Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KAMA wewe ni PROFESA, unaweza pia KUKUBALI kusema ; ''ZIDUMU KAULI za Rais KIKWETE '',kama ZINAKUKUNA.

>> Thursday, October 09, 2008

Naamini binadamu hupenda asikilizwe na ikiwezekana aeleweke.
Bahati mbaya si wote tumebarikiwa KUJUA KITU na kuweza kufikisha ujumbe ukaeleweka na kukubalika.Ndio maana tuko wengi tunajua kuwa TUNAMPENDA na KUMTAKA yule NANIHINO, lakini jinsi yakumtupia KAULI au hata kumsababisha aje nawe migombani kwa hiari kulionja TUNDA , inakuwa SHUGHULI.

Labda ndio maana utasikia fulani kwa KUTONGOZA au mwanadada yule KWA......KIBOKO , kutokana na kuwa wengine siye, KAULI ZETU hazifiki kwa tumlengae, au zikifika, hazisababishi MTU MZIMA na akili zake aamue kuwa atakuvulia nguo, mpaka KIFICHA MBILIMBI wewe BINADAMU mwenziye BILA HAYA.

LOOOOH!

Swali:

  • Unauhakika ujumbe wako unataka umfikie nani?
  • Wewe kama Bloga unafikiri UJUMBE wako unamfikia nani?
Katika pitapita zangu ndani ya BONGO, hasa katika siku ambazo Rais KIKWETE anaongea, nimefanikiwa kugundua kuwa kuna matabaka mawili yanayo sikia tofauti kauli za huyu Mheshimiwa.

Kuna kundi la waitwao WASOMI na Kuna WASIOTAJWA JINA liashiriyo uhusiano wao na shule au masomo ya shule ambayo sio Elimu Dunia. (Sina maana kuwa kuna UKUTA unaotenganisha makundi haya mawili)

Mara nyingi Kikwete akiongea, nimestukia kuwa kuna ambao watadai kitu kama 'HE DOESN'T SOUND PRESIDENTIAL' na ambao watasikia , ' Umemsikia Kikwete mwenyewe kakuambia KABLA HUJALA lazima ULIWE!'


Kuna kitu ambacho naamini kuwa hata kama humpendi Kikwete inabidi ukichukulie maanani.
JARIBU.... Ujiulize kuwa;
  1. ' Hivi KIKWETE akiongea, anaongea na nani na anayemlenga anafikiria nini?'
  2. Je, anafikisha ujumbe atakao kwa anaowalenga?


Kabla sijaendelea......
' Kuna Rafiki yangu KWEBA pale UHOLANZI alishanikalia kooni kuhusu swala hili, kwa kudai kuwa tokea niko TANZANIA, nimegeuka CCM kutokana na mtazamo wangu kuhusu Kikwete akiongea.'


DUH!
Tuendelee....

Mimi naamini Kikwete ni Rais wa pili Tanzania baada ya Nyerere ambaye anajua jinsi ya kufikisha ujumbe wake kwa anaowalenga.
Lakini KUMBUKA ANAOWALENGA INAWEZA KUWA SIO WEWE.


Na naamini kama wewe ni mwanasiasa Tanzania au tu ni Mtongozaji , jifunze kitu kutoka kwa Kikwete , hasa katika kuchagua unamlenga nani na kujua ni kauli gani utumie ili upewe kifuko cha DHAMBARAU.

Simsifii Kikwete, lakini, asilimia kubwa ya watu kwa uchunguzi wangu ambao wanampigia kura Kikwete , Kikwete anajua jinsi ya kuongea nao na kuwafikishia kauli au hata ujumbe ambao kawaandalia.

Naamini kabisa pamoja na kuwa Kikwete yuko ndani ya Mashine Kubwa iitwayo CCM , ila bado ni mtu ambaye akikupania kuja kukukopa unaweza kumpa pesa yako ya kodi ya mwezi ujayo kwa kuamini kuwa baadaye kidogo atairudisha.


Asilimia kubwa ya niliokuwa nawatolea macho na kuwadadisi ambao ndio wapiga kura , watakuambia , hakuna mwanasiasa ambaye amebakiza Uraisi/Raisi au amelikuwa Raisi, ambaye yuko hai Tanzania, ambaye anaongea lugha yao na wanamuelewa kuliko Kikwete hivi sasa.

Profesa Lipumba na wengine wengi , kuna watu kibao niliokutana nao na kuwasikiliza kutoka vijiwe vya kila aina vya watu wa kawaida ambao ndio wapiga kura ,watakuambia husikika kama MWALIMU FULANI ambaye unasubiri tu kipindi chake kiishe anaongea na anachoongea hakikuingii MUKICHWA.

Ndio kuna watu kama Kabwe ambao wanajua kulistukia kundi walilengalo na wakajua nini na kwa staili gani watafikisha ujumbe, lakini staili ya Kabwe imekaamkao wa kunoga ukiwa nje ya Mfumo . Inaweza ikawa ngumu Kabwe akiwa Rais Kabwe au kama tu Mchungaji Mtikila baada ya kamuda fulani kuongezea maji juisi.

KUMBUKA sijasema FIKIRA za Raisi KIKWETE zidumu, lakini nafikiri kuwa unaweza kujifunza kitu hata kama wewe ni mtaalamu wa mambo ya siasa hapo Chuo kikuu kwa kumsoma tu Kikwete Hata kama ni kweli hukubaliani na aidia ya RAIS MSHIKAJI!

Sina uhakika lakini kuwa wanasiasa Tanzania huwa wanatumia WATAALAMU au UTAALAMU katika kujaribu kuangalia kundi walitakalo na jinsi ya kulifikishia UONGO au huwa wanabahatisha tu .

Naanza kuamini Mchungaji Mtikila hatumii utaalamu ndio maana kwa navyojua uwezo wake WAKUFIKISHA UJUMBE ulivyokuwa mkubwa , UJUMBE wake hata kama ule wa chuki kwa aliowaita jina ambalo laweza kuchukuliwa kama tusi ,'MAGABACHORI 'hauwafikii tena walengwa na makali yake kutokana na KUBAHATISHA KWINGI , kutegemea sana HISIA na kutokuwa na kundi maalumu lilengwalo.

Sawa, unaweza kusema kuwa ukiwa mwanasiasa Tanzania ,WALENGWA wako ni Watanzania wote.


Lakini jiulize kitu ......

  • Unafikiri Watanzania wote ni sawa?
  • Unafikiri Kikwete anaathirika nyie wasomi mkidai kuwa anapigaalinacha na anaongea kama mtoto wa kijiweni tu ?
  • Unafikiri Watanzania waliowengi wanaelewa hata kuwa Rais ni timu na sio mtu mmoja?
  • Unafikiri Watanzania wangapi wana DATA ambazo zinaweza kuwajulisha kuwa unawadanganya hata UKIWA unajulikana kama Mengi na unadai utawajaza MAPESA?

DUH!

Ngojea niache hii topiki.

BAADAYE BASI!


Lakini kama unanguvu kidogo ......

Katika pitapita nilikutana na hawa Taifa la kesho...
Photobucket
Mitaa ya Sinza
Photobucket
Huyu Dogo aliniua kwa jinsi alivyo zama kwenye kitabu. Mpaka msamaria mwema akamuomba aende akasome nyumbani maana atagongwa na magari.

Photobucket
Mitaa ya Mikocheni.
Photobucket


Ndio, nilikuwa na Bajaji kama kawa.......
Photobucket

Photobucket


Nilifika Bagamoyo kwa JHIKOMAN pia.
Mpate kidogo akiwa nyumbani na marafiki.


Ilibidi niguse bahari kwa upande wa Bagamoyo kiduchu pia.....



Photobucket
Nilikutana na Ogola .-Holiday Inn

Photobucket

Photobucket
Michuzi -kwa Wachina akiwa na LadyJAYDEE

Photobucket

Lady
Photobucket
Machozi Band

Photobucket

Photobucket

Photobucket
Agapiti

Photobucket

Magusa

Photobucket

Photobucket
Machozi Band


Swali:
  • Hivi unauhakika Profesa unayemuita Profesa anajua nini?
  • Ushawahi kukutana na Profesa mjinga?


Nakuacha na Talib Kweli akikupa kitu Hostile Gospel

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP