Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NDANI ya sekunde fulani TANGU nilipoandika MARA ya MWISHO hapa KIJIWENI!

>> Sunday, October 05, 2008

Mambo vipi wadau!
Shikamoo wakubwa!

Nimerudi kinamna!
Nimejifunza na naendelea kujifunza kinamna.
Nilifurahi , kusikitika na kutokuwa na uhakika wa nini mshawasha kinamna.
Nilifiwa na kushuhudia waliozaliwa kinamna.


Ngoja nikuache na baadhi ya picha za msiba wa babu yangu aliyefariki akiwa na miaka 105.

Photobucket

Bibi akimuaga BABU kwa mara ya mwisho.

Photobucket

Photobucket

Mpaka sasa nimefanikiwa kutembelea Mikoa TISA ndani ya BONGO nyoso.

  • Dar es Salaam
  • Morogoro
  • Kilimanjaro
  • Pwani
  • Dodoma
  • Singida
  • Tabora
  • Shinyanga
  • Mwanza
Kwa ambao hamjafika kwa muda mrefu, kuna mabadiliko mengi karibu kila sehemu ndani ya BONGO.

Yapo mazuri na mabaya kama ......

Tofauti ya masikini na tajiri inazidi kukua.
Simu za mkononi si ajabu kuziona mpaka vijijini.
Barclays Bank inashindana na benki za Kitanzania mpaka kijijini kwenu na huwezi kumtisha mtu na Credit Card yako.

Kwa Dar es Salaam si muda mrefu kutakuwa na Wachina wafundishao watoto wako TUISHENI ya lugha ya KISWAHILI. Kwani sasa kuanzia Wamachinga, Mwenye Baa ya kwenye kona ya mtaani kwenu, mpaka mwenye kumiliki migodi, tayari anaweza akawa ni yule Mchina uliyempita bila kumuangalia juzi kwa kisingizio huvutiwi na Wachina hata ukiwa unaota zile ndoto uotazo wakati muda mrefu umepita bila ya kutekenywa, kuguswa, kufanya mazoezi ya kutengeneza watoto au hata kuvunja amri fulani iliyokatazwa kwenye baadhi ya vitabu maarufu vitakatifu na YULE .

Swali:
  • Hivi ni kweli asilimia kubwa ya watu weusi hawavutiwi kimapenzi na Wachina ?
  • Hivi unavutiwa na bidhaa za Kichina lakini eeh?

Nitaendelea zaidi kukusimulia kuhusu BONGO baadaye!



Hebu pumzika na Ryan Leslie akiwa Studio akikutengenezea kibao DIAMOND GIRL

Dar es Salaam BAJAJi kibao kama unaogopa taxi na ndio usafiri wangu...
Photobucket

Baadaye basi!

Asanteni wote ambao bado mnanitembelea hapa kijiweni!

Asanteni marafiki wote !

Nitaweka baadhi ya picha zenu niliokutananao baadaye!

Tulia na ASA basi akukumbushe JAILER

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Subi Nukta 1:02 pm  

Pole kwa msiba Kaka.
Apumzike pema Babu.
Ninakutakia safari njema na ya salama.
Asante kwa taarifa!

Simon Kitururu 1:14 pm  

@Subi:Asante sana!Nashukuru bado unanitembelea hapa kijiweni!Siku njema !

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP