Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Uwezo na Mapenzi ya MUNGU katika kumsaidia MWIZI kuiba, MZINZI kuopoa NGOMA au Mfuata dini KUFARIJIKA leo na ahadi za akishaKUFA.

>> Monday, October 13, 2008

Tusichojua TUMSINGIZIE MUNGU!
AU?

Labda ni mapenzi ya Mungu mimi na wewe hatujui!
Labda ni mapenzi ya Mungu kuwa hakuna asiyeugua!
Labda ni mapenzi ya Mungu wewe na mimi hatuna kile na tuna hiki.

Lakini utamu waulichonacho INGAWA UPO , labda unapatikana zaidi pale ukijua uchungu wakutokuanacho.

Kwa akili za kibinadamu , labda Mbinguni kunavutia kwa sababu tu unaamini au hata kujua kuwa duniani kunatesa au KUNA MAPUNGUFU. Na labda kama unanogewa na ya dunia, unaweza usivumilie UCHUNGU wa mbinguni ambao kwa wengine ni UTAMU.

Inawezekana kabisa kwa upeo wangu na wako wa kibinadamu kwa matumizi ya huu huu ubongo UTAFSIRIO kuwa CHIPSI MAYAI ni tamu, MBINGUNI KUNABOA.

Au......

Labda wanasayansi wanasema kweli kuwa mwili wa binadamu bila kusahau UBONGO wa BIN ADAMU ndio unatafsiri sana jinsi unavyojinoma au kuumia hapa duniani. Kemikali na homoni zinasababisha upende, unogewe au hata utake zaidi kunanihiii, bila kusahau jinsi MISHIPA ya FAHAMU (nerves) iunganishavyo UJUMBE MWILINI, mpaka unaweza kujisau kuwa utamu wa ngono, kutekenywa au hata chakula UKO kwenye UBONGO na sio kwenye sehemu zako za faragha, kwenye kidongoloso au kwenye ULIMI wako uutumiao kulamba nanihii.


Sasaaa......

Tunachojua ni kwamba, MIMI na WEWE tukifa, MWILI pamoja na UBONGO utarudi kuwa UDONGO. Inamaana karibu kila utumiacho , kupapasa , kuonja kuibia, mpaka kikusaidiacho kutafsiri kuwa wewe KIBOKO na mambo yako kwa tafsiri yako ni MSWANO , kitageuka KUWA udongo na labda kitakuwa kinarutubisha tu mazao fulani kama tu MBOLEA ya MAVI YA KUKU.


Lakini.......

Tunachosikia ni kwamba, binadamu ana ROHO .
Tusichojua ni jinsi gani roho inatafsiri UTAMU au UCHUNGU ikiachana na hilo LIMWILI LAKO au LANGU ambalo tunalazimika tulichambe baada ya kwenda HAJA KUBWA.!

Swali:

  • Unafikiri roho ya binadamu inajua utamu wa BIA, Ngono au utamu wa kumpiga mwenzio?
  • Kama wewe ni mwanamume au mwanamke , unajua uhusiano wa kutaka kwako sehemu za siri za wenzio ufanyikavyo UBONGONI na UONGEZEKO wa mjao wa damu katika sehemusehemu zako za faragha?


Lakini tusiyojua anajua MUNGU!


Narudia kinamna.........

Mapenzi ya binadamu matamu na yanaweza kukusaidia kupata GONO.

Kama wewe ni mwanasayansi utadai kuwa unajua kuwa kemikani na homoni zako ndio zinazosababisha uhisi utamu au uchukie kutokana na tukio.

Kama wewe unaamini katika sayansi utadai kuwa ni kemikali na hormoni mwilini na ubongoni ndio visababishavyo uingie ukichaa wa KULIPENDA na KUENDELEA kukaa na LIMTU LAKO ambalo limesababisha uone ni kitu cha kawaida na ni USAFI kugusanisha VIKOJOLEO VYENU ingawa unadai MKOJO ni uchafu na harufu ya mkojo unaichukia kama tu HARUFU ya SAMAKI MAREHEMU mwenye mafinyofinyo.

lakini.....

Utafiti wa mambo ya ubongo unaonyesha kuwa wale binadamu waitwao wanaakili sana au Majiniasi, bado wanatumia sehemu ndogo sana ya ubongo.

Na inasemekana watumiao UBONGO wakipata jibu la swali, huacha kumlaumu Mungu kwa hilo.
Malaria huacha kuonekana kuwa anayeumwa kalaaniwa , wanampa Kloroquini au hata Muarubaini CHAUMBEA na anapona. Inawezekana pia anayeumwa kichwa akapewa tu dawa na bila ya watu kukumbuka kuomba Mungu amponye. Hata yule kibibi mwenye macho mekundu asingiziwaye uchawi kwa sababu jirani yake ana ukoma, husamehewa chanzo cha kuwa kwake na macho mekundu kijulikanapo, chanzo cha UTASA kijulikanapo kuwa si kweli KALOGWA ndio maana HAPATI MIMBA, na ni lidume lake NDILO linafyatua risasi tupu.

Swali:
  • Si inasemekana Mungu ndiye aliyeruhusu Magonjwa duniani kutokana na upotofu wa binadamu?
  • Ukisha muombea mtu apone kwa Mungu halafu akafa ingawa hukutaka afe, sini mapenzi ya MUNGU?

Lakini tusiyojua anajua MUNGU!



Binadamu ni kiumbe cha ajabu na kigumu kukielewa ujenzi wake kama tu SISIMIZI au MENDE na ujuzi wao wakustukia ulipoacha kiporo tamu tamu ingawa huoni pua zao.

Sawa basi.......!
Labda ni kweli binadamu ndio kiumbe BAABU KUBWA kuliko MENDE ,kwa mtazamo wa binadamu, ingawa hata ndege wanatushinda kwa ujuzi wa Jiografia ya dunia. (Si unakumbuka kuwa ndege wamekuwa wanasafiri kutoka bara moja mpaka jingine kwa miaka kibao kabla hata binadamu hawajajua kuwa Dunia imegawanyika katika mabara na ni ya mviringo?)




Lakini........

MUNGU ni MKUBWA!
Labda ndio maana mambo yakitushinda siye binadamu , tunadai kuwa ni MAPENZI ya MUNGU!

Na ni kweli MAPUNGUFU ya binadamu ni makubwa kiasi kwamba , BINADAMU kumuelewa BINADAMU mwenzie IMESHINDIKANA.

AU?

Swali:
  • Kama unaamini MUNGU anajua yote na amepanga yote, UNAUHAKIKA gani hajapanga kuwa MIMI na WEWE tutaenda jehanamu, kama unaamini kuna jehanamu?
  • Unapozungumzia mapenzi ya MUNGU , UNAUHAKIKA unayajua mapenzi ya BINADAMU?
Lakini tusiyojua anajua MUNGU!

Ila kama wewe huamini MUNGU, labda tusiyojua tutajua kesho!

Tatizo ni......

Hatujui kama tuna kesho.


Kwa hiyo, labda ndio IMETOKA HIYO ,kama hujui na wala hujaonja.

Na labda kama hujui na hujaonja ndio imetoka hiyo, kwani hautakuwa na kitu cha kufananishia kautamu au kauchungu upatako.

Kama hujawai kuonja vitu viwili na hauna cha kufananisha, labda ni kitu kizuri kama uambiwavyo kuwa SUBIRI mpaka UOE ndio UONJE WAKUBWA waonjavyo KWA KISINGIZIO cha KUTAFUTA MTOTO au kiburudisho.

Swali:
  • SI kuna dini maarufu zishaurizo kuwa UKISHAOA hakuna kuliacha hilo LIMTU katika SHIDA na RAHA, na kama ni maandazi na chai ni mwiko kutaka kuonja togwa kwa vitumbua?


Lakini tusilo lijua , ANALIJUA MUNGU!


Na kama kuna mbinguni , labda tujuavyo VITAKUFA na LIUBONGO hili lisababishalo tufikiri tunajua.

DUH!
Naacha hii topiki!

Ngoja nikakague Nyati kidogo.........(usishuke mbugani kama mimi nilivyofanya lakini)


Asanteni tena WADAU!
Baadhi ni hawa katika picha zangu ambao hamkunitenga.....

Photobucket
Stephano


Photobucket

Super Ngedere

Photobucket

Danny

Photobucket
Jacky


Photobucket
Vitali MAEMBE Nanenane MORO

Photobucket
Vitali- Bagamoyo

Photobucket
Jonas na Salim- ZE CLUB , Morogoro
Photobucket

JHIKOMAN


Photobucket
The CHEF--Peace of Mind

Photobucket

Morogoro

Photobucket
Bagamoyo

Photobucket
Dada Yulia

Photobucket
Heri na Mrinde

Photobucket
KC Msiba

Photobucket
Mhina wa Tanzanite na DJ Peter Moore
Photobucket
DJ Peter Moore kazini
Photobucket
Tanzanite Band kazini- Mzalendo Pub, Millenium Tower

Nakuacha na muziki aina ya QAWWALI ukiletwa na USTAD NUSRAT FATEH ALI KHAN akikupa kibao ALLAH HOO au GOD is ONE.


AU ngoja tu PUBLIC ENEMY wakupe HE GOT GAME

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP