Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

HAJA ya HAMU ya KUWA na HAMU!

>> Thursday, October 30, 2008

Binadamu na hamu
Haja na Binadamu

Kifurushi cha haja
Kifuko cha hamu
hamu ya kuua haja


Mwenye jungu la hamu
ni mchaguzi wa haja

Haja kutenda cha haja
matokeo hayati hamu ya haja

Haja ni kuamka
kufa nusu ni kulala

Hatua ni kukaa,
haja ikiwa kusimama.

Haja kama ni kutembea,
ujanja hamu kutambaa.

Haja na hamu ni kukimbia
mwenye busara kasimama.

Hamu na haja ni kusimama
mchovu kakaa.
Aliyepata..........
kalala!
Asiyepata..................
kalala!

Kwa mchovu haja ni kulala,
na kufa nusu ni kulala.

Hamu ya mkwepa kufa,
siri ya muendekeza hamu ya haja.

Hayati mjaa haja na hamu
Kifo si cha haja wala hamu.
----------------------------------------------------------------------------------
USITISHIKE usiponielewa !
Labda huna HAJA ya kujua ninaongelea nini ingawa una HAMU yakujua naongelea nini!:-(


BAADAYE BASI!

Tulia na THE KNUX ft SYMETRIX live


AU ngojea DJ DOPE amuongeleshe MALCOM X

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MARKUS MPANGALA 11:34 am  

malcom X jamani jamani... mmm OBAMA je haiwezi kuwa kama huyu?

Simon Kitururu 12:05 pm  

@Markus:Obama Mpole halafu nadhani wako katika kipindi tofauti kihistoria.

luihamu 7:02 am  

mkuu hilo shairi naliforward kwa Anti Serina.

Simon Kitururu 1:02 pm  

@Rasta:Poa tu Mkuu!

MARKUS MPANGALA 5:26 pm  

jamani vipi kama Malcom X angelikuwapo au angeliachwa(bila kuuawa) hadi kipindi hiki ingekuwa vipi????

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP