Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda UNAMUOGOPA na WALA HUMPENDI huyo MWENYEZI MUNGU:

>> Wednesday, October 15, 2008

Binadamu wenye AKILI TIMAMU ni waoga na ukiwawezesha kuchagua wakuonea, wataonea VIBONDE.

Ni vigumu kwa mwenye akili MUKICHWA kukiri mbele ya NJEMBA afikirialo halitapenda lichukiwe kuwa analichukia.
Hata iwe ni kale kabosi kako tu kenye umbo dogo na kwa kisiri unahisi ni kajinga lakini kanaweza kakakufukuza kazi ikupatiayo vipesa vya kutesea binadamu wenzako na kagari kako Mkweche , ikibidi itabidi ukasifie kuwa unakapenda kama sio kukahonga sehemu zako za haja ndogo.

Wapo ambao wanaweza kumtukania MUNGU kama tu wawezavyo kukutukana WEWE na MIMI.
Wapo ambao tunaamini hata kumtukana binadamu mwenzako ni UJINGA.

Lakini wengi wapo ambao hata mapenzi ya MUNGU hatuyaelewi lakini hata kujiuliza sana kuhusu Mungu tunaogopa kukufuru.

DUH!

Basi bwana ,labda ni kweli UNAMPENDA MUNGU wako na ni kweli anakupenda ndio maana anakuacha uwe hai halafu MAISHA MAGUMUUUUUUUUUU!

DUH!

Swali:

  • Si kuwahai ni jambo la kushukuru na wote wajiuao Wajinga?
  • AU?

  • Unaweza kumuogopa na kumpenda mtu?

Nawaza tu MKUU na usichukie kama kweli unadai wewe ni MTU wa UPENDO hata kwetu wenye dhambi!

DUH!
Naacha!

Ngoja Yvonne CHAKA CHAKA atusimulie jinsi jinsi anavyompenda DJ katika I am IN love with THE DJ

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP