ya utamu wa UKIPENDACHO.
Labda itabidi tu ufurahie chuki kwa kukuokoa kutoka katika maisha yakutojua Upendo ni nini.
Labda tushukuru kwa kuwa Binadamu kwa sababu UBINADAmu unatusaidia kushindwa kuelewa hata mapenzi ya MUNGU wa UPENDO awezaye yote aachiapo tuwapendao wateseke na tuwachukiao wawini MAISHA au hata sehemu za siri za tumtamaniye.
Mwenye chuki na MTU au hata CHUPI , ni rahisi kufananishwa na BINADAMU MBAYA. Mtu mzuri anafananishwa na matendo mengi watu waaminiyo ni matendo mazuri kama vile UPENDO au UKARIMU hatakama matendo hayo yanaweza kukuzawadia UKIMWI.
Binadamu huongelea, husifia upendo na amani mpaka anaweza akasahau kuwa mara nyingi ni chuki na vita vilivyomgundulisha starehe moyoni.
Hakuna binadamu asiye na chuki na kitu fulani kama sio chuki kwa MLENDA au LISURA lako ambalo kuna baadhi ya binadamu au hata mbwa waonyeshao dalili ya kulipenda au walisifialo kuwa zuri.
Tusitake kujidanganya.....
Kwa wakristo watakustua kuwa Yesu wa upendo alikuwa anachukia kama kwa Waislamu , Mtume Mohamedi alivyokuwa anachukia .
Wale Miungu wengine ambao baadhi wanasaidia mpaka akina NANIHINO kupaa na ungo pia nasikia wakichukia, hata mvua hazinyeshi pale kijijini kwetu. Swali:
Si ni kweli Mungu wa upendo alianza kuchukizwa na vitendo vya binadamu tokea ADAMU na HAWA?
Sasaaa..... Unauhakika gani kuwa unajua UPENDO ikiwa tafsiri ya UPENDO wa kibinadamu labda wala haifanani na Mungu amaanishavyo kwa neno UPENDO?
SWali:
Unauelewa upendo wa Mungu kama huelewi Mungu muweza yote kuachia uwepo wa chuki?
Unauhakika unauelewa upendo wa MUNGU kama upendo wako mwenyewe unategemea CHUKI?
DUH! Unauhakika hujachukia bado? Acha hizo , nisije nikakuchukiza bure!
Naacha, topiki imenishinda!
Siku njema! Lakini hebu tumcheki huyu jamaa akionyesha upendo kwa OBAMA
au labda tumcheki tu huyu Tembo akimuonyesha upendo Kifaru. Read more...
Labda UNAKUFURU kwa kumsifia HAYATI Mwalimu NYERERE ukikumbuka sifa za Ubinadamu. KWA KIBINADAMU ni vigumu kuona uwepo wa MTOTO bila mchango wa BABA na MAMA. Lakini....
Labda kwa upeo WA KIBINADAMU, ni vigumu pia KUONA uwepo wa NCHI FULANI bila mchango wa MTU FULANI. Lakini..... Binadamu ni MSAHAULIFU na ndio maana stori za MAREHEMU WOTE DUNIANI zikumbukwazo kuhusu MAREHEMU ni NUSUNUSU.
Inawezekana unachokumbuka kuhusu MAREHEMU ni KILE UTAKACHO KUKUMBUKA.
Ubinadamu pia unaweza kuchangia ujue UPANDE MMOJA wa kitu kimhusucho MAREHEMU. Pia inawezekana ujuacho kuhusu marehemu ni kile tu marehemu alichotaka ujue kuhusu yeye kwa kudhani ndio kitakacho kukusaidia au kukudhuru. Inawezekana WAKUSIMULIAO kuhusu marehemu HAWATAKI ujue kitu fulani au kwa mapungufu ya kibinadamu hata wao hawakumuelewa marehemu na ni asilimia kiduchu tu waijuayo kuhusu marehemu. Stori za wadaio kumjua marehemu zinaweza zikawa ni za ubunifu mzuri kutokana na WAPENDAVYO KUMKUMBUKA marehemu.
Swali:
Hujawahi kusikia watu au hata ndugu zako wakisimulia KW MOYO MKUNJUFU kitu kuhusu wewe , kitu ambacho unajua hakina uhusiano na wewe?
Unafikiri kuna mtu amjuaye mtu mwingine kwa uhakika?
Unakumbuka mambo asilimia ngapi kuhusu marehemu wa mwisho wewe kukutoka?
Unafikiri una muda kiasi gani cha kumjua mtu mwingine ?
SASAAAA....... ngoja niseme............
Aliyetutoka kwa kumuita MAREHEMU , twaweza kuwa tunakiri kuwa alikuwa BINADAMU.
Sifa mojawapo ya UBINADAMU ni MAPUNGUFU. ''Marehemu alikuwa MTU mzuri''; ni kauli maarufu MSIBANi au katika kumzungumzia KIPENZI aliyetutoka.
''Marehemu alikuwa MWANASIASA MBOVU''; ni sentensi inayoweza kuvumilika katika kumuongelea marehemu katika baadhi ya vikundi msibani kirahisi zaidi . SIASA nzuri kwa wengine si lazima iwe ni nzuri kwako.
Kuna sifa ambazo akipewa binadamu , kwa wenye kuamini MUNGU wataanza kukosa maana ya UPEKEE wa UWEZO wa MUNGU kama binadamu pia kwa akili yake anatatua na kuona mbele na anastahili sifa kipekee kwa uwezo wake binafsi usiohitaji msaada wa msuli wa MUNGU.
Kuna mambo asifiwayo MAREHEMU ambayo hutokana na UPUNGUFU wa KIBINADAMU wakustukia au kuweza kuona halihalisi bila mchango ambao MAREHEMU AMETOA.
Labda mchango wa MAREHEMU kukupeleka shule ndio umechangia tatizo lako la KUDHANI UNAJUA SANA ambalo litachangia kwenda kwako MOTONI siku ya MWISHO.
Labda mchango wa siasa za MAREHEMU ndio unaoendeleza tatizo lako la kibinadamu la kuamini kuwa binadamu wote si sawa hapa duniani kwa sababu wengine wanatokea nchi ya KIGAGAGIGIKOKO wakati wewe unatokea nchi ya PEMBA.
Labda marehemu anazidi kukuaminisha kuwa nchi zinamipaka hapa duniani na kuwa nyie ni wakarimu halafu wao sio.
Labda marehemu anasababisha TATIZO lako la kuongea KISWAHILI na kuchangia watoto wako wasivyojua KIHAYA kitu ambacho kinahakikishia baada ya miaka kadhaa hakuna atakayejua kuongea KICHAGA.
SASAAAAAAAAAA...
Mwalimu Nyerere hatuwezi kukana mchango wake kwa TANZANIA. Wote tunakiri kuwa alikuwa anaakili sana. Lakini kuwa na akili hakuna maana kuwa alikuwa anajua yote. Makosa yalifanyika kama yatakavyoendelea kufanyika na binadamu wote duniani. Na ni kweli binadamu yeyote mwenye busara na akili atakubali kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa Mjinga tu kama WEWE na MIMI. Swali Unafikiri kuna binadamu hata mmoja asiye MJINGA?
MUNGU amlaze mahali MEMA Mwalimu NYERERE!
Lakini.....
Labda tofauti kubwa kati yake Mwalimu Nyerere , MiMi na WeWe ni kwamba , wote tunajua alijitahidi kufanya kwa vitendo yale aliyoamini kuwa ni ya maana na ya msaada au MCHANGO mkubwa hapa duniani.
Lakini labda MIMI na wewe mchango wetu kwa nguvu ZETU zote kutokana na kaelimu kenyewe, kauwezo kenyewe na kaofisi kenyewe ka mabua tufanyiako kazi, ni kusaidia kuokota tu takataka pale mtaani naIKIWEZEKANA kujaribu KUUJAZA ulimwengu kwa kuzaa kwa mpango ,kujaribu kuelimisha taifa lijalo , watoto wetu au kumpa mimba mtoto wa tajiri ,ili angalau mtoto atokananaye na matendo yetu kwa kisingizio chochote kile AWE na afadhali katika maisha na awe mchango chanya katika DUNIA hii.
DUH! Swali:
Nchi ni nini?
Tanzania ni NCHI au jina jipya lililotungwa na BINADAMU kuwakilisha sehemu fulani?
Watu wa sehemu fulani wana mchango gani katika maana ya neno NCHI?
Naacha!
Tulia kidogo na Muheshimiwa katika jamii , MAREHEMU Richard Pryor akupe maneno ya hekima(usiangalie lakini kama unatafusiri ya matusi kichwani). Read more...
Inasemekana kula UGALI na MAHARAGE kila siku hukinaisha kama tu ukila PILAU au MABIRINGANYA kila siku.
Inasemekana kuwa baada ya kuchoka kula kiporo cha wali na maharage yalioungwa na nazi ya jana uyapendayo,vyakula vyote vitakavyofuatia vitakuwa vitamu na vitakusaidia unogewe tena na wali na maharage ya jana yalioungwa na nazi hapo siku za baadaye.
Lakini... Ukiongelea chakula, labda ni tofauti na ukiongelea binadamu. Inasemekana mapenzi ya binadamu na chakula , yanalemea upande mmoja, kutokana na chakula kutokuwa na kauli kuhusu jinsi gani kinafikiria ukilavyo au ujilambavyo.
Swali:
Katika mapenzi yako , umpendaye ana kauli zaidi ya kudai leo hajisikii vizuri kunanihii?
Unatumia kigezo gani kupenda chakula ambacho hutumii kulipenda LIMTU lako?
Utamu waKIMADA au LILE TU JAMAA ambalo JAMII , DINI au KAUBONGO KAKO kanakukataza KUONJA , kutokana na kukaaminisha KAUBONGO KAKO kuwa JAMII , DINI au KAUBONGO KAKO ni kautamu KALIKOKATAZWA, ni UTAMU tu ambao UBONGO wako unatafsiri kuwa ni tofauti kidogo na kautamu upatako kwa mke au mume wako.
Lakini.....
Si kweli kuwa LIKIMADA lako au LILE LIMTU lalo la nje ni tamu kuliko LIMTU lako LA NDANI.
Lakini......
Limtu la nje linaweza likasababisha unogewe zaidi na LIMTU lako la ndani, kama tu liwezavyo kufanya ukawa unalipa limtu lako la ndani mgongo ukilala na kudai kuwa umechoka wakati unalifikiria na kuliota limtu lako la nje.
Swali:
Sasa utajuaje UTAMU kama hakuna UCHUNGU?
Udhaifu wa binadamu ni pamoja na kuumia roho, wivu na ubongo kujifunza kitu baada ya kugusa moto. Ukigusa moto ukaungua , utataka kuufunza ubongo kukukumbusha usiguse tena moto. Ukionja tamu, utataka uufunze ubongo jinsi ya kupata tamu ili urudierudie kuonja tamu.
Cha kushangaza ni kwamba , ladha chungu unaweza kuufunza ubongo ukaona ni tamu. Ndio maana kuna wadaio kuwa walipoonja BIA mara ya kwanza waliona ni chungu ingawa leo wanadai ni tamutamu kunoga. Labda ndio maana afurahiaye MAZOEZI ukamwambia kuwa anachofanya ni ADHABU , atadai anaumia na haoni tamutamu ya mazoezi.
Swali:
Unafikiri Utamu ni nini?
Unafikiri WAKUBWA wazima wangapi wanaweza kuona maziwa ya MAMA ni MATAMU kama toto lilozaliwa tu na bila aibu linajua CHUCHU inatoa nini?
DUH!
Kama toto lilozaliwa tu linajua maziwa ya mama ni matamu, labda utamu hauhitaji kitu chakufananishia.
Lakini .....
Labda penzi la MUME na MKE linatakiwa liongezewe vikorombwezo kama tu toto linyonyalo liongezewavyo aina nyingine ya chakula jinsi siku zinavyoenda .
Lakini.......
Labda jinsi uongezeavyo vikorombwezo kwenye penzi lako na limtu lako ni sawa tu na jinsi toto uliongezeavyo milo mingine lifanikiwavyo kuongeza UJAZO wa MAVI na harufu ya kinyesi.
Lakini....... Labda WEWE na Penzi lako na LIMTU lako ni tofauti na YULE na LIPENZI lake, na kama upendavyo kubadili vitumbua na kula maandazi siku mojamoja au tisatisa, ndivyo YULE aridhikavyo na UJI wa MIHOGO kila siku.
Lakini....... Labda huwezi kabisa kufananisha mapenzi ya mtu na mtu na mapenzi ya mtu na chakula kama tu ushindwavyo kula mihogo huku ukilazimisha kaubongo kadhanie unakula keki.
Swali:
Unafikiri kuna kitu mtoto anafananisha dunia nacho kimfanyacho akizaliwa tu aanze kulia?
Si inasemekana ukiwa unajichua mwenyewe, kujirutubisha mwenyewe au hata unafanya penzi na usiyempenda, unaweza kujenga akilini picha ya umpendaye kama wafanyavyo baadhi ya MALAYA na siku moja moja unaweza kudakwa kwa kukosea jina la limtu lako kwa kutaja jina la kipenzi chako UKIPENDACHO kikweli MOYONI, AKILINI na ROHONI?
Sasaaa...
KUMBUKA nawaza tu HAPA , halafu Topiki imenishinda!:-(
Naacha basi!
Nakutakia kila la heri ambaye unajua utamu wa aina moja tu!
Nakutakia kila lakheri ambaye unajua tamutamu mbalimbali lakini tamu uliyonayo unaamini itakuwa inanoga hivyo hivyo kubwa kuliko kesho au hata kesho ya mwaka kesho.
Nakutakia kila la kheri ULIYEACHA tamu ya zamani ukidhani TAMU MPYA ni tamu kubwa kuliko na kugundua kuwa tamu ya zamani ndio ILIKUWA tamu HASWA na haipatikani kwa utamu ule tena.KIBEBA TAMU kimeshastukia HUNA MPANGO!:-(
YOTE MAISHA ! SI ndio UBINADAMU AU? BAADAYE BASI!
Nakuacha na zilipendwa kutoka South AFRICA kutoka kwa CHICCO akikuambia WE CAN DANCE
Au ngojea tu Professor Jay akuambie HAPO SAWA. Read more...